Ajali Tanzania: Mawazo mbadala kuhusu udhibiti wa ajali Tanzania

Wanavyotofautisha leseni za abiria wanatakiwa pia kutofautisha adhabu. Ukiwa name class C basis ukifanya kiss hukumu take I we Mara mbili Saudi ya dreva wa kawaida. Hawezekani umebeba abiria halafu ufanye kosa huukumiwe sawa na mwenye Vitz.
Ni kweli mkuu...maana watazunguka kila kona kutafuta dawa ya ajali hazitoisha...kwa sababu zinasababishwa na madereva zaidi kuliko ubovu wa magari...adhabu kali zinaweza kuwatia adabu kiukweli
 


N11_road_south_of_Newtownmountkennedy.jpg

Jamani, hebu tuwe realistic tuache ndoto za alinacha. Hivi kweli nchi kama Tanzania unaweza kutengeneza barabara kama hii toka Dar hadi Kigoma au Tunduma? Hata nchi nyingi zilizoendelea hakuna kitu kama hicho, bali hizo zinakuwa barabara katika eneo la karibu na mjini, au ukanda wa kilometa 50 toka mji mkubwa.

Hata bondeni ambako wenzetu wameendelea, ukiangalia barabara zao kubwa mbili, N1 na N2, si kwamba N1 iko hivyo toka Johannesburg hadi Cape Town, na N2 iko hivyo toka Durban hadi Cape Town. N1 na N2 zinafanywa kuwa dual carriageway maeneo ya karibu na mijini tu, ukisha toka nje ya mji zinakuwa na kawaida single lane.
 
Hoja yangu ni, madereva wa mabasi wapimwe akili na matumizi ya madawa ya kulevya mf,bangi, pombe kituo hadi kituo. Pili, ukaguzi wa leseni na vyeti liwe ni zoezi la kudumu. Tatu, trafiki wanaokula rushwa waendelee kufukuzwa kazi, nne, wamiliki wa mabasi walazimishwe kutoa mkataba wa ajira kwa madereva wawili kwa kila gari.
 
Niambie kama kuna kipimo cha akili na kinapatikana wapi , na uniambie kinaitwa nini , kama tunavyofahamu ukitaka kupima joto unatumia thermometer sasa ukitaka kupima akili utatumia nini?
 
Tano, mabasi yafanyiwe ukaguzi na Sumatra/Askari, kabla ya kuanza safari
 
Naunga mkono hoja,nimeshtuka nimesoma kwenye gazeti Mwananchi la leo kuna habari inayosema na imethibitishwa na kamanda Mpinga kwamba kuanzia Juni/Agost mwaka huu ajali zimeuwa watu 1,078 na kujeruhi watu 3,715,yaani miezi mitatu ajali zinauwa na kujeruhi idadi hiyo je mwaka mzima watakufa wangapi???wakati mwengine abiria tunakuwa hatuna umoja,unakuta may be mpo safarini dereva haendeshi kwa usalama ukijaribu kumkanya abiria wenzako wanakukebehi utasikia "huyo ndo mara yake ya kwanza kupanda bus anasikilizia"wengine wanakwambia ww unaenda kwenu ssi tunawahi biashara zetu,ukipiga cm polisi akija konda anashuka wanaenda nyuma ya gari akirudi anagonga bodi bus linaondoka mwendo ni ule ule tena umezidi,Tanzania yetu omba kwa Mungu akufikishe kwa miujiza yake tu ila sheria zetu zimeingiliwa hazitulindi tena tuwapo barabarani.
 
Ndg wanabodi Heshima kwenu..

Bila shaka vifo vingi vinavyotokea kwa kiasi kikubwa hivi sasa ni kutokana na ajali za magari barabarani hasa Mabasi..

Tunaipongeza serikali kwa hatua mbalimbali ambazo imekua ikichukua ili kukabiliana na Changamoto hii kubwa japo kwa kiasi kikubwa bado ajali ni janga kwa nchi yetu..

Kwa kua akili ni nywele na kila mtu anazake,nami pia naomba kuwashirikisha fikra nilizonazo kama ifuatavyo..

1)SERIKALI IANZISHE VYUO MAALUMU KWA AJILI YA MAFUNZO YA UDEREVA WA MAGARI YA ABIRIA PEKEE..

Serikali na sio vyuo binafsi vianzishe vyuo maalumu kwa ajili ya Madereva wa Abiria pekee...
Hii itasaidia kupunguza madereva wa Mtaani wanaopiga dayworker kisha baada ya Muda wanaendesha mabasi ya Abiria.

Nimesema vyuo maalumu na wala si VETA wala vyuo binafsi Kutokana na sababu kua sasa ,VETA na vyuo vingine binafsi vimekosa credibility yaani mtu yeyote anaweza pata leseni hata kwa magumashi ilimradi awe na pesa..

