Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

- Mkuu I beg to differ mkuu, Mwakyembe ni PhD wa sheria, sasa inapokuja masuala ya sheria yes anayo authority tena kubwa sana ya kumuuliza form four leaver yaani mkuu wa Traffic wa mkoa kama kweli ana uwezo mkubwa kuelewa sheria kuliko yeye, hii ni fact sio matusi wala kejeli,

- Na uliyoyasema kuhusu Komando, kwa kweli hayana uhusiano wowote na utendaji wake wa kazi kwa taifa, huyu amekua ni baadhi ya wananchi wachache sana wachapakazi kwa taifa letu, wasiokuwa wezi na waaminifu.

Respect.

FMEs!

Mkuu
Nami naomba kutofautiana na wewe kidogo,jamaa hawa wameenda mafunzo kwa ajili ya kazi hiyo, naimani kubwa japo sio kwa 100% hakuna chuo kikuu ambacho Mwakyembe amesoma ama ana Phd ya usalama Barabani wenda hata certifate hana kwanamna nyingine ni BIG ZERO kwa mambo ya sheria barabani.

Sasa yeye kuhoji usomi kwa polisi ni kwa reference ya elimu ipi? kama sio zarau.
 
Mkuu
Nami naomba kutofautiana na wewe kidogo,jamaa hawa wameenda mafunzo kwa ajili ya kazi hiyo, naimani kubwa japo sio kwa 100% hakuna chuo kikuu ambacho Mwakyembe amesoma ama ana Phd ya usalama Barabani wenda hata certifate hana kwanamna nyingine ni BIG ZERO kwa mambo ya sheria barabani.

Sasa yeye kuhoji usomi kwa polisi ni kwa reference ya elimu ipi? kama sio zarau.

- Sheria ni sheria, sijui kama Mwakyembe amesomea sheria za Ikulu, lakini najua for a fact kwamba mara kwa mara hutumwia sana na rais pamoja na Ikulu kuhusu ishus za kisheria nzito za kitaifa, ninaamini akipewa articles za sheria za bara bara atazielewa kwa haraka na kina zaidi kuliko hao maofisa wa Traffic, hili sidhani kama ni gumu kulielewa.

- Labda alamumiwe kwa mapungufu yake mengine, lakini hili la umahiri wa sheria, Mwakyembe yuko juu katika taifa letu!, kama sio yeye kule EAC tungeingia kichwa kichwa na kuishia kuumia kama ile miaka ya zamani! siasa za Kyela sizijui lakini ninajua authority aliyonayo Mwakyembe kisheria bongo.

Respect.

FMEs!
 
Mkuu kwa hili? sidhani..wenyewe wana matangazo yao, kuna bwana mmoja anaitwa FATAKI, na wamemhusisha na wakina baba wanaobeba vibinti vya shule na kisha kuwafanyia mchezo mbaya...maana yake ni kwamba itaendelea kuwa vigumu kwa wenye magari binafsi kubeba wanafunzi kwa kuhofia kuitwa mafataki!

Kaizer,

Kuna nchi HITCHHIKING au Autostop ni MARUFUKU. Wanatengeneza utaratibu ili iweze kujulikana nani anambeba nani. Hii huondoa utata hapo mbeleni kwamba baba fulani anatumia watoto wa shule kwani kwa utaratibu huo, anapangiwa watoto na watu wazima. Na zinaweza kuwepo kadi special na scanner na serikali inagharamia ili kila anayebeba au kuingia kwenye gari, anakuwa scanned na anapotoka ku scan tena. Kwa mpango huo, itajulikana fulani siku fulani alikuwa kwenye gari fulani kuanzia saa fulani hadi fulani.

