Ajali Tanzania: Mawazo mbadala kuhusu udhibiti wa ajali Tanzania


Mawazo yako mbadala nayaunga mkono, kitu kingine ambacho ningependa kuongeza ni kubadili sheria ya barabara. Naamini ukitenganisha lanes zinazokwenda muelekeo mmoja na upande mwingine, ajali za uso kwa uso ambazo Tanzania zimekuwa nyingi zitapungua. Ukiwa na lanes kama hizi hapa chini, ajali za ana kwa ana zitapatikanaje? Hata kama mtu ana-over pass gari nyingine, anafanya hivyo akiamini kabisa hakuna gari atakayokutana nayo ikiwa inakuja kuelekea direction nyingine. Tumeona ziara nyingi za JK kufungua barabara mpya but sidhani kama suala la ajali mara nyingi huwa linaangaliwa. Kinachoangaliwa ni kura na kula tu. Ni wakati sasa sheria ya barabara ibadilishwe ili ziweze kupanuliwa na kutengwa by traffic directions kama kwenye hii picha chini.

 
Solution rahisi ni moja tu...
Barabara zote kuu zifanywe double... I mean mbili kwenda mbili kurudi, za kwenda na kurudi zitenganishwe kwa tuta...

Ajali zote mbaya ni "uso kwa uso"... yaani anayeenda na anayerudi... na hapo ni watu wanaovatekiana...
 

Exactly... this is what I am talking about
 
Yeah umejibu vizuri sana mkuu! Lakini kwa nchi ilyojaa rasirimali kama yetu haya yote si yanawezekana? Tembelea nchi ndogo tu jiran ya Rwanda utazame systems zao ndo ujiulize hapa kwetu kunani?

Kwa mujibu wa katiba ya sasa Wananchi wamepewa mamlaka ya kuwachagua viongozi wanaoona wanafaa kuwaongoza na kulisukuma gurudumu la Maendeleo mbele,2015 ni mwakani tu mkuu tumia fursa hiyo ipasavyo ikiwezekana toa hamasa na kwawengine pia.
 
Natamani ushauri wako ungefikiamamlaka husika maramoja.
 

Heshima kwako Mkuu...
 
Ngugu zangu waTanzania walioko ndani na nje ya nchi,Nawasalimu.

Huwa naandika makala ya maaendeleo lakini Tatizo hili la AJARI ambalo kila siku tunasikia,limenishawishi kuandika
haya ambayo ninaenda kuandika kuhusu AJARI.

Napenda kutoa ushauri kwa serikali kukomesha AJARI

1.RAISI tunaomba utoe amri kwa wakuu wa mikoa yote,makamanda wa polisi ,wakuu wa wilaya kuwa ''AJARI IKITOKEA KWENYE ENEO LAkO LA KAZI BASI wanafukuzwa kazi.

2.Trafiki wote wafanye patrol barabarani kubaini madreva ambao wanakwenda kasi,wachukuliwe hatua kali

3.Usalama wa Taifa wafanye uchunguzi kubaini TRAFIC wanao kula rusha barabarani

4.Serikali ikague lesseni na vyuo waliosomea madreva wote,kama dreva hakusoma kwenye vyuo ambavyo vina tambulika na serikali wanyan'ganywe lesseni

5.Serikali itoe muda wa gari kufika sehemu usika mfano kutoka DAR hadi mwanza ni masaa 12 barabarani,ikiwa dereva akifika kabla ya masaa hayo basi ''jela

6.MMABSI yote ya abiria inatakiwa wakate bima kwa abiria ,na serikalai iweke kiwango cha juu kama fidia wa wahanga wote wa ajari ,Mfano ukipoteza ndugu kwenye ajari,mhanga anatakiwa alipwe TSH 40 million

7.Dereva Akisababisha ajari ataenda jela miaaka 30 na kunyan'ganywa lessen.

8.Serikali iimalishe alama za barabarani,na kupanua barabara

Nyingine NITAZILETA BAADAE ,TUJADILI HIZI KWANZA
 
Mkuu ushauri wako ni magoli sana, lakini kwa hilo la pili binafsi nina mtazamo nalo tofauti! Hivi askari katika basi ni wakazi gani kama abiria wenyewe huwa tunakaa kimya katika matukio ya barabarani. Mfano tunawashuhudia madereva wakienda mwendo kasi na sisi tumo ndani tuliii, tunavutwa na breki za ajabu kisa dereva anataka kuovertake katika mazingira hatarishi tumenyuti tu. Sisi wenyewe hatujali maisha yetu tunataka mtu wa nje (polisi) aje kujali!!!!!

Mimi binafsi naamini abiria tuna nafasi kubwa ya kuzuia hizi ajali!!
 

Solution rahisi ni moja tu...
Barabara zote kuu zifanywe double... I mean mbili kwenda mbili kurudi, za kwenda na kurudi zitenganishwe kwa tuta...

Ajali zote mbaya ni "uso kwa uso"... yaani anayeenda na anayerudi... na hapo ni watu wanaovatekiana...

Wakuu sipingani na mawazo yenu ila tunaangalia nini kifanyike Kwa wakati uliopo.

