AJABU: Chenge aitetea DOWANS ilipwe!

AJABU: Chenge aitetea DOWANS ilipwe!

Sikubaliani na makosa/vitendo mbalimbali vya huyu visenti lakini pendekezo lako la kutaka anyongwe umelitoa kama si kwa jazba basi bila kufikiria. Anyongwe kwa kosa lipi? La kutoa ushauri wa kisheria?
 
Kwa vile kibarua chake karibu kitaota majani anatafuta namna mbadala ya kujikimu.
 
Kwa vile kibarua chake karibu kitaota majani anatafuta namna mbadala ya kujikimu.
Nani ana ubavu wa kukiotesha kibarua cha chenge na wenzake majani? Naona wewe unaota ndoto za mchana na siasa za Tz huzijui kabisaa. Nani wa kusema katika chama cha magamba kukiotesha kibarua cha chenge na wenzake majani? Nape alikurupuka hata mwezi haukuisha akanyamazishwa kimyaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
 
ANDREW J. CHENGE
Mheshimiwa Andrew Chenge ni Mbunge wa Bariadi Magharibi na alikua Waziri wa Miundombinu katika Serikali ya sasa ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Kabla ya hapo, Mheshimiwa Chenge alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa miaka yote kumi ya utawala wa Rais Benjamin W. Mkapa. Kwa wadhifa huo, Mheshimiwa Chenge ndiye alikuwa “mshauri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya mambo ya sheria na … aliwajibika kutoa ushauri kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuhusu mambo yote ya kisheria, na kutekeleza shughuli nyinginezo zozote zenye asili ya au kuhusiana na sheria….”[6] Katika kipindi hicho cha miaka kumi na mbili, Mheshimiwa Chenge amehujumu taifa la Tanzania kama ifuatavyo:
  1. Kama Mkurugenzi katika kampuni ya kigeni ya Tangold Limited alishiriki na/au kufaidika na malipo haramu ya dola za Marekani 13,736,628.73 ambazo zimeelezewa kwa kirefu katika sehemu inayomhusu Gavana Balali;
  2. Kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mheshimiwa Chenge ameshiriki kuishauri vibaya na/au kutokuishauri vizuri Benki Kuu ya Tanzania na kusababisha ufujaji wa mabilioni ya fedha za umma ambayo yameelezewa katika sehemu inayomhusu Gavana Balali;
  3. Kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mheshimiwa Chenge ameshiriki moja kwa moja katika kutoa ushauri kwa Serikali na/au Wizara ya Nishati na Madini kuingia mikataba mibovu na makampuni mbali mbali ya madini ya kimataifa ambayo kwayo taifa limepoteza mabilioni ya fedha za kigeni. Kwa mfano, katika hotuba yake Bungeni tarehe 6 Novemba 2006, aliyekuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa Bernard Membe alitoa taarifa kwamba katika kipindi cha miaka mitatu hadi kufikia 2006, makampuni ya uchimbaji dhahabu yaliyoko Tanzania yaliuza dhahabu yenye thamani ya shilingi bilioni 2,340 wakati ambapo makampuni hayo yalilipa mrahaba na kodi nyinginezo kwa Serikali za shilingi bilioni 72. Katika kikao cha Bunge la Bajeti la mwaka 2007, aliyekua Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa William Ngeleja aliliambia Bunge kwamba katika kipindi cha kuanzia mwaka 1998 Mgodi wa kwanza wa dhahabu wa Lusu Nzega ulipofunguliwa hadi mwaka huu, makampuni ya uchimbaji dhahabu yaliuza nje dhahabu yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 2.614 wakati Serikali ikiambulia mrahaba wa dola milioni 78 tu! Endapo Mwanasheria Mkuu wa Serikali Chenge angeishauri vema Serikali ya Jamhuri ya Muungano kama alivyotakiwa na Katiba ya nchi yetu, taifa lisingekuwa linapoteza utajiri wake wa madini kwa kiasi kikubwa namna hii.

Source: List of Shame
 
Nakumbuka Bunge lililopita, Mbunge mpya kwa tiketi ya cdm, Tundu Lissu, alipokuwa anajitafutia umaarufu Bungeni kwa kufanya u"tundu" na kuzua malumbano kwa kila hoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, alisimama Chenge na kumpa Tundu hoja moja tuu ya kisheria ambayo ilimfanya Tundu kuwacha utundu wake wa kulumbana, kwani kwa pale ilidhihirika wazi kuwa Tundu ni katoto kwa Chenge kisheria. Nani anaekumbuka?

Kwa mantiki hiyo, ikiwa Chenge kasema fedha ya Dowans walipwe, basi ujuwe kaiona sheria kwa jicho la wazi na anajuwa kutokuwalipa Dowans kunaweza kuleta utata zaidi na kuliingiza Taifa kwenye utata zaidi, Jee, inawezekana kuwa hata Symbion hawatakubali kulipia mitambo ambayo bado ina deni?
Hiyo picha yako inaonesha una busara kumbe!!! huo utaalam wa sheria alionao sana huyo Chenge si ndio ule ulioitia aibu serikali yake mpaka waziri wa mambo ya nje analalama kwa waingereza? Zaidi ya miaka kumi iliyopita alikuwa mbumbumbu wa kisheria tena akiwa mwanasheria mkuu, akaishauri serikali kununua rada kwa double price hakuona athari zozote. Huo ujuzi kautoa wapi leo kuona athari za kutoilipa Dowans?
PELEKA UJINGA WAKO HUKO KIBARAKA WA MAFISADI WEEE.
 