Mbona Maumba aliwatumia watoto wadogo kwa ingawa alikuwa fundi cherehani, je mafundi cherehani wote wamekuwa waovu? Mwanaume mmoja akibaka, basi wanaume wote tukatwe KIFAA CHA KUBAKIA? Au Wanaume wote tuondolewe karibu na watoto wa Kike? Watu kama hawa siku zote walikuwepo, wapo na wataedela kuwepo. Ni sehemu ya jamii na lazima kusolve tatizo na watu watakaotaka kusaidia kubeba watoto/watu wazima kwenda mjini basi wafanye hivyo.
Nina wasiwasi inaweza kuwa ni mbinu za wenye daladala kwani wengi wakibeba watu basi soko lao linaweza kuanza kuwa katika hali ngumu. Haya mambo inabidi kuyafanyia uchambuzi mzuri na migambo imara kabla ya kuanza. Ndiyo hiki tunasema Kikwete anaogopa kufanya mambo siyo popular. Ni kujaribu tu ingawa hakuna uhakika kama utafanikiwa. Usipojaribu, amini usiamini utakuwa siku zote palepale.
 
- Sheria ni sheria, sijui kama Mwakyembe amesomea sheria za Ikulu, lakini najua for a fact kwamba mara kwa mara hutumwia sana na rais pamoja na Ikulu kuhusu ishus za kisheria nzito za kitaifa, ninaamini akipewa articles za sheria za bara bara atazielewa kwa haraka na kina zaidi kuliko hao maofisa wa Traffic, hili sidhani kama ni gumu kulielewa.

- Labda alamumiwe kwa mapungufu yake mengine, lakini hili la umahiri wa sheria, Mwakyembe yuko juu katika taifa letu!, kama sio yeye kule EAC tungeingia kichwa kichwa na kuishia kuumia kama ile miaka ya zamani! siasa za Kyela sizijui lakini ninajua authority aliyonayo Mwakyembe kisheria bongo.

Respect.

FMEs!

Mkuu
tatizo langu na Mwakyembe sio usomi wake jamaa ni kichwa kweli na ni mzuri sana ktk elimu lakini mimi beef langu kwake ni kututisha kwa elimu yake .
Harafu kingine lile jimbo la kyela limemushinda awaachie vijana chipukizi waliendeleze vizuri na hatimaye Tz nzima .
 
Mkuu
tatizo langu na Mwakyembe sio usomi wake jamaa ni kichwa kweli na ni mzuri sana ktk elimu lakini mimi beef langu kwake ni kututisha kwa elimu yake .
Harafu kingine lile jimbo la kyela limemushinda awaachie vijana chipukizi waliendeleze vizuri na hatimaye Tz nzima .
MkamaP,
Lakini ombi lako sii ndio kazi wa wapigakura?..
Unajua tukianza kuzunguka sana tutapoteza mwelekeo.. Hizi habari za yeye kushindwa Kyela naweza kuesema unatumia ujuzi fulani kuelewa hayo..Unaweza kabisa kutumia kuishi kwao Kyela kuwa sababu na mimi sina sababu ya kusema unanitisha na kuishi Kyela?..tutafika kweli!

The guy is educated hivyo hawezi kukubali ujinga ujinga unapotumika hasa na vyombo vyetu vya usalama. Mwakyembe ni mmoja wa viongozi wetu ambaye anakemea UOVU, vitu ambavyo sote tunafahamu vinatendeka nchini na vipo vinaathiri mamillioni ya wananchi. Ikiwa leo Mwakyembe anakatazwa ama kukataliwa kutoa ushahidi fikiria wewe mlalahoi itakuwa vipi..kumbuka ya baba yake AC.. mke wa Mwaikambo, dereva wa Sokoine, yaliyomkuta Mama yetu mama Mbatia, Wangwe na kadhalika ushiahidi wote umetungwa na vyombo vyetu wakati hatuna vifaa kabisa.. Elimu ya mtu bila vifaa vya kutendea kazi ni kudanganyana..Ni upigaji RAMLI hakuna zaidi ndio maana hakuna haki hata kidogo.

Hakuna mtu aliyesema Polisi wetu hawakusomea sheria wala hawafahamu sheria za barabarani.. Ila unapojaribu kutomhoji victim wa ajali na kuanza kutunga ushahidi kwa kutumia cheti chako bila kuelewa historia nzima ya ajali ni kuepuka ukweli..Hivyo hata Mwakyembe ana haki ya kutumia cheti kuhoji uhalali wa report hiyo.

Hata iwe Marekani au wapi ni lazima ushahidi ndio hutengeneza vipimo vya ajali au mauaji..Siku zote swala lolote huanzia na mtu aliyeona au kuwepo ktk tukio hilo kisha hapo ndipo hujengwa kilichotokea na sii kinyume..
 
