Ajali Tanzania: Mawazo mbadala kuhusu udhibiti wa ajali Tanzania

kupata michezo yako ya uhakika na kushinda zaidi leo shukrani kwa wachezaji wangu wote wa jana
1097012
 
MAbasi ya kwenda Kigoma hususani Adventure Na Saratoga Jamaa gari zao hazina mikanda almost Siti zote ila zinaruhusiwa kutoka Ubungo abiria wakiwa hawajafunga mikanda kabisa..


Wale watu Wa sumatra na Traffick kituo cha mabasi Ubungo hawafai na hawajui kazi yao.. Baadhi ya Zile gari hata Mtoto Wa darasa la pili hawezi ziruhusu kusafiri...



Msipofanyia kazi hili ombi ipo siku Kangi Lugola atafikishiwa hii taarifa.
 
Compliance haimati. Tafrafiki wanalazimisha makosa kabisa! Ni shida kabisa,yaani wananyang'anya watu hela k2a nguvu huko barabarani kupitia faini za kulazimisha.
 
Najua kuna trafiki wa kutosha humu jamvini,kuna tatizo kubwa la waendesha baiskeli usiku. Wanendesha baiskeli ambazo hazina taa wala refrector. Jambo hili ni chanzo kikubwa cha ajali usiku. Wananchi waelimishwe kuhusu tabia hii hatarishi.
 
Haya hapo mazuri lakini tatizo kubwa ni barabara ndogo. Magari kupishana uso kwa uso ni tatizo na serikali ijitahidi sasa tukimaliza kujenga barabara tuzipanue na kuwe na pande mbili. Mfano mimi naishi Texas nikisafiiri naendesha kasi ya 120 per km hr (75 per mile) lakini niko safe kwasababu ya tuna 4 ways au zaidi.
 
Najua kuna trafiki wa kutosha humu jamvini,kuna tatizo kubwa la waendesha baiskeli usiku. Wanendesha baiskeli ambazo hazina taa wala refrector. Jambo hili ni chanzo kikubwa cha ajali usiku. Wananchi waelimishwe kuhusu tabia hii hatarishi.
Wiki iliyopita nimemkosakosa mwendesha baiskeli pale Morocco,siku amini kama nimemkwepa
 
Shule, shule, shule,

Nilipata bahati kutembelea nchi moja nilishangazwa na utaratibu wao wa kutoa leseni.

Hebu cheki utaratibu huu halafu mfananishe na TZ.

1. Mtu unaingia darasani mwaka mzima kujifunza theories. Hapa ina maana unajifunza alama zote za barabarani na kuzielewa maana yake. Wakati huo huo unaingia barabarani Practical ukiwa na mwalimu kwenye gari maalum.

2. Baada ya mwaka mmoja, unapewa provisional licence ambayo unaruhusiwa kuendesha gari ila ukiwa na mtu mwenye senior licence pembeni. Hii nayo ni kwa mwaka mzima halafu ndo unapata full licence.

3. Ukitaka kuwa dereva wa public service vehicles (Taxi, Buses) unatakiwa kuwa na leseni yenye miaka kumi au zaidi. Huko hamna mambo ya class A, B, C, D, au E. Huko ni experience na nidhamu.

4. Ukifanya kosa pointi zinatolewa, zikifika kiasi fulani unatakiwa kuingia darasani si chini ya miezi sita. Hapo ndipo unalipia gharama za shule ambazo si mchezo.

5. Dereva wa public transport (buses) kwa mwezi analipwa si chini ya $ 1,000. Wanaheshimu kazi ya udereva.

6. Hairuhusiwi kuagiza nje ya nchi gari lenye umri wa zaidi ya miezi 12.

Sasa kwa hali kama hii, ajali bado zipo lakini si fatal kama bongo. Ajali ni chache sana ukilinganisha hata na America ingawa wapo kwenye car ownership ratio sawa.

Point zako nimezikubali sana, kwani kutozwa faini tu kunamfanya dereva kutafuta njia ya kuzipata hizo pesa ambayo pengine itakuwa sababu ya ajali tena, kama kujaza abiria zaidi ya uwezo n.k. Cha kuongeza nafikiri ni-

1 kuimarisha taarifa za madereva (data base) ili kila muajiri ajue toka kwenye central information za kila dereva kabla ya kuajiri
2 Serikali iwe na jarida lenye kuonyesha mafanikio kila hatua wanayochukua ili zile hatua zenye mafanikio hasi zitolewe
3 Kuwepo kwa utafiti wa mara kwa mara wa kujua mwenendo wa madereva bara barani.
4 Madereva wa Magari ya mizigo nao wawekewe masharti maalum kwani ndio wasababishaji wakubwa wa ajali.
5 Kesi za madereva waliosababisha ajali iwekwe katika luninge, na ikibidi wahojiwe mara kwa mara na waandishi wa habari ili kukuza moral feelings kwao na madereva wengine. Yaani kuwepo na uwanja wa kuelewa walichokifanya na athari zake ili wawe walimu kwa wengine.
6. Kuanzishwe mtandao/jumuiya au chama cha walioathirika ambao wataisukuma serikali, vyama vya madereva na wananchi ili kuliona hili tatizo la ajali kuwa ni la kitaifa na kutia msukumo kwa serikali wakati wote.
7. Wahanga, walioathirika au ndugu zao wa karibu wataarifiwe muendeleo wa kesi za madereva waliosababisha ajali hizo, ili ijulikane kama wamehukumiwa kwa makosa waliyotenda. Hii itawaletea waathirika wa ajali angalau kuja kuwa mkondo wa sheria umefanya kazi yake.
 
Watu wanasema Texas sijui wapi kuna two separate ways katika kila highway ni sawa na ni nzuri lakin sisi kwakuwa uwezowetu Mdogo tufanye yanayowezekana. Kama

Moja wahusika na Barabara kama TANROAD wawe makini kila ubovu wa Barabara yaani mashimo yazibwe mapema.

Pili alama za barabarani wahakikishe zipo kila panapotakiwa.

Tatu Madereva wafuate vema salama hizo
 
Tarehe 15 January 2022 basi la machame likitokea arusha kwenda iringa lilidondoka kolo kondoa na kuuwa watu 3 na wengine kupata vilema .

Chanzo cha ajali ni kuwa machame alitoa basi lililokuwa bovu baada kuona watu walikuwa wengi wakisubili kutoka babati kwenda kondoa.

Nature ya barabara ya babati kwenda kondoa ni kona nyingi sana na milima kuwa mingi. Ili mfike salama nilazima basi liwe zima na umakini wa dereva.kwa kweli ajali sikia kwa mtu ikikukuta kuna kupoteza maisha au kilema au kupata post traumatic stress.

Basi lilitokaje babati kuja kondoa likiwa bovu na kwanini polisi hawakagui mabasi.

Naomba serikali ichukue hatua kali sana isimuone mtu yeyote haya maana watu wanakufa na wengine kupata vilema .
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom