Ajali: Basi la Kampuni ya BM Coach lafeli breki maeneo ya Wami

Ajali: Basi la Kampuni ya BM Coach lafeli breki maeneo ya Wami

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,277
Basi la Kampuni ya BM Coach linalofanya safari zake kati ya Morogoro kwenda Moshi limepata ajali leo Novemba 16, 2018 wakati linashuka katika mteremko maeneo ya mto Wami kabla ya daraja.

Kwa mujibu wa taarifa za awali hakuna majeruhi wala vifo isipokuwa abiria kupata mshtuko na taharuki, huku chanzo cha ajali ni basi kufeli upepo kwenye mfumo wa breki na kusababisha gari kutofunga breki vizuri hali iliyopelekea kuteleza kutokana mvua iliyonyesha hivyo dereva wa basi kuamua kulibamiza kwenye Lori lililokuwa kando.
IMG_20181116_123623_214.jpeg
 
yaani, ujinga wake wa kutocheck upepo alipokuwa mizani, ndio upelekee kuharibu mali za wengine!?

Hii si sawa kabisa, dereva awajibike, na bima wasilipe kabisa!
jipeleke mirembe ukapimwe,mali wewe unaona ni bora kuliko uhai wa binadamu mwenzako,umejaa ubinafsi maana hukuwa na ndugu au jamaa yako kwenye lile bus,endelea kujifungia kwenye ivory tower yako ila elewa ipo siku utatolewa na kuingizwa mwingine.
 
Ndege Marubani wakifa Auto Pilot inawaongoza mpaka mwisho wa safari na mnatua salama!?
Basi kusingekuwa na haja ya Marubani.
Ndio maana huwa napanda ndege tu mabasi sio salama.

Imagine mko kwenye mwendo 80kph alafu dereva anafariki ghafla si wote mnaondoka nae??

Bora ndege zina auto pilot.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Back
Top Bottom