Mambo mawili naweza sema kuhusu hili.
1. Watanzania hawawezi tena kukubali kazi zinazofanywa kisiasa tu badala ya kitaalamu. Bora Polisi wafanye kazi yao kama inavyotakiwa.
2. Wasiwasi wa Mwakyembe kwamba yawezekana lori lilitaka kumdhuru makusudi ameuelezea vizuri. Kama kuna wanaodhani kwamba watatumia tena njia ya kuua kila anayetaka kuipeleka nchi yetu kwenye maendeleo ya kweli na ya wote, yafaa wagundue kwamba wanapambana na watu wengi na safari hii hawataweza kushinda. Kama wana akili bora wachague kubadilika taratibu, wataishi - kama utawala wa ufalme Uingereza - vinginevyo watashangaa si siku nyingi watakapoathiriwa vibaya -kama ilivyotokea kwa wafalme wa Ufaransa. Historia, ndugu zangu, ni kitu kitamu sana.
 
Kaizer,

Kuna nchi HITCHHIKING au Autostop ni MARUFUKU. Wanatengeneza utaratibu ili iweze kujulikana nani anambeba nani. Hii huondoa utata hapo mbeleni kwamba baba fulani anatumia watoto wa shule kwani kwa utaratibu huo, anapangiwa watoto na watu wazima. Na zinaweza kuwepo kadi special na scanner na serikali inagharamia ili kila anayebeba au kuingia kwenye gari, anakuwa scanned na anapotoka ku scan tena. Kwa mpango huo, itajulikana fulani siku fulani alikuwa kwenye gari fulani kuanzia saa fulani hadi fulani.

Mbona Maumba aliwatumia watoto wadogo kwa ingawa alikuwa fundi cherehani, je mafundi cherehani wote wamekuwa waovu? Mwanaume mmoja akibaka, basi wanaume wote tukatwe KIFAA CHA KUBAKIA? Au Wanaume wote tuondolewe karibu na watoto wa Kike? Watu kama hawa siku zote walikuwepo, wapo na wataedela kuwepo. Ni sehemu ya jamii na lazima kusolve tatizo na watu watakaotaka kusaidia kubeba watoto/watu wazima kwenda mjini basi wafanye hivyo.
Nina wasiwasi inaweza kuwa ni mbinu za wenye daladala kwani wengi wakibeba watu basi soko lao linaweza kuanza kuwa katika hali ngumu. Haya mambo inabidi kuyafanyia uchambuzi mzuri na migambo imara kabla ya kuanza. Ndiyo hiki tunasema Kikwete anaogopa kufanya mambo siyo popular. Ni kujaribu tu ingawa hakuna uhakika kama utafanikiwa. Usipojaribu, amini usiamini utakuwa siku zote palepale.

Mkuu,, in a normative perspective, hilo linawezekana, na limewezekana kwa wenzetu. Sisi hatuna hata vitambulisho vya utaifa,, hatujulikani tunakaa wapi kwa maana ya physical address..unaweza kupima mwenyewe tunahitaji muda kiasi gani kufika huko....
 
Mtanzania,

Mkuu tuseme mathlan unazungumza unalolifahamu lakini bilka shaka mpango wa Kikwete hutokana na hoja za Wabunge kusisitiza na ukifuatilia zaidi utaona kuna baadhi ya wilaya zinmepata shule nyingi kuliko nyinginezo..

Katika swala la shule nadhani hatuna haja zaidi ya kutazama maendleo yake kwani hakika wilaya yenye shule za sekondary zaidi ya 20 ni mafanikio makubwa kwa viongozi wote wa wilaya hiyo..Kifupi hapa mimi nimebakia domo wazi na kuanza kuwafikiria wabunge wetu sisi wengine..

Kitu cha muhimu napenda kusikia zaidi malumbano yenu kwani yananipa picha zaidi ya utendaji kazi na nadhani hapa tulipo tumefikia sehemu nzuri ya kuelimishana kuliko kuendelea na upuuzi wa kukabana makoo..

