Ajali ya chopa: Kamanda Kova ameonesha udhaifu

1: Kova sii bodyguard wa vice presida. Hahusiki na ulinzi binafsi wa makamu.
2: Kova alitoka nje kutoa msaada kwa nje kwan ndani walikuwepo adcs.
3: Hata simba askari katika kundi panapotokea shambulio la ghafla hukimbia kutoka katika eneo walipo wenzie mita chache aweze kumtafuta adui yupo wapi

hoja dhaifu unataka kuificha jamii kit u gani has a kuhusiana name chili suala LA kova amefanya kosa hajafanya
 
Sasa ulitaka aseme uongo? Huo ndio ukweli wenyewe wa kile kilichotokea na ninamsifu kwa kuwa mkweli na muwazi ili watu tumjue ni kamanda wa aina gani.
 
Maswali mawili kabla ya kumlaumu: was he part of the delegation or security detail?? Mkuu hakuwa na mlinzi wake??
 
Swali la kijinga sana

Weee kwenye kifo utaweza kupata muda wa kufikiria mwenzako?

Hata unaposafiri na ndege wanasema jisaidie kwanza wewe halafu ndio uwafikirie wengine, ingelipuka unadhani kungekuwa na muda wa kubebana?

Kama huamini ngoja yakukute ndio utajua kuwa ajali sio mchezo na akili yako haiwezi kuwa sawa kwa sababu lazima uchanganyikiwe labda uwe komando...

Ni kweli unaweza usipate muda wa kufikiria wenzako katika kujiokoa, lakini pia inategemea hao wenzako ni kina nani. Mfano unajiokoa bila kumfikiria mwanao, au mkeo, au baba yako, hakika wewe akiri itakuwa ilikuruka kwa wakati huo. Kwa ufupi hoja si kufikiria mwezako, hoja ni matamshi ya Kova ya kwamba alikuwa wa kwanza kutoka, ni hoja ya Kitoto kabisa inayoonyesha hali ya kichwani ya mkuu huyu wa kanda maalumu.
 
Jana katika vyombo vya Habari na magazeti ya leo Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Suleiman Kova amenukuliwa ‘akijigamba’ kuwa alikuwa wa kwanza kuruka kutoka katika Helikopita iliyopata ajari.

Ndani ya ndege hiyo alikuwemo Makamo wa Rais Dkt. Bilal, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi Dkt, Magufuli na watu wengine.

Napata shida sana kumuelewa Kova. Atawezaje kutoka ndani ya chopa na kumuacha Makamo wa Rais? Watawezaje kutoka kwenye ndege na kumwacha Mkuu wa Mkoa ambaye ndie mwenyekiti wake wa Kamati ya Ulinzi na Usalama?

Jambo hili analoliona kwake ni ujasiri ni fedheha kwa askari. Ni raia tu (ambaye hajapa mafunzo ya kijeshi) anaweza kufanya hivi na kasha kujisifu kuwa nijasiri.

Tumeumbwa wabinafsi, na kwenye kufa ndio kabisaaaaaaaaa.
 
Swali la kijinga sana

Weee kwenye kifo utaweza kupata muda wa kufikiria mwenzako?

Hata unaposafiri na ndege wanasema jisaidie kwanza wewe halafu ndio uwafikirie wengine, ingelipuka unadhani kungekuwa na muda wa kubebana?

Kama huamini ngoja yakukute ndio utajua kuwa ajali sio mchezo na akili yako haiwezi kuwa sawa kwa sababu lazima uchanganyikiwe labda uwe komando...
Anatakiwa kuwa amefundishwa haya. Mfano wako wa kwenye ndege pamoja kuwa ni sahihi, lakini kwa wahusika ndani ya ndege wanatakiwa mara baada ya kujiwekea mazingira salama wanafanya kazi ya kuokoa. Yeye anajigamba alikuwa wa kwanza kuruka kisha mabadiliko wake wakaokolewa na watu waliokuwa nje! Nafikiri tatizo kubwa alipobaini sham mleta hoja ni maiigambo aliyotoa ya kuonyesha ushujaa wake wa kuwawajibisha kwanza kuruka kutoka ndani ya ndege akisahau kuwa alikuwa na mabadiliko wake aliotakiwa kuwalinda na kuhakikisha usalama wao!
 
Swali la kijinga sana

Weee kwenye kifo utaweza kupata muda wa kufikiria mwenzako?

Hata unaposafiri na ndege wanasema jisaidie kwanza wewe halafu ndio uwafikirie wengine, ingelipuka unadhani kungekuwa na muda wa kubebana?

Kama huamini ngoja yakukute ndio utajua kuwa ajali sio mchezo na akili yako haiwezi kuwa sawa kwa sababu lazima uchanganyikiwe labda uwe komando...