Lakini pia ili mtu A-qualify kusomea udereva wa magari ya abiria awe amesoma mpaka kidato cha nne na awe amefaulu ili kupata watu makini wanaojielewa na si kuokoteleza hadi STD VII kama ilivyo sasa.

2)KILA BASI LISAFIRI NA ASKARI WA BARABARANI ANGALAU MMOJA:

Sio lazima askari aanze mwanzo wa safari mpaka mwisho wa safari...kunaweza kua na utaratibu wa askari maalumu wa barabarani kupokezana kila wilaya ambako gari hiyo itapita..hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kum-control driver hivyo kufata sheria zote za barabarani kama inavyopaswa.

3)MISHAHARA YA MADEREVA IBORESHWE

Hii itasaidia watu wengi kuwa motivated na kupenda kazi ya udereva ma mabasi hivyo kupata watu wengi wanaoqualify,hii inamana mtu aiendeshe gari kwa kua ameona ndo sehemu ya kutokea bali udereva uwe tamanio la mtu mwenyewe.

Wapewe pesa ya kutosha na posho juu ili kumfanya Dereva afurahie kazi yake na kupunguza msongo wa mawazo..

4)MISHAHARA YA ASKARI WA BARABARANI IBORESHWE

Hii itasaidia kwa kiasi kikubwa askari hawa kutoshawishika kuchukua pesa ndogondogo wanazopewa njiani hivyo kupelekea kufanya kazi zao kwa uaminifu na umakini wa hali ya Juu.

5)ASKARI WA BARABARANI WAPUNGUZWE

Wingi wa Askari wa barabarani waliopo hivi sasa haimanishi ni kuboresha utendaji na udhibiti wa ajali barabarani..unaweza kua na askari wachache na wakafanya kazi nzuri yenye zaidi,iwapo madereva hawataokotwa mitaani,wakalipwa pesa vizuri na askari nao wakalipwa pesa vizuri hakika makosa barabarani yatapungua kwa kiasi kikubwa..hii ina apply kwa madereva wa magari yote barabarani...

Iwapo adadi ya askari barabarani itakua ndogo itakua rahisi kuwa hudumia financially na kwa pesa nzuri zaidi.
Nashauri askari barabarani walipwe kuanzia milioni 1 kwa Mwezi.
Utitiri wa askari barabarani haimanishi ndio uimarikaji wa utendaji kazi.

6)UKAGUZI WA MABASI YA ABIRIA KABLA YA SAFARI UIMARISHWE..

Ukaguzi wa maramojamoja unaofanywa na askari wa barabarani kwa sasa unamapungufu makubwa..
Pawe na kikosi kazi maalumu ambacho kazi yake ni kukagua mabasi yote ya abiria siku moja kabla ya safari na gari hiyo iwe na alama kua imekidhi vigezo vya kusafirisha abiria kesho yake..Hii itasaidia hasa kupunguza ajali zitokazazo na uchovu wa magari yenyewe hasa yale yanayounga safari bila kupumzishwa..
ikiwa na pamoja na kumpima dereva kabla ya kuanza safari kama hatumii madawa ya kulevya wala kilevi chochote..

7)SUMATRA WASIFANYE KAZI KWA MATUKIO PEKEE

SUMTRA Wasisubiri kupaza sauti katika kuwaambia umma kua nauli zitapanda kutokana na bei za mafuta kuongezeka,na wasisubiri mpaka matatizo yatokee ndo wajitokeze kwa waandishi wa habari kama wanavyofanya hivi sasa.SUMATRA Ifanye kazi yake ipasanyo na isifanye kazi kisiasa...

Nimesema ni mawazo tu sio msaafu wala Biblia unaweza kosoa au kuboresha kwa Mtazamo chanya ili kutoa mawazo sahihi kisha yafanyiwe kazi na mamlaka husika.

Karibuni kwa Mawazo chanya pia.

Sababu ulizotaja sio mbaya ila hazijangatia mazingira halisi ya kitanzania kwa sababu hazitekelezeki katika muda mfupi. Kwangu mimi sababu kuu ya ajali hizi ni:

1. Madereva kutopata muda wa kutosha wa kupumzika. Hii huwafanya kukimbia sana ili kuokoa muda na kupata muda wa kutosha wa kupumzika.
2. Sheria kuzuia magari kutembea usiku. Kwa magari kutembea mchana tu, husababisha wear and tear kuwa kubwa. Pia muda wa service hautoshi kwa sababu ya muda. Mathalani Kwa gari linalofika Dar saa 4 au 6 usiku na kutakiwa kugeuka saa 12 asubuhi, ni wazi kuwa mafundi hawatapata muda wa kutosha wa kufanya service.