Ningeomba tu kusikia zaidi mazuri ya Mwakyembe kwa wilaya ya Kyela kama alivyosema Shalom maanake swala la shule ni mojawapo, Kuhusiana na kuwasisitiza vijana kweli bila uwekezaji au kuwawezesha vijana hao ktk ubunifu ni swala ambalo bado serikali yetu inafikiria ni swala la watu binafsi..

Kama nilivyosema tumeingilia Ubepari bila kufahamu unafanya kazi vipi.. Nchi za magharibi hata zile shule au Hopspital za watu binafsi zinapata subsidies kutoka serikalini, na biashara zote hizi za huduma zinakwenda sambamba na serikali..Utakuta mgonjwa akilazwa Hospital ya Private lakini analipiwa na serikali au mtu anakwenda shule ya private na serikali inatoka kiwango fulani kufidia gharama..

Unaweza kuta mwanafunzi anaingia Chuo Kikuu akilipa dollar 10,000 lakini mwanafuinzi toka nchi ya nje ktk shule hiyo hiyo hulipa mara mbili ya kiwango hicho..

Tanzania kila kitu Private ni private hata ktk huduma muhimu utakutwa mwanya shule au Hospital ndiye anaamua kitakachofanyika na kwa ghartama gani...

Mimi nadhani inabidi tuwaelemishe Wabunge wetu, waende Bungeni na picha ya Ubepari kuliko imani waliyojengwa kwamba vUbepari ni kila mtu na mzigo wake hivyo hakuna kitu kuwezeshwa..Fanya kazi kwa nguvu ni lazima utafanikiwa!.. Hii ni imani ya kikoloni, imani potovu na haiko ktk Ubepari isipokuwa malengo huwekwa na wewe mwananchi unatakiwa ku play your part!..

Kama alivyosema Mtanzania, familia yake walikuwa wakizalisha magunia mengi wakati wa zamanai na hii nafahamu ilikuwa zamani kweli wala sii wakati wa Mkapa. Kilimo kimeanguka kutokana na mipango mibaya ya serukali nzima na hata mimi nimetoa mfano wa Ukerewe ambako tulikuwa wakulima wazuri wa Mpunga tukiuita - Faya, huu ulinukia kama wa Kyela lakini umepotea kwani wakulima walianza kula mbegu. Imetokea kila wilaya nchini na haya ni makosa ya Wabunge wote kutotetea kilimo ktk budget ya seriikali..Kama wabunge wetu wameshindwa kuikataa Budget inayokiweka kilimo, elimu na Afya nyuma ni jukumu letu kuwalaumu Wabunge wote waliopitisha budget hiyo..

Tanzania itaweza tu kujitegemea kwa kufikiria kile tunachoweza kuzalisha na kikauzika..huwezi kupandisha uchumi wa nchi kwa services ambazo zinatokana na mashirika ya nje ambayo yanatoa services moja kwa moja kwa mteja hayana chain ya trickle down..Ukitazama simu nyaya zake hatutengenezi nchini, sincard, simu zenyewe, milingoti, dish na hata uniform za wafanyakazi vyote vinaagizwa nje iweje vitu hivi vilete maendeleo nchini na viwekewe msisitizo zaidi...

Bila shaka utaona sehemu nyingi nipo na Mwakyembe kwa sababu najua kazi ngumu waliyokuwa nayo Wabunge lakini in general hawa watu hawatutendei haki wananchi na wala hakuna exceptional Kitaifa. Na ndio maana nimetaka unieleze alofanya Mwakyembe mara nyingi kama sii zote wabunge wengi huwezxi hata kuhesabu vidole vya mkono mmoja. Hardly kumkuta Mbunge kafanya mabo MATANO makuu kwa wilaya yake ktk miaka mitano aliyokaa Bungeni..
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI




...(5) Ajali ilitokea saa 1 na dakika 10 na muda mfupi baadaye RPC wa Iringa alidai na kunukuliwa na gazeti la The Citizen kesho yake kuwa chanzo cha ajali hiyo kilikuwa shimo la barabarani na kwamba ajali hiyo haikutokana na njama au hujuma zozote. Msimamo wa RPC ulipingwa na kauli ya Meneja wa TANROADS, Iringa kuwa shimo lililokuwepo barabarani lilikuwa dogo mno kuweza kusababisha ajali ya gari aina la Landcruiser lenye mataili makubwa.