No thank you! Naomba nitofautiane na wewe. Nadhani sote tunamkumbuka au tumewahi kusika habari za Lt. Col. Yonatan Netanyahu. Huyu alikuwa KAMANDA (au KIONGOZI) wa makomandoo waliohusika kuvamia Entebe, July 4, 1974 kuwaokoa mateka wa ki-Israel waliokuwa wametekwa na utawala wa Idd Amin.

Kwa nafasi yake (Netanyahu), ungedhani labda angekuwa mtu wa kulindwa lakini haikuwa hivyo, badala yake alikuwa mtu wa mwisho kuondoka kwenye tukio jambo lililosababisha kifo chake. Huyu alijua wajibu aliokuwa nao na sio mwingine bali kumwokoa hadi yule raia wa mwisho masikini kabisa na alitimiza wajibu huo ipasavyo bila kujali hatari iliyokuwa ikimkabili.

Leo, Kamanda Kova yu na Makamu wa Rais na viongozi wake wakuu badala ya kuwa mlinzi anakuwa wa kwanza "kujiokoa" akiwaacha wakuu wake "wakiteketea". Hao ndio maaskari wetu tuliowakabidi dhamana ya uhai wetu. Kama kwa viongozi kafanya hivyo, hivi sisi makapuku atatufanyiaje? Vyeo nchi hii ni kujaza matumbo tu badala ya wajibu wa msingi tunaopaswa kuutimiza.

Dhima ya Jeshi la Polisi ni "kuhakikisha usalama wa raia na mali zao"; ha ha ha! Kova mfano bora wa kuepukwa.
 
Ningekuwa makamu wa raisi ningepiga chini huyu bwana mara moja. Ni sawa na Raisi aanguke yule jamaa wa nyuma yake akimbie kumwacha Raisi.
 
Swali la kijinga sana

Weee kwenye kifo utaweza kupata muda wa kufikiria mwenzako?

Hata unaposafiri na ndege wanasema jisaidie kwanza wewe halafu ndio uwafikirie wengine, ingelipuka unadhani kungekuwa na muda wa kubebana?

Kama huamini ngoja yakukute ndio utajua kuwa ajali sio mchezo na akili yako haiwezi kuwa sawa kwa sababu lazima uchanganyikiwe labda uwe komando...

kipindi hicho, nelson Mandela alipokuwa rais wa SA alifanya ziara katika jimbo fulani.
Akiwa huko kilitijea kumbunga kilichoangusha nyumba na kuezua mapaa.
Kimbunga kilichobeba vitu vigumu na vizito kulielekea mahali aliposimama Nelson Mandela, kuona hivyo, walinzi wake wanne walimfuata na kumsukuma chini, huku wai wakijiangusha juu yake kumfunika. Takataka zilizobebwa na kimbunga zikadindoka na kupiga miili yao, baada ya muda kidogo hali ilipokuwa inaelekea kutulia, vijana hao waliinuka kwa kasi huku wamembeba Mandela kama watu wabebavyo machela uwanjani na kutoweka naye eneo hilo.
tukio lingine lilitokea katika maadhimisho ya miaka fulani ya JWTZ, maadhimisho hayo yalifanyika makao makuu ya JWTZ mtaa wa Lugalo upanga. Mkuu wa Maheshi wa Tanzania General Davis Mwamunyange, alikuwepo eneo hilo. Wakati maonyesho yakiendelea, ghafla ukatokea upepo mkali ulioezua maturubai huku ukiyabeba mengine na kuyatupa kando.
Hapo ilitokea tafrani kubwa maana askari na watu wengine waliumizwa huku wengine wakikimbia hovyo. Muda wote General Mwamunyange na askari waliokuwa wamekaa pamoja jukwaa kubwa hakuna aliyeinuka pamoja na kuwa jukwaa lao pia liluezuliwa.
Alipoinuka pale ,Mwamunyange , akikwenda moja kwa moja kutoa huduma kwa majeruhi akisaidiana ma wenzake wa high table.
 
Jana katika vyombo vya Habari na magazeti ya leo Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Suleiman Kova amenukuliwa ‘akijigamba' kuwa alikuwa wa kwanza kuruka kutoka katika Helikopita iliyopata ajari.

Ndani ya ndege hiyo alikuwemo Makamo wa Rais Dkt. Bilal, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi Dkt, Magufuli na watu wengine.

Napata shida sana kumuelewa Kova. Atawezaje kutoka ndani ya chopa na kumuacha Makamo wa Rais? Watawezaje kutoka kwenye ndege na kumwacha Mkuu wa Mkoa ambaye ndie mwenyekiti wake wa Kamati ya Ulinzi na Usalama?

Jambo hili analoliona kwake ni ujasiri ni fedheha kwa askari. Ni raia tu (ambaye hajapa mafunzo ya kijeshi) anaweza kufanya hivi na kasha kujisifu kuwa nijasiri.

