Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

Wapinga ufisadi wote hawapaswi kupata ajali, kuugua, kuandikwa vibaya, kukosolewa,.... na ikitokea hayo mabalaa yakawakuta, mafisadi waandamwe, walaaniwe,...Hebu tukuekue kidogo WATANZANIA wenzangu.
 
Pole sana mkubwa tunakuombea upate nafuu urejee kwenye mapambano. Na tunamshukuru mungu kwa uzima ulio nao.
 
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa afande Advocate Nyombi ajali hii imetokea pale gari ya Dr. Mwakyembe ilipokuwa inataka kulipita lori, ambapo gari hilo la mbunge likagonga shimo lililo katikati ya barabara. Baada ya kugonga shimo, gurudumu likachomoka na gari kumshinda dereva, likagonga mti na kupinduka vibaya.
Ajali hii imetokea eneo la Ifunda.


Nawatakia majeruhi afya njema na Mungu awajalie wapone na waendelee na majukumu ya kulijenga taifa.
 
Jamani kwa sasa tuombe wahusika wote katika ajali wawe salama. Chanzo tutakijua baadaye toka kwa wahusika wenyewe. Poleni wahusika wote kwenye ajali hii. Mungu awape uponyaji wa haraka. Na pia msisahau kumshukuru mungu kwa kuwaponya na ajali hiyo.
 
Wakulu,

Kwanza naombautoa pole kwa wale wote waliopata Ajali bila kuangalia huyu ni nani,hapa wote tumekaa kuangalia Mwakyembe peke yake na hatuangalia Dereva ana khali gani.,Hii ni tabia ambayo tumerithishwa na CCM,ubinafsi na ndiyo inatufanya tuwe hapa kila siku

Tunathamini wale wenye majina tu,yaani ni bora mtu amsikini aliyeko sehemu flani afe ila mwingine apone na ndiyo maana ukeienda Hospital Bombo au sehemu za starehe na ukiwa umeongozana na Pedeshee au Mkuu yoyote wata ku-skip..

anyway Bongo yetu

Wenye Taarifa Derve anaendeleaje?Je kuna wengine wlaiokuwapo katika hiyo Gari?
 
Eee! Mungu wa Ibrahim Mjaalie Mpambanaji wetu huyu afya njema, because we need him now more than ever! Get well soon comrade!
 
Msitafute mchawi, ni ajali ya kawaida, Mwenyezi Mungu awaondolee maumivu na awajaalie kupona haraka.
 
Tunamshukuru Mungu! Taarifa nilizozipata sasa hivi kutoka pale hospitali ya mkoa ni kwamba Dr Mwakyembe yu salama, ingawa ana maumivu sehemu za shingo na taya. Madaktari wanaangalia iwapo kuna internal bleeding ili waweze ku-control. Dereva wake bado hajazinduka, yeye ameumia zaidi. Gari ya Dr Mwakyembe ilipata ajali wakati dereva wake alipokuwa ana-overtake malori mawili na ghafla kukutana na mashimo na kusababisha gari kupinduka. Lakini MUNGU mkubwa! Kwa hiyo mafisadi hawawezi kupumua kwani sala za Watanzania wote wanaoipenda nchi yao na waliojipanga tayari kwa UKOMBOZI wanamwombea kamanda huyu Dr Harrison Mwakyembe.
 
Mungu wetu na Baba yetu, mjalie mja wako Dr harrison Mwakyembe apone mapema, tunamuhitaji katika kipindi hiki cha kupambana na Ufisadi na mafisadi papa.
 
- Inasikitisha sana hii habari, Mkuu Nsaji hebu tuweke sawa na latest huko, maana huyu ni mpiganaji wetu hodari na tunamuaminia, Mungu ampe nafuu haraka sana.

Respect.

FMES!
 
Rostam atoa salamu za pole kwa mwakyembe

tbc

Haiwezi kuwa imetoka moyoni, huo ni unafiki tu wa RA kama kweli ametuma hizo salam za pole.
Halafu hawa TBC wanavibweka. Kwanini wamtafute RA ili atume salam?mbona wasimtafute Selelii au Anna Malecela? Mi nadhani ile nguvu aliyoitumia kupata kipindi maalum kumjibu mzee Mengi bado imewalevya tbc ya Dunstan Tido Mhando.
 
Huu ndio upupu wa CCM na serikali yake, wanapitisha mradi wa kujenga barabara nne toka chalinze mpaka Tanga na huku barabara mbili tu ni mbovu ajabu toka Iringa mpaka Mbeya. Barabara ya Ir - Mby inahitaji major repair before you even think of barabara nne toka chalinze mpaka Tanga.

Wakuu hivi ndivyo vipaumbele vya Rais mliyemchagua?

Swali: Je huu mradi ulikuwemo kwenye ilani ya CCM ya mwaka 2005?? Au kikwete anajirahisishia atakapostaafu 2015 awe anamtembelea mstaafu mwenzake Lushoto huku akitanua kwenye barabara nne??
 
Confirmed. Dr Mwakyembe amepata ajali mbaya Ifunda na amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa. Hajitambui na Madaktari wanafanya kila wanaloweza kumsaidia. Taarifa kamili ya maendeleo ya hali yake mtaipata baadae maana nipo eneo la hospitali. Wakati huu tumuombee kwa Mungu apate nafuu.

radio one wanasema eti mwakyembe amevunjika taya tu...
ukweli haufichiki, hata ukiufunika kwa blanketi utaibuka tu...
tutege masikio ndugu zanguni
 
JF jamani, Mwakyembe kapata ajali tunaongelea na njia nne sijui za chalinze Tanga etc. kwahiyo Iringa-mbeya kungekuwa na njia nne kajali zingeisha kabisa!!? na kwahiyo mwakyembe asingepata ajali!!!? Tuwe na imani kidogo na tukumbuke maneno ya baba wa Taifa wakati sokoine amefariki kwamba tuamini ni ajali! kama ikithibika vinginevyo basi uchunguzi ufanyike na ukweli ujulikane. Kwa sasa tunaamini ni ajali! taarifa nilizonazo mimi ni kwamba ana maumivu kiasi na anachechemea mguu mmoja. Ndege (aidha ya serikali au ya kukodi) imeshaondoka kwenda kumchukua na kumleta Dar.
 
Back
Top Bottom