Ajali: Basi la Kampuni ya Ilasi Express limegonga basi la Mbeya Express maeneo ya Igawa

Kulikua na sheria mabasi yote yanayo safiri umbali zaidi ya Km 500 kuwa na madereva wawili.

Lakini pia utakuta dereva jana kalala na kimada na kachelewa kulala. Wote mnajua mapenzi yanavyo maliza nguvu lazima usinzie.

Pia unakuta kwa route ndefu kama hizi dereva anaunga wiki nzima yupo barabarani.

Ajali nyingi zinatokana na mambo ya fuatayo

1. Ubovu wa magari: mabasi kuto fanyiwa servive inavyo takiwa na sijawahi ona traffic wakikagua zile kazi za service.

2. Madereva kuchoka: ni mara chache sana k
Kwa route ndefu kuona madereva wanapokezana na sijawahi ona traffic wakikagua hilo. Mfano route toka mbeya lazima iwe na madereva wawili.

3. Abiria: abiria wapumbavu ambao wanajifanya wanataka kuwahi. Siku moja kidogo nimtukanw mzew mmoja kwa hekima nikamwelekeza kwamba wenzake wenye haraka qana magari yao au wanakqea pipa.
 
Hawa jamaa ni uchovu tu wala sio basis....ngoja niwaeleze kisa cha kweli kilichonitokea mwezi uliopita!

Siku ya safari nilikua natoka Njombe kwenda Kahama! Kwa bahati mbaya basi ambalo nilipanda Njombe to Dodoma liliharibika Iringa ikatulazimu kubadilisha Gari!

Kitendo hiki kikatufanya tuchelewe kufika Dodoma na hivyo nikapata basi linaitwa Mbondo Star kwenda Kahama.

Safari ilianza majira ya SAA 1730hrs. Nilikua siti ya mbele kabisa mlangoni, baada ya kufika Manyoni nilianza kuona kama vile Dereva amechoka! Lakini niliamua kukaa kimya, tulifika Singida kwa shida sana maana alikua analazimisha kuendesha (mwili umechoka) hivyo kupelekea kukoswa koswa Mara kibao!

Baada ya kutoka Singida nikagundua kuwa Kuna nyakati alikua anahama kabisa njiani...na kwenda kwenye Site ya mwingine! Mara mbili au tatu nilimshtua kuwa unasinzia, na mara kibao aliamshwa na taa Kali au honi Kali za malori ya mizigo!

Tulifika Mlima Sekenke akafanya maamuzi ya kijinga sana nusura yatugharimu maisha, ali-overtake kwenye mlima kwenye kona ghafla ni lory lingine linapandisha!

Baadae akasimmamisha Gari, akampa Kondakta, muda huo yapata SAA tano au sita kasoro usiku! Nikajifanya nimelala, akaanza kumuelekeza kuwa akipishana na Gari asilisogelee sana! Yeye akalala pale mbele kwenye godoro.

Baadae akahamia siti za nyuma kulala! Huyu sasa nae ikawa ni kituko, baada ya kufika Nzega na yeye alikua ameshachoka vibaya sana, Gari zima nadhani walikua wamelala isipokua mimi na yeye nadhani!

Akaanza kusinzia huku anaendesha, nikamshtua Mara mbili nakumbuka kabla ya kufika Nata! Baada ya hapo ikawa sasa ni usiku mkali, magari yamepungua sana njiani, watu wamelala, Barbara haiko busy! Aiseee jamaa alihama kabisa kabisa akataka kutubwaga! Nikamuita kwa nguvu akashtuka, akairudisha barabarani.....

Nikatoka kwenye siti yangu nikaenda kukaa nae nikaanza kumpigisha story nakumbuka ilikua tunakaribia KAGONGWA jamaa alikubali kuwa walikua wamechoka! Hadi tunafika Kahama ilikua SAA Tisa usiku.

Nimefupisha ila ile safari ni Mungu tu maana ilikua na matukio mengi ya kutisha
Dah pole Sana mkuu... Na huko njiani hamna traffic
 
Kuna kitu kimoja ambacho seriakali inatakiwa ichukuwe hatua kali: Kizingizio cha kusema ''breki zilifeli''. Gari likifanyiwa service inavyotakiwa na dereva akiendesha kwa tahadhari hikin kisingizio cha break kufeli kitaondoka.
Hao wanakimbia hovyo ndio maana akikuta gari imeharibika hawezi kukwepa au kusimama halafu wanasingizia breki zimefeli
 
Mkuu usirudie kosa hilo tena la kumuacha dereva mchovu awaendeshe.