MUNGU IBARIKI TANZANIA

Dk. Harrison G. Mwakyembe (Mb)
Kunduchi, Dar e s Salaam
28/05/09

...inaonekana huyo meneja wa TANROADS anaona ni halali hilo shimo kuwepo barabarani, almuradi halina madhara kwa Landcruiser na matairi makubwa!

Uwajibikaji ziro!
 
- Hii topic jinsi nyani anavyokomwa yaani sina hamu ngoja niongeze popcorn, leteni habari vijana, Kyela hiyo inakuja na mambo sana.

- Tupo pamoja sana wakuu!

Respect.

FMEs!
 
Mkandara,

Nimekosa uhondo jana, kumbe huku kumewaka moto?

Naona umemuua Shalom kwa kumwambia aondoke kwenye personal attacks na aje kwenye hoja. Ni sawa na kumtoa nyoka shimoni na kumwacha peupe na kumfanya Mtanzania aponde bichwa bila matatizo. Jamaa kumbe hana data kabisa za Kyela, anaongelea mambo sijui ya mwaka gani.

Mtanzania nimemnyanyulia kofia kwa data za Kyela, hizo shule mimi niko hapa hata nisingeweza kuzitaja zote. Upambe bila data hugeuka kuwa balaa, omba wakusaidie data kama kweli unataka kuwa effective hapa JF.

Hiyo Kyela unayotaka kuwekeza nafikiri utakuwa mgeni kabisa. Hata kwa mtu ambaye anakuja Kyela mara moja kwa miaka mitano hawezi kusema Kyela kulikuwa na shule mbili tu.

Mbona nasikia unazunguka na mheshimiwa ukiwa Kyela? Yaani huulizi hata hii ni shule gani na ilijengwa lini? Kila anachosema mheshimiwa unaitikia tu?

Karibu kwenye JF ya data maana hata kule kwenye mashambulizi na kejeli, mtanzania kaamua kutupa bomu la nuclear likumalize kabisa kama wale Wajapani. Usiwe unachokoza sana watu waliokuzidi nguvu, wanaweza kufanya kweli kama alivyofanya Mtanzania hapo juu.

Haya tuendelee, kwa hapa Kyela hakuna jipya weekend hii zaidi ya halmashauri ya CCM mkoa kukubaliana na adhabu ya kumpa onyo mwenyekiti wa CCM Kyela kwa kuyumbisha chama. Huu ndio mwisho wa lile zogo la viongozi kupigwa. Pia Kyela wiki jana ilikuwa tulivu na hekaheka za wapambe kupakana matope zilipungua labda shauri ya ajali ya mheshimiwa na wana Kyela waliamua kusahau tofauti zao na kuwa pamoja.
 
Mkuu
tatizo langu na Mwakyembe sio usomi wake jamaa ni kichwa kweli na ni mzuri sana ktk elimu lakini mimi beef langu kwake ni kututisha kwa elimu yake .
Harafu kingine lile jimbo la kyela limemushinda awaachie vijana chipukizi waliendeleze vizuri na hatimaye Tz nzima .

- Mwakyembe kuzungumzia elimu yake sio kutishia ila ni kusema ukweli, kama anasema ana elimu ambayo hana hapo naweza kukuelewa, lakini kama anazungumzia elimu aliyonayo kweli hakuna uabaya wowote,

- Uchaguzi unakuja sasa waache wananchi wa Kyela waamue wanamtaka nani, JF hatuamui nani awe au asiwe mbunge wa wananchi, ingawa pia tuna haki ya kusema maoni yetu,

- Unasema jimbo limemshinda as opposed to mbunge yupi aliywahi kuongoza Kyela? au kwa data gani hizo?

Respect.

FMEs!
 
- Mwakyembe kuzungumzia elimu yake sio kutishia ila ni kusema ukweli, kama anasema ana elimu ambayo hana hapo naweza kukuelewa, lakini kama anazungumzia elimu aliyonayo kweli hakuna uabaya wowote,FMEs!

