Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

Thank God. Alikuwa amepata shock ya ajali na sasa amezinduka. Madaktari wametuondoa hofu kuwa hana majeraha makubwa. Wanasubiri vipimo kufanya uchunguzi zaidi kabla hawajamruhusu kutoka.


Nsaji Mpoki kama uko maeneo ya karibu jamani angalieni usalama wake. Kama amezinduka naomba hata kama ni maji ya kunywa asipewe na mtu asiyefahamika ukaribu wake na Harrison. Na akipata nafuu aondolewe hapo haraka sana aletwe Hospital Dar, I mean after the First Aid/Treatment!!! Tena na Dr. wake awe ndiyo mshusika mkuu kwa treatment, ikiwezekana aitwe aje Iringa ili aungane na madaktari wa hapo na kuamua kumleta Dar, pleaase naombeni.

Nimesikitika mno. Harrison, Please we need you than ever!!! Mungu usitache wakiwa. Leteni habari zaidi ya maendeleo ya afya yake huko. Ikiwezekana wakati analetwa Dar iwe with strict confidence na hospital pia, ikiwezekana badilini magari on the way to Dar after driving a certain distance!!!! Take it!!
 
MtindiowaUbongo na Uwiano Maalum, si utani, mnanichefua! Tumeletewa taarifa ya ajali iliyomhusisha Dr. Mwakyembe, nyie wawili mnaaza kulete malumbano yasiyo na HOJA! That is absurd!
Kweli mkuu, kwenye jamii zetu zote kwenye msiba au janga watu wote wanaungana pamoja na kuacha tofauti zao pembeni.

Kwasasa japo tuonyeshe utu kwa kutokuingiza siasa au vijembe mpaka ukweli mzima ukipatikana.

Ni kuwaombea walioumia na familia zao ili mungu awape nguvu kipindi hiki.
 
MtindiowaUbongo na Uwiano Maalum, si utani, mnanichefua! Tumeletewa taarifa ya ajali iliyomhusisha Dr. Mwakyembe, nyie wawili mnaaza kulete malumbano yasiyo na HOJA! That is absurd!

Sawa kaka, nimesikia.

Sikupenda tu walivyotaja wasiohusika, si vema.Hatimae imesemwa ni speeding, si njama
 
Kuna taarifa inayoingia sasa inasema Dr. Harrisson Mwakyembe, Mbunge wa Kyela amepata ajali leo asubuhi. Je kuna mtu yeyote aliye na taarifa sahihi kuhusu hili tukio? Tafadhali tuhabarishe

Watu wengine bana!
 
Nilikuwa nashangaa kwamba walikuwa Iringa mapema hiyo, lakini habari kutoka Kyela zinasema ni kama waliondoka jana jioni na kulala Makambako na kuanza safari upya leo asubuhi.
 
Isije ikawa mambo yaleyale ya Salome Mbatia na kina Edward Moringe Sokoine!! Oooh Mola tuachie Dr. Mwakyembe angalau kwa miaka kadhaa mbele.

Wapiganaji tumepata pigo kubwa!!
 
Kumbe aligonga lori,
Lakini wenyeji wanasema alikuwa anaovateki lori akakutana na vibamps vidogo vidogo dereva akashindwaa kulimudu gari likapinduka.
 
Aisee hii hatari! Tuombe apone arudi kwenye mapambano maana upande wa pili jamaa asiporudi katika khali ya kawaida then mapambano yatakuwa yamepungukiwa nguvu kidogo. Lakini mungu atasaidia.

Pia tusubilie kusikia chanzo cha hiyo ajari maana hawa mafisi hawajali wanaweza fanya lolote ili mradi mambo yao yaende watakavyo.

Pole yake...
 
Bad news kwetu wapinga ufisadi.
Pole sana Dr. Mh. Mwakyembe.
Nakutakia upone haraka na urudi kwenye front line ya kuwanyima usingizi mafisadi.
Mapambano bado yanaendela.
 
Get well soon Harrison!
testing of your faith gives you the power of going on in hope.
 
Back
Top Bottom