GE2025 Kesi ya Tundu Lissu: Pingamizi la Jamhuri lagonga mwamba

GE2025 Kesi ya Tundu Lissu: Pingamizi la Jamhuri lagonga mwamba

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,152
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam mapema leo, Jumatatu Oktoba 13.2025 imetoa 'uamuzi mdogo' kufuatia pingamizi lililokuwa limewekwa mwishoni mwa juma lililopita na upande wa Jamhuri katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Tundu Lissu

Pingamizi hilo lilitokana na mshtakiwa ambaye anajitetea mwenyewe kwenye kesi hiyo kuomba kielelezo D1 (maelezo ya maandishi ya shahidi wa pili wa Jamhuri Inspekta wa Jeshi la Polisi John Kaaya aliyoandika akiwa kwenye Kituo cha Polisi) cha PW2 ambaye ndiye shahidi, upande wa Jamhuri ulipinga kielelezo hicho kupokelewa Mahakamani hapo kutokana na kile kilichoelezwa kuwa mshtakiwa hajazingatia taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa sheria pale mshtakiwa anapotaka kumuhoji shahidi kuhusu maelezo aliyotoa hapo awali

Katika kujenga msingi wa pingamizi lao, Mawakili wa Jamhuri Ajuwaye Nzegeli (Wakili wa Serikali Mkuu) na Job Mrema (Wakili wa Serikali Mkuu) waliipitisha Mahakama kwenye marejeo ya mashauri mbalimbali ya aina hiyo yaliyoamuliwa na Mahakama Kuu na Mahakamani ya Rufani, marejeo ambayo katika uamuzi wake Mahakama imesema hoja hiyo haijabishaniwa na pande zote mbili

Katika uamuzi wake, jopo la Majaji watatu (3) wanaosikiliza kesi hiyo wakiongozwa na Jaji Danstan Ndunguru wamesema mshtakiwa amefuata taratibu zote zinazohitajika kisheria katika kuomba kielelezo hicho kupokelewa Mahakamani

Wamesema kwa mujibu wa taratibu za kisheria panapotokea mazingira ya aina hiyo kuna hatua tatu (3) za kufuatwa, kwanza ni shahidi kusomewa maelezo yake, baada ya hapo mshtakiwa atabainisha maeneo anayoona yana 'kasoro' kwa ulinganifu ili ayafanyie dodoso na kwamba kwa muktadha wa kesi pingamizi hilo Mahakama imeona kuwa mshtakiwa alibainisha maeneo 45, na jambo la tatu ni kumuhoji mshtakiwa endapo yuko tayari kielelezo hicho kipokelewe Mahakamani na kitumike kama sehemu ya ushahidi wake, hatua ambazo zote zilifuatwa

Kufutia maamuzi hayo ya Mahakama, sasa kielelezo hicho (D1) kinakuwa cha kwanza cha mshtakiwa Tundu Lissu kuwasilishwa Mahakamani hapo, na sasa kesi hiyo inaendelea ambapo mshtakiwa anaendelea kumuhoji maswali ya dodoso (cross examination).

Pia Soma: Tundu Lissu alivyofikishwa Mahakama kuu leo Oktoba 13, 2025 kuendelea na mahojiano na shahidi wa pili
1760339649201.png
 
Hizo hoja za Jamhuri anazoonesha Jaji kuzipinga na kumpa faida Lissu ni vile vitu rahisi ambavyo haviwezi kuharibu muelekeo wa kesi kwa jinsi ambavyo wali plan.

Yale mapingamizi mazito ambayo yalikuwa yametolewa na Lissu ikiwemo kuiomba Mahakama kufuta kesi, huwezi kuona yanakubaliwa hata kama ni reasonable kiasi gani.

So hapa ni kama wamewatafutia heading kina Millard Ayo ili kuionesha dunia kuwa kuna fairness kwenye court.
 
True! Mpango mzima wa hii kesi ni kumalizika katika mazingira ya kutatanisha baada ya Samia The Killer kuapishwa na kuanza muhula wa pili.
 
Huyu mwamba Tundu Lissu ana akili nyingi mpaka zimepitiliza! Inspekta amekuja kichwa kichwa kutoa ushahidi wake wa mchongo na kujikuta ameingizwa king! Kwa hali hii tayari itakuwa ni kikwazo siku zijazo kwa mawakili vilaza wa serikali.

..kesi hii ilipaswa kuonyeshwa mubashara ili vijana wanaosomea sheria wajifunze kutokana na kinachoendelea mahakamani.

..TAL alimzunguka shahidi Kaaya kwa kuanza naye mbali sana kwa maswali na ghafla shahidi akawa amenasa kwenye mtego.
 
Hizo hoja za Jamhuri anazoonesha Jaji kuzipinga na kumpa faida Lissu ni vile vitu rahisi ambavyo haviwezi kuharibu muelekeo wa kesi kwa jinsi ambavyo wali plan.

Yale mapingamizi mazito ambayo yalikuwa yametolewa na Lissu ikiwemo kuiomba Mahakama kufuta kesi, huwezi kuona yanakubaliwa hata kama ni reasonable kiasi gani.

So hapa ni kama wamewatafutia heading kina Millard Ayo ili kuionesha dunia kuwa kuna fairness kwenye court.

..Majaji na Wanasheria ya Serikali wamejichanganya.

..Kilichotokea ni Majaji na Mawakili wa serikali kulazimika kumeza ndoana yao wenyewe

..Mwanzo walidhani wanamkomoa TL lakini sasa maamuzi yao ya awali yamekuja kuwaathiri upande wa serikali.
 
Back
Top Bottom