Mkuu, naona kuna sehemu member mmoja humu anasema yeye na Kombe (James) wamefundishwa certificate ya sheria na Dr Mwakyembe pale mlimani...inawezekana msingi wa hilo suala hapo juu ni huo?

Respect mkuu.
 
Hivi hizi ajali za kupanga zitaisha lini au wanaopanga ajali hizi kwa mashujaa wetu wa kupinga ufisadi tuwatafute ili wasiendelee na hujuma zao.Wana JF wapanga ajali wanajulikana kuanzia ya Salome Mbatia,Mwakyembe na Kimaro.Wafuatao hawakosi kwenye mipango hii ya uuwaji RA,EL,HC,LM na wafuasi wao.Kumbuka walichofanya kwa Balali,Kubenea na walichopanga kumfanyia R.Mengi.Wana JF tuwashauri Watanzania cha kufanya juu ya mauaji haya ya Kijasusi.
 
Kinachonishangaza Mimi kuhusu Viongozi wetu wa Tanzania mpaka kitu kiwatokee wao ndio wafahamu kuhusu Chombo chetu cha usalama wa raia ni kichwa cha mwendawazimu.Bado tuna mwendo mrefu sana kurekebisha Polisi wetu ambao wanajiunga na chombo hiko kwa Ajili ya kujitajirisha na sio kutoa huduma kwa wananchi wanasahau kazi yao ni kulinda na kutetea raia na "sio kupiga na kupokea rushwa"
 
Yaani inji hii, mmmh!! Ukifikiria saaana utachanganyikiwa! Hayo ndio mambo ya Traffic!! Nachoshangaa hakuna mkubwa yeyote (hata yule mkubwa saana!) ambaye hajui kinachoendelea!!
 
IGP abeba zigo la Dk. Mwakyembe

SIKU nne tangu Mbunge wa Kyela, Dk. Harisson Mwakyembe (CCM) kulishutumu Jeshi la Polisi kwa kuliambia kuwa linafanya kazi chini ya kiwango na kukosa umakini, kutokana na ripoti iliyotolewa kuhusu ajali yake, kuna taarifa jeshi hilo limeamua kupitia upya ripoti hiyo na kuchukua maelezo yake.

Uamuzi huyo unasemekana umefikiwa ili kumaliza utata na malumbano yaliyoanza kushamiri mara baada ya kamati iliyoundwa na Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema kuchunguza chanzo cha ajali hiyo, kutoa ripoti kuwa ilisababishwa na uzembe na mwendo kasi wa dereva wa mbunge huyo, Joseph Msuya.

Awali, kabla ya kutangazwa kwa ripoti hiyo, Dk. Mwakyembe akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alielezea mazingira ya ajali hiyo na kudai kuwa kulikuwa na lori mbele yao na ndilo lililosababisha ajali na kusema kwamba mbinu zilizotumika na dereva wa lori hilo kutengeneza ajali hiyo ni za hali ya juu ambazo amekuwa akiziona kwenye sinema.

Lakini maelezo hayo yalikanushwa vikali na ripoti ya kamati iliyokuwa ikiongozwa na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, James Kombe ambayo ilienda mkoani Iringa eneo ilipotokea ajali hiyo na kufanya uchunguzi.

Ripoti ya kamati hiyo, ilisema kuwa mbunge huyo hapaswi kusema mambo asiyojua kwa kuwa kabla ya ajali kutokea alikuwa amelala hivyo haelewi chanzo cha ajali hiyo.

Akizungumza na Tanzania Daima, kwa niaba ya IGP Mwema, msaidizi wake, Hamis Juma, alisema kuwa kutokana na taarifa hizo mbili; ya Mwakyembe na Kamati ya Kombe kutofautiana, sasa jeshi hilo limeamua kuzipitia upya.

Hamis ambaye alisema IGP Mwema hasingeweza kuzungumza na Tanzania Daima, kwa siku ya jana kwa kuwa yupo katika mapumziko, alibainisha kuwa baada ya kukamilisha upitiaji wa ripoti hizo, majibu yake yatatolewa hadharani ili jamii iweze kujua undani wa suala hilo.

