Shule, shule, shule,
Nilipata bahati kutembelea nchi moja nilishangazwa na utaratibu wao wa kutoa leseni.
Hebu cheki utaratibu huu halafu mfananishe na TZ.
1. Mtu unaingia darasani mwaka mzima kujifunza theories. Hapa ina maana unajifunza alama zote za barabarani na kuzielewa maana yake. Wakati huo huo unaingia barabarani Practical ukiwa na mwalimu kwenye gari maalum.
2. Baada ya mwaka mmoja, unapewa provisional licence ambayo unaruhusiwa kuendesha gari ila ukiwa na mtu mwenye senior licence pembeni. Hii nayo ni kwa mwaka mzima halafu ndo unapata full licence.
3. Ukitaka kuwa dereva wa public service vehicles (Taxi, Buses) unatakiwa kuwa na leseni yenye miaka kumi au zaidi. Huko hamna mambo ya class A, B, C, D, au E. Huko ni experience na nidhamu.
4. Ukifanya kosa pointi zinatolewa, zikifika kiasi fulani unatakiwa kuingia darasani si chini ya miezi sita. Hapo ndipo unalipia gharama za shule ambazo si mchezo.
5. Dereva wa public transport (buses) kwa mwezi analipwa si chini ya $ 1,000. Wanaheshimu kazi ya udereva.
6. Hairuhusiwi kuagiza nje ya nchi gari lenye umri wa zaidi ya miezi 12.
Sasa kwa hali kama hii, ajali bado zipo lakini si fatal kama bongo. Ajali ni chache sana ukilinganisha hata na America ingawa wapo kwenye car ownership ratio sawa.