Kova alikuwa sahihi kutoka wa kwanza.Uaskari ni fani.Kwenye rescue operation kwenye tatizo kama hilo yeye kama askari alitakiwa awaonyeshe wapi kwa kutokea au kurukia kwa kutangulia mbele kuruka na kuwa na uhakika alliporukia pako salama ili waliobaki wafuate pale alipopitia na kurukia nao wajiponye.Asingetangulia nani angejua apitie wapi na akiruka aliye fanya safety assurance kuwa panarukika na pako salama kwa kuangukia hao viongozi wakiruka ni nani? Ilibidi atangulie na kutangulia mbele kunapotokea hatari kwa mlinzi yeyote wa kiongozi ni wajibu na muhimu kiaskari.

Kova anastahili pongezi na kupandishwa cheo kingine na ana haki ya kutamba kuwa wa kwanza kutoka.Hongera kova kwa kuwa wa kwanza kuruka kuonyesha njia warukie wapi.
 
kamanda kova ameonyesha udhaifu mkubwa ikiwa yeye ni askari na kumuacha makamu wa raisi ndani ateketee, lakini hii inaonyesha picha halisi ya ni askari wa ainagani tulio nao katika nchi hii askari ambao wako radhi kupiga watu virungu wakiwa kwenye maandamano ya amani ila hao hao huwakimbia raia wapatapo na majanga!
 
huyu jamaa ukimuangalia vizuri ni kama hayupo vizuri upstairs! sijui ni nani uwa ana mpandisha vyeo hadi kufikia kuwa CP
Namkumbuka Kova akiwa mpelelezi Dar alivyokamata fedha dola bandia pale Savings Bank kwa cashier mmoja wa Kihindi na zikayeyuka. Zilipoyeyuka akapandishwa cheo na kupelekwa Mbeya. Rafiki yake Said Mwema analijua hili. Huwezi kuwaacha viongozi wako ukatimka. Kova alipanda chopa hiyo kuwalinda maboss wake. Nadhani mnamsingizia hakusema hivyo!!
 
Jana katika vyombo vya Habari na magazeti ya leo Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Suleiman Kova amenukuliwa ‘akijigamba’ kuwa alikuwa wa kwanza kuruka kutoka katika Helikopita iliyopata ajari.

Ndani ya ndege hiyo alikuwemo Makamo wa Rais Dkt. Bilal, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi Dkt, Magufuli na watu wengine.

Napata shida sana kumuelewa Kova. Atawezaje kutoka ndani ya chopa na kumuacha Makamo wa Rais? Watawezaje kutoka kwenye ndege na kumwacha Mkuu wa Mkoa ambaye ndie mwenyekiti wake wa Kamati ya Ulinzi na Usalama?

Jambo hili analoliona kwake ni ujasiri ni fedheha kwa askari. Ni raia tu (ambaye hajapa mafunzo ya kijeshi) anaweza kufanya hivi na kasha kujisifu kuwa nijasiri.
Ha ha ha !
Sipati picha ya kumuona Afande Kova na kitambi chake cha chini,akiruka bila parachuti!!!
 
No thank you! Naomba nitofautiane na wewe. Nadhani sote tunamkumbuka au tumewahi kusika habari za Lt. Col. Yonatan Netanyahu. Huyu alikuwa KAMANDA (au KIONGOZI) wa makomandoo waliohusika kuvamia Entebe, July 4, 1974 kuwaokoa mateka wa ki-Israel waliokuwa wametekwa na utawala wa Idd Amin.

Kwa nafasi yake (Netanyahu), ungedhani labda angekuwa mtu wa kulindwa lakini haikuwa hivyo, badala yake alikuwa mtu wa mwisho kuondoka kwenye tukio jambo lililosababisha kifo chake. Huyu alijua wajibu aliokuwa nao na sio mwingine bali kumwokoa hadi yule raia wa mwisho masikini kabisa na alitimiza wajibu huo ipasavyo bila kujali hatari iliyokuwa ikimkabili.

Leo, Kamanda Kova yu na Makamu wa Rais na viongozi wake wakuu badala ya kuwa mlinzi anakuwa wa kwanza "kujiokoa" akiwaacha wakuu wake "wakiteketea". Hao ndio maaskari wetu tuliowakabidi dhamana ya uhai wetu. Kama kwa viongozi kafanya hivyo, hivi sisi makapuku atatufanyiaje? Vyeo nchi hii ni kujaza matumbo tu badala ya wajibu wa msingi tunaopaswa kuutimiza.

Dhima ya Jeshi la Polisi ni "kuhakikisha usalama wa raia na mali zao"; ha ha ha! Kova mfano bora wa kuepukwa.

Hebu cheki signature yako mkuuu!!!!!!

Unaongelea Israel tena makomandoo kwa kesi ya Tanzania mkuu unalinganisha nini hapa!!!!!!
Hati ya muungano tu watu wanatoana roho siku ya ngapi leo!!!????

Uzalendo hauji kwa kazi mtu anayofanya ni suala mtambuka haswaaa tena ni nyeti kabisaaaaaaa.........je uzalendo upo katika nchi hii!!!?????
 
Back
Top Bottom