Msaidizi huyo alisema, ili kumaliza mkanganyiko wa taarifa zilizoanza kutolewa katika jamii, Jeshi la Polisi limechukua ripoti ya kamati yake na ile taarifa iliyotolewa na Mwakyembe kupinga kile kilichoelezwa na kamati hiyo.

"Siwezi kukuambia msimamo wa IGP kuhusu suala hilo, lakini ndani ya siku mbili tutatoa taarifa rasmi, na ni vema mkumbuke kuwa wakati ripoti ile inatolewa, Mwema alikuwa nje ya nchi," alisema Hamis.

Taarifa ambazo Tanzania Daima ilizipata kutoka katika chanzo kimoja cha habari zilisema kuwa, IGP Mwema alienda kumjulia hali Mwakyembe nyumbani kwake Kunduchi Mtongani, jijini Dar es Salaam, na kumuahidi kuwa atalifanyia kazi suala hilo.

Chanzo hicho kilizidi kupasha kuwa, IGP hakuweza kuiona taarifa ya ripoti hiyo kabla ya kutolewa, kwa kuwa alikuwa nje ya nchi ingawa yeye ndiye aliyeunda kamati hiyo, lakini hata hivyo aaliahidi kuwa, tayafanyia kazi madai hayo katika kipindi kifupi.

"IGP alikwenda kumuona Dk. Mwakyembe na kumuahidi kuwa atafanyia kazi sakata hili ili kutatua utata unaonekana kuanza kushamiri, hasa baada ya kutolewa kwa ripoti ya Kamati Maalum aliyoiunda," kilisema chanzo hicho.

Hata hivyo, msaidizi wa IGP Mwema alikataa kuzungumzia kukutana huko kwa bosi wake na Mwakyembe.

"Siwezi kuzungumzia suala la IGP kukutana na Dk. Mwakyembe, muulizeni vizuri aliyewaambia au kama mnaweza mnaweza kumuuliza IGP kesho," alisema Hamza.

Tanzania Daima iliwasiliana na Mwakyembe kwa njia ya simu ambapo alisema hawezi kuzungumza kwa kuwa hasikii sauti ya upande wa pili kutokana na kelele zilizopo nyumbani kwake, hasa katika kipindi hiki anachoumwa.

Alisema kumekuwa na idadi kubwa ya wageni wanaokwenda kumjulia hali, akalitaka gazeti hili kumuandikia ujumbe mfupi wa maneno (SMS).

"…Haloo nani mwenzangu? Unasemaje? Siwezi kukusikia vizuri kwa kuwa hapa kuna kelele, itakuwa vizuri kama utanitumia message," alisema Dk. Mwakyembe na kukata simu.

Hata hivyo, Tanzania Daima ilipomuandikia SMS mbunge huyo hakuweza kujibu mpaka tunakwenda mitamboni.

Dk. Mwakyembe ambaye alijipatia umaarufu mara baada ya kuwasilisha ripoti ya kamati teule ya Bunge iliyoundwa kuchunguza uhalali wa zabuni iliyoipa ushindi Kampuni ya Richmond Development ambapo ilibaini kuwapo kwa mazingira ya rushwa wakati wa utoaji wa zabuni hiyo, aliikosoa taarifa ya Kamati ya Kombe na kusema kuwa kamati hiyo ilifanya kazi kama wapiga ramli.

Katika ukosoaji huo, alitumia maneno na vifungu mbalimbali vya sheria ambapo alisema kuwa, uamuzi wa kamati hiyo kutaka dereva wake akamatwe na kushitakiwa, ni sawa na kumuhukumu mapema (pre-judge) kuwa ni mwongo na mzembe.

"Uamuzi huo hauendani na utawala na misingi ya haki inayolindwa na katiba, na unaigeuza mahakama kuwa ni chombo cha kupiga muhuri (rubber-stamp) maamuzi ya polisi," alisema Mwakyembe.

Alisisitiza ukweli kuwa, ripoti hiyo imedanganya na kwamba hakuwa amelala kutokana na safari yake hiyo ilikuwa imeanzia Makambako alipokuwa amelala, hivyo si kweli kwamba alikuwa katika usingizi kabla na baada ya ajali hiyo kutokea.