Next time unapaswa kumshauri asimamishe basi sehemu salama alale kupunguza uchovu maana kama ulishuhudia kuyumbayumba kwa dereva ulikuwa uanelekea kushuhudia mwisho wa safari kabla ya kufika muendako
Hawa jamaa ni uchovu tu wala sio basis....ngoja niwaeleze kisa cha kweli kilichonitokea mwezi uliopita!

Siku ya safari nilikua natoka Njombe kwenda Kahama! Kwa bahati mbaya basi ambalo nilipanda Njombe to Dodoma liliharibika Iringa ikatulazimu kubadilisha Gari!

Kitendo hiki kikatufanya tuchelewe kufika Dodoma na hivyo nikapata basi linaitwa Mbondo Star kwenda Kahama.

Safari ilianza majira ya SAA 1730hrs. Nilikua siti ya mbele kabisa mlangoni, baada ya kufika Manyoni nilianza kuona kama vile Dereva amechoka! Lakini niliamua kukaa kimya, tulifika Singida kwa shida sana maana alikua analazimisha kuendesha (mwili umechoka) hivyo kupelekea kukoswa koswa Mara kibao!

Baada ya kutoka Singida nikagundua kuwa Kuna nyakati alikua anahama kabisa njiani...na kwenda kwenye Site ya mwingine! Mara mbili au tatu nilimshtua kuwa unasinzia, na mara kibao aliamshwa na taa Kali au honi Kali za malori ya mizigo!

Tulifika Mlima Sekenke akafanya maamuzi ya kijinga sana nusura yatugharimu maisha, ali-overtake kwenye mlima kwenye kona ghafla ni lory lingine linapandisha!

Baadae akasimmamisha Gari, akampa Kondakta, muda huo yapata SAA tano au sita kasoro usiku! Nikajifanya nimelala, akaanza kumuelekeza kuwa akipishana na Gari asilisogelee sana! Yeye akalala pale mbele kwenye godoro.

Baadae akahamia siti za nyuma kulala! Huyu sasa nae ikawa ni kituko, baada ya kufika Nzega na yeye alikua ameshachoka vibaya sana, Gari zima nadhani walikua wamelala isipokua mimi na yeye nadhani!

Akaanza kusinzia huku anaendesha, nikamshtua Mara mbili nakumbuka kabla ya kufika Nata! Baada ya hapo ikawa sasa ni usiku mkali, magari yamepungua sana njiani, watu wamelala, Barbara haiko busy! Aiseee jamaa alihama kabisa kabisa akataka kutubwaga! Nikamuita kwa nguvu akashtuka, akairudisha barabarani.....

Nikatoka kwenye siti yangu nikaenda kukaa nae nikaanza kumpigisha story nakumbuka ilikua tunakaribia KAGONGWA jamaa alikubali kuwa walikua wamechoka! Hadi tunafika Kahama ilikua SAA Tisa usiku.

Nimefupisha ila ile safari ni Mungu tu maana ilikua na matukio mengi ya kutisha
 
Japo umeangalia upande mmoja. Je hilo basi lilikuwa limepaki barabarani linagengenezwa walichukua tahadhari? Waliweka alama za usalama?
Kuna kitu kimoja ambacho seriakali inatakiwa ichukuwe hatua kali: Kizingizio cha kusema ''breki zilifeli''. Gari likifanyiwa service inavyotakiwa na dereva akiendesha kwa tahadhari hikin kisingizio cha break kufeli kitaondoka.
 
Mimi nadhani ni uchovu tu wa madereva...basi linaenda tunduma toka dar linafika saa nne usiku na kesho linageuza na dereva saa kumi anatakiwa kuwa macho kuanza kujiandaa..pia unakuta ni dereva mmoja
 
Chanzo cha ajali hiyo ni Basi la Ilasi Express kufeli breki na kwenda kuligonga basi la Mbeya Express kwa nyuma lililokuwa limepaki kwa matengenezo.

Halafu kuna watu wanajiita inspectors wanachungulia uvunguni mwa magari as if wanaangalia usalama kumbe wanatafuta chanzo cha mlungura
 
Back
Top Bottom