3. Mabasi mengi kuondoka kwa wakati mmoja.

SULUHISHO

Ili kuondoa tatizo hilo, ni kuondoa kikwazo cha magari kutembea kwa masaa 24 na kisha kuweka interval ya magari yanayoelekea sehemu moja kuondoka kila baada ya saa moja.
SULUHISHO
 
Cha Muhimu ni kurudisha nakuboresha zaidi usafiri wa reli uwe wa kisasa.Hii itapunguza utitiri wa mabasi barabarani..Nchi hii wameuwa reli ili vigogo wafanye biashara ya mabasi
 
Mabasi huwa yanakimbia sana , hii inasababisha impact kubwa inapotokea ajali, kuna kitu kinaitwa tracking system wangeanza na hiyo, mabasi yote yafungwe na yawe monitor kwa speed isizidi 80km/hr , mfano mzuri ofisini kwetu tulikuwa hatuna limit yani gari zilikuwa zinakimbizwa kama ndege ya chini mpaka jasho linakutoka, wameweka hii kitu mwendo ni 80km/hr tu unasafiri ukiwa na amani.
 
ishu kubwa kwangu naona magari yanayotembea zaidi ya masaa10 na kufika vituoni ama mwisho wa safari kuanzia saa4 usiku yasiruhusiwe kuendelea na safari kesho yake ili gari ifanyiwe service bora na si bora service.Siku moja niliwahi kuwa pale Nyegezi basi fulani iliingia saa6:30 usiku alafu saa10 ikawa stand tena inapakia kurudi dar ..kwa hari kama hii tunatarajia nini hili lije kufika tena ubungo saa3/4 usiku?
 
Cha Muhimu ni kurudisha nakuboresha zaidi usafiri wa reli uwe wa kisasa.Hii itapunguza utitiri wa mabasi barabarani..Nchi hii wameuwa reli ili vigogo wafanye biashara ya mabasi

Mkuu,tayari hapo kwenye red wewe mwenyewe unakiri kua usafiri wa reli umefanywa wa kusuasua maksudi ili wafanye biashara ya Mabasi ..sasa unafikiri wazo la kurudisha usafiri wa reli kwa sasa ni rahisi kama utatuzi wa haraka kunusuru hali mbaya ya ajali zinazoendelea??????
 
Nimetafakari sana namna watanzania tunavyoteketea kwa ajali za mabasi. Nimejiuliza maswali mengi nikakosa majibu. Labda wanaJF wenzangu mnaweza kushare nami. Mfano hivi upeo wa traffic police wetu unaishia tu kukagua driving licence, kadi ya Gari, honi, headlights, bima, road licence, uchakavu wa matairi tuu? Vipi mechanical wellbeing ya Gari? Vipi speed governors zilizogharimu watu hela nyingi? Tutakufa sana kwa upeo wa hawa maafande wetu.
 
Mimi nadhani hata tukiwajengea boarding school madereva wasome miaka mitano itakuwa solution. Hii issue ni uzembe zembe na kujiamini sana bila tija.

Hata wasomi wetu mambo ni haya mikataba mibovu wanaingia, Ma-doctor hivyo hivyo, wakandarasi wanajenga chini ya kiwango, Jamaa wa bodaboda fujo tu yani kila kona hakuna hafadhali. Labda tuweke double road kama walivyo shauri wengine.
 
serikali ilitumia kodi zetu nyingi kujenga mkonga wa taifa wa internet lakini bado haujatusaidia sana. Tuutumie huu mfumo kufunga camera barabarani kama zifanyavyo nchi zilizoendelea. Hii manpower ya kikosi cha usalama barabarani kutwa kushinda barabarani ingetumika kushinda kwenye computer na ku-monitor madereva wasiotii sheria za barabarani

Nafuwewe.
 
Kwa kuwa ajali za kutisha hasa za mabasi ya abiria zinazidi kuteketeza maisha ya Watanzania kuna haja jeshi la polisi baada ya mabadiliko ya sheria za barabarani litumie askari wake kuendesha magari haya ya abiria badala ya madereva wa kiraia wanaovunja sheria za barabarani kila siku hali inayosababisha kutokea ajali hizi kila siku.

Ninatumaini makamanda wa polisi wa kila mkoa wataweka utaratibu wa askari wao kuendesha mabasi haya ya abiria.Ni ukweli usiopingika iwapo askari wakitumika kuendesha mabasi ya abiria uwezekano wa kutokea ajali ni mdogo.Utaratibu huu uwekwe kwa magari ya njia ndefu na mwendo uwe kilometa 50 kwa saa.

Hivyo jeshi la polisi lifanye mazungumzo na wamiliki wa magari ili wawaachie jukumu la udereva wa mabasi yao ili kupunguza ajali.
 
Back
Top Bottom