Aidha, alisema kuwa hakutendewa haki kwa mujibu wa kanuni za haki za asili na kuhoji kuwa, kuna kitu gani kilichozuia kumhoji yeye na dereva wake ili kukidhi matakwa ya kanuni hiyo na kupata picha iliyo kamilifu zaidi.

"Laiti mimi na dereva wangu tungelisikilizwa, nina uhakika kuwa taarifa ya kamati hiyo maalum isingelisomwa kuchelea kulidhalilisha Jeshi la Polisi kwa kukosa umakini na viwango," alisema Mwakyembe.

Wakati huo huo, watu 12 wamekatwa na Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za kupanga mawe barabarani kwa lengo la kutaka kumteka Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro (CCM) akiwa na familia yake pamoja na na rafiki yake Joseph Temu aliyekuwa akiendesha gari aina ya Mercedes Benz.

Ajali hiyo ilitokea juzi katika Kijiji cha Mikongeni, Kata ya Lembeni wilayani Mwanga ambapo inadaiwa kuwa mbunge huyo na rafiki yake walikuta mawe yamepangwa katikati ya barabara katika eneo lenye kona jambo lililosababisha gari hilo kuyagonga na kuharibika.

Baada ya kupata ajali hiyo, Kimaro na wenzake walipata msaada wa kuvutwa na gari kubwa kuelekea sehemu salama na walipiga simu polisi ambao walikwenda eneo la tukio na kukuta mawe hayo yameondolewa.

Kwa mujibu wa chanzo kimoja cha habari, vijana hao wanashilikiwa na polisi kwa uchunguzi zaidi na wakionekana kutenda kosa hilo watafikishwa kwenye vyombo vya sheria.


Source:Tanzania Daima.
 
Na Patricia Kimelemeta (Mwananchi) - Dereva wa Lori atafutwa


JESHI la Polisi linaendelea kumsaka dereva wa lori lililosababisha ajali iliyomjeruhi Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe.

DK Mwakyembe alipata ajali hiyo mwishoni mwa mwezi uliopita, katika eneo la Ihemi mkoani Iringa akiwa njiani kutoka Makambako kuja Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Robert Manumba, alisema dereva wa lori lililosababisha kupinduka kwa gari la Dk Mwakyembe, hajapatikana na kwamba jitihada za kumtafuta bado hazijazaa matunda.

Alisema dereva huyo alitoweka mara tu baada ya ajali hiyo, jambo lililosababisha asitambuliwe.

Alisema ikiwa watafanikiwa kumpata dereva huyo watakuwa wamefanikiwa kubaini chanzo cha ajali hiyo na hivyo kuhitimisha kazi ya uchunguzi.

Manumba alisema uchunguzi huo ndiyo utakaoamua kuhusu hatua za kisheria dhidi ya dereva huyo.
 
Habari iliyokuja sasa, Polis wanadai eti dereva wa lorry haonekani yaani hajapatikana ili kukamilisha uchunguzi wao.
Source -mwananchi
 
Na Patricia Kimelemeta (Mwananchi) - Dereva wa Lori atafutwa


JESHI la Polisi linaendelea kumsaka dereva wa lori lililosababisha ajali iliyomjeruhi Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe.

DK Mwakyembe alipata ajali hiyo mwishoni mwa mwezi uliopita, katika eneo la Ihemi mkoani Iringa akiwa njiani kutoka Makambako kuja Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Robert Manumba, alisema dereva wa lori lililosababisha kupinduka kwa gari la Dk Mwakyembe, hajapatikana na kwamba jitihada za kumtafuta bado hazijazaa matunda.

Alisema dereva huyo alitoweka mara tu baada ya ajali hiyo, jambo lililosababisha asitambuliwe.

Alisema ikiwa watafanikiwa kumpata dereva huyo watakuwa wamefanikiwa kubaini chanzo cha ajali hiyo na hivyo kuhitimisha kazi ya uchunguzi.

Manumba alisema uchunguzi huo ndiyo utakaoamua kuhusu hatua za kisheria dhidi ya dereva huyo.

Wanamtafuta tena dereva wakati uchunguzi ulishafanyika na dereva wa Mwakyembe kuonekana ndio "mzembe"? Au sio mkuu Mtanzania
 
Back
Top Bottom