Ajali: Basi la Kampuni ya Ilasi Express limegonga basi la Mbeya Express maeneo ya Igawa

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Basi la Kampuni ya Ilasi Express limeligonga basi la Kampuni ya Mbeya Express maeneo ya Igawa mkoani Mbeya usiku wa kuamkia leo Novemba 10, 2019.

Mabasi hayo yalikuwa yakitokea jijini Dar es salaam kuelekea mkoani Mbeya

Taarifa za awali zinasema kuna vifo vya watu wawili mmoja kutoka katika basi la Ilasi na mwingine katika basi la Mbeya Express huku kukiwa na majeruhi zaidi 40

Chanzo cha ajali hiyo ni Basi la Ilasi Express kufeli breki na kwenda kuligonga basi la Mbeya Express kwa nyuma lililokuwa limepaki kwa matengenezo.
IMG_20191110_115250_078.jpeg
 
Haya mabasi ya Ilasi yanapata ajali sana......Lingine liligonga lori pale Morogoro mwezi uliopita.

Owner ni Mkinga?!

cc: Laki si Pesa
Kuna kitu kimoja ambacho seriakali inatakiwa ichukuwe hatua kali: Kizingizio cha kusema ''breki zilifeli''. Gari likifanyiwa service inavyotakiwa na dereva akiendesha kwa tahadhari hikin kisingizio cha break kufeli kitaondoka.
 
Miezi mitatu iliyopita nimenusurika kifo hapo Igawa. Nilikoswa koswa na basi lililoovateki lori nikanusurika kukimbiza gari korongoni

Alama za barabarani haziruhusu mwendo wa kasi wala overtake.

Mabasi yanakimbia sana eneo hilo hivyo ajali nyingi chanzo hao madereva. Pia DTO wa hapo amulikwe yeye na team yake hawasimamii ipasavyo sheria.

Mungu awapumzishe marehemu.
Mungu awape haueni majeruhi wote
 
Hawa jamaa ni uchovu tu wala sio basis....ngoja niwaeleze kisa cha kweli kilichonitokea mwezi uliopita!

Siku ya safari nilikua natoka Njombe kwenda Kahama! Kwa bahati mbaya basi ambalo nilipanda Njombe to Dodoma liliharibika Iringa ikatulazimu kubadilisha Gari!

Kitendo hiki kikatufanya tuchelewe kufika Dodoma na hivyo nikapata basi linaitwa Mbondo Star kwenda Kahama.

Safari ilianza majira ya SAA 1730hrs. Nilikua siti ya mbele kabisa mlangoni, baada ya kufika Manyoni nilianza kuona kama vile Dereva amechoka! Lakini niliamua kukaa kimya, tulifika Singida kwa shida sana maana alikua analazimisha kuendesha (mwili umechoka) hivyo kupelekea kukoswa koswa Mara kibao!

Baada ya kutoka Singida nikagundua kuwa Kuna nyakati alikua anahama kabisa njiani...na kwenda kwenye Site ya mwingine! Mara mbili au tatu nilimshtua kuwa unasinzia, na mara kibao aliamshwa na taa Kali au honi Kali za malori ya mizigo!

Tulifika Mlima Sekenke akafanya maamuzi ya kijinga sana nusura yatugharimu maisha, ali-overtake kwenye mlima kwenye kona ghafla ni lory lingine linapandisha!

Baadae akasimmamisha Gari, akampa Kondakta, muda huo yapata SAA tano au sita kasoro usiku! Nikajifanya nimelala, akaanza kumuelekeza kuwa akipishana na Gari asilisogelee sana! Yeye akalala pale mbele kwenye godoro.

Baadae akahamia siti za nyuma kulala! Huyu sasa nae ikawa ni kituko, baada ya kufika Nzega na yeye alikua ameshachoka vibaya sana, Gari zima nadhani walikua wamelala isipokua mimi na yeye nadhani!

Akaanza kusinzia huku anaendesha, nikamshtua Mara mbili nakumbuka kabla ya kufika Nata! Baada ya hapo ikawa sasa ni usiku mkali, magari yamepungua sana njiani, watu wamelala, Barbara haiko busy! Aiseee jamaa alihama kabisa kabisa akataka kutubwaga! Nikamuita kwa nguvu akashtuka, akairudisha barabarani.....

Nikatoka kwenye siti yangu nikaenda kukaa nae nikaanza kumpigisha story nakumbuka ilikua tunakaribia KAGONGWA jamaa alikubali kuwa walikua wamechoka! Hadi tunafika Kahama ilikua SAA Tisa usiku.

Nimefupisha ila ile safari ni Mungu tu maana ilikua na matukio mengi ya kutisha
 
mimi habari za kulala wanaume wote 35 na wanawake gari zima,halafu mnamwachia roho zenu mwanaume mmoja,ambaye hamjui kaamkaje ndio habari nisizozitaka.

yaani huwa nakosa kabisa sababu ya kulala kwenye gari,na hunifanya kufika safari naumwa kichwa sana.
 
Mabasi yanatakiwa kuwa na fine tofauti na magari madogo. Dereva wa basi anakuwa na abiria wengi na amaesoma masomo ya ziada siyo sawa na wenye vigari vidogo. Hivyo hatutegemei afanye makosa ya hovyo.
 
Back
Top Bottom