Ajali mbaya Mbezi Afrikana

Ajali mbaya Mbezi Afrikana

Je ndiye alikuwa anaendesha hilo gari?@Papaa Kinyani.
Kama sikosei ipo thread ya leo humu iliyothibitisha huyo daktari wa falsafa na mtaalamu wa mifumo ya kompyuta wa idara ya sayansi ya chuo kikuu cha Dar es salaam ndiye binafsi alihusika na ajali hiyo. R. I. P. Dr. Mgaya.
 
Me ni shuhuda gari ni land cruser v 8 no.DFL 598 mpya kabsa me nimeshudia mwenywe na picha nimepost hapo na cyo x trail kama mleta mada anavyoaminisha watu mwenye kujua muhsika ajitokeze liliteketea lote na yeye akiwemo ndani haijajulikana ni nani gari ilivyogonga truck ilianza kupga alam na mkanda ukajilock chakushangaza tulishndwa kumtoa kwenye gari
Hamkuweza kuvunja vioo?
 
Ndugu Wanaudasa,

Ninasikitika kuwataarifu habari za msiba wa Dr. Richard Mgaya wa Idara ya Sayansi na Uhandisi wa Kompyuta kilichotokea usiku wa kuamkia jana. Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara (Dr. Honest Kimaro) kifo cha Dr Mgaya kimesababishwa na ajali ya gari.

Siku ya jana kulisambaa picha kwenye mitandao ya kijamii za gari lilipopata ajali eneo la Mbezi Afrikana baada ya kugongana na lori na kuwaka moto. Mashuhuda walishuhudia gari likiwaka moto na hivyo dereva aliungua moto na kuteketea na hakuweza kutambulika. Hivyo watu wakasambaza ujumbe kwa kutaja plate number za gari lililoungua ili kutafuta utambulisho wa dereva.

Kwa masikitiko makubwa, imejulikana kwamba dereva wa gari hilo alikua ni Dr. Richard Mgaya. Idara ya Sayansi na Uhandisi wa Kompyuta na jamii ya CoICT kwa ujumla imeshtushwa sana na msiba huu.

Dr. Mgaya alijiunga na idara yetu miaka kama minne hivi iliyopita akitokoea masomoni Marekani na alikua ni mtaalamu kijana wa Artificial Intelligence ambayo ni moja ya specialities za computer science zenye wataalamu wachache sana wa kiwango cha PhD hapa nchini mwetu (kama wapo zaidi ya yeye). Taarifa za kwamba aliyeungua kwenye gari hili alikua ni Dr. Mgaya zimeifikia familia yake leo mchana.

Pamoja na ujumbe huu, nimeambatanisha baadhi ya picha zilizopigwa eneo la tukio. Ni msiba mgunu sana kuuelezea na kuukubali.

Mungu mwenyewe awe faraja kwa ndugu, jamaa, wafanyakazi wenzake na familia nzima ya UDSM.
 
Ajali imetupotezea msomi kijana mahiri mno...pumzika panapostahili Dr. Speculations zitakuwa nyingi lakini mwisho wa siku utabaki ukweli mmoja tu... "Dr. Mgaya katutoka milele " pole Taifa pole marafiki na jamaa na poleni sana sana familia na ndugu wa marehemu....mbele yake nyuma yetu....Death is a state not a process...RIP DR.
 
532e1013b9251e6acd6bb0ef1b924df7.jpg

Hiyo ni ratiba ya mazishi ya marehemu dr. Richard Mgaya yatakayofanyika siku ya leo alhamisi ya tarehe 7 april 2016
 
Poleni sana wafiwa Mungu awape uvumilivu wa kimapendo na Faraja, Pumzika kwa Amani Dr Richard Mgaya
 
Majira ya saa kumi na moja asubuhi kumetokea ajali mbaya sana eneo la Mbezi Beach Afrikana.

Gari aina ya Nissana xtrail au Honda ikiwa inatokea Mwenge imegonga kwa nyuma truck na kuungua hapohapo.

Kwa mujibu wa mashuhuda watu wawili waliokuwemo ndani ya gari wamefariki kwa moto wakiwa ndani.

Kwa adabu zangu sitoweza kuweka wala sikupiga picha.

View attachment 334553

View attachment 334554
Bado huna akili na hiyo picha uliyoweka ya ajali ya juzi ina maana gani?
 
Back
Top Bottom