Awasilisha ushauri mkali wa kisheria Uingereza

Asema kesi ya kupinga tuzo nchini haina nguvu

Mwanasheria Mkuu wa zamani wa serikali, Andrew Chenge, ameamua kuitetea kampuni ya Dowans ilipwe na serikali ya Tanzania Sh. bilioni 94 kama ilivyoamriwa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro (ICC).

Chenge ametoa utetezi kwa niaba ya mlalamikaji kwenye shauri la usuluhishi kati ya walalamikaji wawili ambao ni Dowans Holdings SA akiwa ni mlalamikaji wa kwanza na Dowans Tanzania Limited mlalamikaji wa pili dhidi ya Kampuni ya Umeme nchini (Tanesco) ambaye ndiye mdaiwa.

Mbali ya kuwa mwanasheria mkuu wa serikali, Chenge pia amekuwa waziri katika serikali ya awamu ya nne, akianzia Ushirikiano wa Kimataifa, kisha Ujenzi (wakati huo Miundombinu) ambako alijiuzulu kwa sababu ya sakata la rada. Katika sakata la rada, Chenge alikuwa mtuhumiwa muhimu, na sakata hili liliisha kwa Kampuni ya BAE ya Uingereza kukubali kulipa fidia kwa uzembe wa kuweka kumbukumbu, na kukwepa kigingi cha rushwa.

Katika maelezo ya Chenge ambayo yameelezwa kuwa ni ushauri wa kitaalam, uliotolewa kwa maandishi Mei 6, mwaka huu katika Mahakama Kuu ya Uingereza, kitengo cha Biashara unalenga kuhalalisha malipo ya tuzo kwa kampuni ya Dowans iliyoamriwa kulipwa na ICC.

Katika maelezo yake hayo yanayorejewa kuwa ni ‘Ripoti ya kitaalamu ya Andrew Chenge', anaanza utangulizi wake kwa kueleza kuwa yeye ni Andrew Chenge anayeishi katika kiwanja namba 240, Nyumba namba 546, Barabara ya Ghuba, eneo la Oysterbay jijini Dar es Salaam Tanzania Anaendelea kueleza katika maelezo yake kuwa, anatoa maelezo hayo kufuatia ombi la Stephenson Harvard, wakili wa walalamikaji na katika kuitikia barua yao ya Aprili 15, mwaka huu ambayo bila ya viambatanisho vyake imenakiliwa kama ushahidi namba "AJC 1"

Aliendelea kueleza kuwa alipata Shahada yake ya Sheria (LLB) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1972. Alisema baada ya hapo alijiunga na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali na baada ya hapo kwa muda wa miaka minne alikwenda Harvard Marekani, Benki ya Dunia na katika kazi za kibinafsi, kisha alirejea kwenye idara ya sheria za kiraia na za kimataifa iliyokuwa katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali mwaka 1978.
Chenge alisema aliteuliwa kuwa Mwanasheria Mwandamizi wa serikali mwaka 1988 na Naibu Mwanasheria Mkuu na Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria mwaka 1991.

Alisema aliteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa serikali ya Tanzania mwaka 1993 ambapo alishikilia nafasi hiyo hadi Desemba mwaka 2005. Alisema alichaguliwa kuwa Mbunge wa Bariadi Magharibi mwaka 2005 na hadi leo anaendelea kuishikilia nafasi hiyo. Alisema nakala ya wasifu wake (CV) imetolewa kama kielelezo "AJC2"
"Sasa nitashughulika na hoja na maswali yaliyojitokeza kwenye barua ya Stephenson Harwood. Ninaitoa katika kielelezo"AJC3" taarifa ambayo nimeirejea katika ripoti yangu hii ambayo marejeo yake katika namba za kurasa kwenye AJC 3 zimekolezwa," anasema Chenge.

Katika maelezo yake ya utetezi ya kuzifafanua hoja na maswali yaliyojitokeza katika barua waliomwandikia walalamikaji, Chenge ameangalia ‘utawala wa kisheria wa kuipinga tuzo iliyotolewa katika Mahakama za Tanzania' akiitumia sheria ya usuluhishi ya mwaka 2002.

Alisema pamoja na vifungu vyote vilivyoondolewa, vilivyorejewa na vilivyorekebishwa kuhusiana na suala linalohusu tuzo, kanuni ambazo bado zipo lazima zisomwe pamoja na sheria ya usuluhishi ya mwaka 2002 ambapo nakala ya sheria hiyo na kanuni za usuluhishi za Tanzania za mwaka 1957 anaeleza kuziambatanisha.