Kutengeneza lanes mbili kila upande ni best solution ila sio applicable Kwa muda huu. Barabara zetu za magumashi tu zinachukua years kukamilika Hizo lanes mbili zitachukua miaka mangapi!!

Hatuwezi kuendelea kusubiri Hizo lanes huku ndugu zetu wanakufa Kwa ajali kila uchwao lazima jambo lifanyike sasa huku long term plans nikiwa under construction.
 
Mkuu hakuna mtu anayejali maisha ya wasafiri. Kwanza wasafiri wenyewe hawako makini wanachekelea tu dereva akiendesha ovyo. Wanasosimamia usalama wao wanaangalia pesa tu.
 
1.Madereva wa safari ndefu wawe wawili au 3,pia trafic wawe waadrifu na wakali ktk kusimamia sheria na kuacha hongo
 

Ninafikiri kuna haja ya kutoa Elimu kwa Raia(Abiria) juu ya Haki zao wanapokuwa ndani ya Chombo cha usafiri hii itachangia abiria kuwa aware endapo dereva atakiuka sheria barabarani....Heshima kwako mkuu!
 
Wadau kuna watanzania wenzetu wanajitahidi sana kutoa mchango wao katika kusaidia jamii ipone katika janga fulani
Sijajua kwanini walio katika media uwa awatoi mchango wao katika kile ambacho wasanii uamua kujitolea kwa jamii.Nafahamu media inayo ushawishi mkubwa kwa jamii kuijenga au kubomoa.

Lakini wako bize kupiga ya moto na kitorondo masaa 24 wakati taifa liko bize kupambana na janga la AJALI.Sikatai msipige nyimbo hizo,bali huu ni wakati wa kucheza wimbo ule wa mr blue yuko recho na barnaba wimbo unaitwa dereva makini.Wimbo wa jcb na joseph haule unaitwa kwenye corner.Walau mkicheza nyimbo hii zitawasaidia madereva na abiria wenyewe wanaosikiliza humo mabarabarani.
"HAKI YAKO KUFIKA SALAMA UNAKOKWENDA,ABIRIA TUNAKUPENDA,KUNA WATOTO,KINA MAMA NA WATOTO NAO WANAKWENDA".
 
Nafikiri tuanzie humu ndani kuwahamasisha japo kwa kuziweka hizo pini ulizozitaja ili kuwakumbusha madereva wa vyombo vya moto kuwa makini barabarani kwani naamini humu jf madereva ni wengi.
 
Wakuu sio mara moja nimeshuhudia ujinga mkubwa unaoweza kusababisha ajali kwa madereva wa mabasi yaendayo mikoani wanapokua barabarani, kwanza huwa sio wastaarabu barabarani kwa maana ya kwamba huwa hawajali watumiaji wengine wa barabara na hawako patient kabisa, pili huwa hawapendi kuchukua tahadhari kwa kisingizio tu kuwa wanaharaka kitendo kinachofanya wawe wana'overtake' hovyohovyo tu bila kujali alama yoyote ya barabarani. Binafsi nawapongeza madereva wa malori wengi wao huwa waungwana sana barabarani na japo huwa wanasafiri umbali mrefu ila ni watu wa msaada sana barabarani, nasema hivi kwa kuwa ninaexperience ya kuendesha highways mchana na hata usiku pia na hawa jamaa wa malori hawana shida sana kama wenzao wa mabasi.. Inafikia wakati mtu ukitaka kusafiri na gari lako unawazia mabasi kwa jinsi madereva wake walivyowehu. Hivi kweli inakuaje dereva aliebeba watu anakua rough barabarani kuliko hata dereva aliebeba mizigo (malori) na bado eti tunaambiwa kuendesha mabasi unatakiwa uwe na leseni adimu ya class C? Hebu angalia kwa mfano picha hii chini hawa madereva utasema kweli wanaakili timamu?
Hivi kwa mtindo wa udereva wa namna hii ajali zitaisha Tanzania? Hivi hata sehemu ndogo ya kusubiriana kupita huwa wanataka wote wapite na kila mtu anamuwashia mwenzake taa asubiri mwishowe wanaishia kugongana uso kwa uso hiyo ni akili kweli?



 
Wanavyotofautisha leseni za abiria wanatakiwa pia kutofautisha adhabu. Ukiwa name class C basis ukifanya kiss hukumu take I we Mara mbili Saudi ya dreva wa kawaida. Hawezekani umebeba abiria halafu ufanye kosa huukumiwe sawa na mwenye Vitz.
 
Wanavyotofautisha leseni za abiria wanatakiwa pia kutofautisha adhabu. Ukiwa name class C basis ukifanya kiss hukumu take I we Mara mbili Saudi ya dreva wa kawaida. Hawezekani umebeba abiria halafu ufanye kosa huukumiwe sawa na mwenye Vitz.
Hebu endesha hiyo simu vizuri mkuu utasababisha ajali
 
Nafikiri tuanzie humu ndani kuwahamasisha japo kwa kuziweka hizo pini ulizozitaja ili kuwakumbusha madereva wa vyombo vya moto kuwa makini barabarani kwani naamini humu jf madereva ni wengi.

Kweli mkuu,naomba tusadie kwa hilo,ujumbe uwafikie wengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…