Chenge alisema sababu pekee zinazoweza kuifanya tuzo hiyo ikapingwa zimeelezwa katika sheria hiyo ya mwaka 2002 na hasa katika kifungu cha 16 ambacho kinaruhusu tuzo kupingwa ikiwa tu limetolewa kutokana na mwenendo mbaya au kama imepatikana isivyo kihalali.

Alisema chini ya kifungu cha 15, tuzo inaweza kurudishwa kwa ajili ya masahihisho katika mahakama iliyotoa maamuzi hayo. Akizungumzia namna ya kuipinga hukumu ya tuzo chini ya kutolewa kwa mwenendo mbaya (misconduct), Chenge alisema neno hilo halikutolewa maana yake kwenye sheria ya usuluhishi ya mwaka 2002 na kwamba hakuna mamlaka yoyote Tanzania ambayo imetafsiri neno hilo na kwamba kwa maoni yake mahakama za Tanzania zitaliangalia suala hilo kwa ufinyu na kutilia mkazo kama mahakama au mjumbe wake hakutenda haki au isivyo sawa.

Baada ya hapo, Chenge alizungumzia pingamizi dhidi ya tuzo lililowasilishwa na Tanesco na wadau wengine na hasa maswali manne yaliyotolewa katika aya ya 10 iliyotolewa kama kilelezo "AJC 1" . Alisema kwa kuangalia alichopewa yeye, pande hizo mbili katika mgogoro huo zilikubaliana kutumia sheria za Texas katika mgogoro wao na kwamba wakati wanakubaliana Tanesco hawakuhoji uhalali wa kuzitumia sheria hizo, hivyo anaona hoja ya Tanesco ya kuhoji maamuzi yaliyofikiwa kwa kutumia sheria za Texas haina mashiko.

Akizungumzia aya ya sita ya pingamizi la Tanesco, Chenge alisema kwamba ' inaonekana aya hiyo inakubaliana na maoni yake kwamba kinachounda mwenendo mbaya ni mapungufu ya taratibu za haki. "Kwa hiyo siamini kama sababu hizo 11 walizotoa zinaunda mwenendo mbaya."

Akizungumzia pingamizi la Tanesco la aya ya tisa lisemalo kwamba tuzo iliyotolewa ina makosa kisheria katika macho ya kumbukumbu, Chenge alisema hilo ni suala la ushahidi na si la sheria kwa msingi kwamba mahakama ina mamlaka ya kuingilia.
Alisema kesi ya D.P Shapriya imeshalifafanua vizuri sana suala hilo.

Alimalizia kwa kusema kwamba maoni yake kwa aya ya 10 ya pingamizi la Tanesco kwamba tozo iko kinyume cha sera ya umma haina nguvu ya kushinda kwa sababu zilizoelezwa katika aya ya 15.

NIPASHE ilimwuliza Chenge anajisikiaje anapotaka kuibana nchi yake ilipe kampuni hiyo ya kigeni na alijibu kuwa hawezi kuzungumzia mambo yasiyomhusu na alimtaka mwandishi kuendelea na shughuli zake.

"Nimesema siwezi kuzungumza masuala ambayo hayanihusu na naomba uendelee na shughuli zako inamaana hunielewi?" alisema Chenge kwa kifupi na kuhoji kisha akakata simu.

Source: Nipashe 1st June 2011

my take: magamba sasa inageuka na kuwa 'ama zangu ama zako'
 
Nakumbuka Bunge lililopita, Mbunge mpya kwa tiketi ya cdm, Tundu Lissu, alipokuwa anajitafutia umaarufu Bungeni kwa kufanya u"tundu" na kuzua malumbano kwa kila hoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, alisimama Chenge na kumpa Tundu hoja moja tuu ya kisheria ambayo ilimfanya Tundu kuwacha utundu wake wa kulumbana, kwani kwa pale ilidhihirika wazi kuwa Tundu ni katoto kwa Chenge kisheria. Nani anaekumbuka?

Kwa mantiki hiyo, ikiwa Chenge kasema fedha ya Dowans walipwe, basi ujuwe kaiona sheria kwa jicho la wazi na anajuwa kutokuwalipa Dowans kunaweza kuleta utata zaidi na kuliingiza Taifa kwenye utata zaidi, Jee, inawezekana kuwa hata Symbion hawatakubali kulipia mitambo ambayo bado ina deni?
kwa ulichokiandika hapo unataka kutuambia kwamba Chenge anajua sana sheria siyo?Inawezekana kwamba anaijua kweli sheria lakini kujua kwake sheria hakujaisaidia hii nchi!Serikali iliingia mikataba mibovu ya madini Chenge akiwa mwanasheria mkuu,je kwa wakati huo alikua hajui sheria au alikua na manufaa binafsi?kama nitakua sahihi basi inawezekana pia akawa ana manufaa binafsi katika hili suala la Dowans.Tatizo si Chenge kujua sheria bali ni kujua kwake sheria kunaisaidia nini hii nchi!
 
Back
Top Bottom