AJABU: Chenge aitetea DOWANS ilipwe!

BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,507
11,883
Katika kudhihirisha uswahiba na ufisadi wa mapacha watatu, Chenge amewasilisha pingamizi la kisheria kutetea DOWANS ilipwe na serikali ya Tanzania.

Source: Nipashe la leo

=============================================
DOCS:

Chenge1.jpg

chenge2.jpg


More DOCS; DOWNLOAD THE ATTACHMENTS BELOW
 

Attachments

  • chengessubmissioninlondon1.zip
    1 MB · Views: 91
  • chengenadowans2.zip
    1 MB · Views: 82
Mbunge wa Bariadi pamoja na tuhuma nzito zinazo onyesha negative atitude kwa WATZ kama vile tuhuma dhidi ya rada, kumiliki mabilion ya fedha nje ya nchi, kutia mkono wa kumuondoa spika SITTA aliye pendwa na WATZ wengi kuwa spika wa Bunge.

Leo napata habari mbaya kwetu kuwa CHENGE amepeleka ushauri mzito wa kisheria ili DOWANS walipwe sh. 94 bil.

Source GAZETI LA NIPASHE.

CHENGE kama kuna kosa WATZ wamekufanyia basi wasamehe bure, mbona wao wanakupenda wamekupa ubunge (kama hukuchakachua) kuonyesha wanakupenda tusamehe tu hata kama una mgawo DOWANS.
 
That's what's up! Na hii serikali isivyo na hela...mbona walimu watalipwa mshahara wa july, december ??
 
Nimeshtuka kweli niliposkia hbr hyo,nami nikajiuliza AMEJITOLEA AU AMEOMBWA?AU NDO ANADHIHIRISHA YEYE NI GAMBA?SO HATA AKITEMWA LIWALO NA LIWE?
 
Vijisenti sasa ameamua kuanika makucha yake ya kifisadi na kutojali wananchi wake. Sijui wanamchagua kwa vigezo gani kuwa mbunge huko jimboni kwake, anazo sifa kamilifu za kutokua binadamu wa kawaida.
 
kwani mliambiwaje wakati wa uchaguzi???

CCM wakiendelea kutawala ndo tutazidi kwenda kuzimu
 
kuna njia nyingine ya kumnyonga chenge tofauti na hukumu ya mahakamani?Maana mpaka sasa anajiita mr clean
 
Heheheheheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee,

Watanzania tutakoma kudadeki!
 
katika kudhihirisha uswahiba na ufisadi wa mapacha watatu,chenge amewasilisha pingamizi la kisheria kutetea dowans ilipwe na serikali ya tanzania.source nipashe leo
Bongolala, wakati nasubiri kulisoma hilo Nipashe, ningependa kusisitiza mahitaji ya kisheria na mahitaji halisi ni vitu viwili tofauti. Mahitaji ya kisheria ni laz`ima yatekelezwe no matter what, hata kama sio mahitaji halisi.

Tozo la Dowans lililotolewa na ICC ni hitaji la kisheria, kwa mujibu wa mkataba husika, uamuzi wa ICC ni uamuzi wa mwisho, haupingiwi na mahakama yoyote labda kufanyiwa mapitio na ICC yenyewe, hivyo kitendo cha kuusajili mahakama za nchini, ni kwa lengo la kuusajili uamuzi ule kwa utekelezaji tuu.

Siungi mkono tozo hiyo ya ICC kwasababu sio tozo halali, ila kisheria, maadamu wanasheria vichwa maji wetu waliukubali ule mkataba, na hivyo ndivyo mkataba unavyosema, then tozo hiyo imehalalishwa na mkataba mbovu ule, hivyo toso ile ni halali kisheria.

Nawaombeni wana jf na wananchi wote wa Tanzania, lazima tuukubali ukweli mchungu kwa kumeza kidonge kichungu cha tozo hii, tutatake tusitake, lazima tutalipa tuu, hatuna popote pa kutokea unless Tanzania kama nchi, tujitoe ICC na kuwafukuzia mbali hawa wanyonyaji wote wanaojiita wawekezaji wa kwendo makao n a mitaji yao, wakatumie fedha zao kutengeneza madini yao na sisi watuachie almasi zetu, Wasukuma tuzichezee bao, na dhahabu zetu tuziache humo humo ardhini, tubaki na umasikini wetu huku tumekalia malia zetu, kuliko kuwaruhusu wazipore kubadilishana na pipi huku wakituacha na umasini wetu palepale.
 
hata kama ungekuwa wewe,ungefanyaje? Watanganyika wenyewe wamelala,afanyaje? Anatanua night clubs kama kawaida (last weekend nilimuona Club San Siro saa 7 usiku), anatanua mitaani kama kawaida, kila kukicha anabandikwa vyeo tu!! Ilibidi apewe mkwara kimatendo japo mmoja tu kuonyesha tunam-mind!!
 
Watanzania watamnyonga kiaina paomoja na wadhamini wao ccm ambao wamekaa kimya kama vile hawapo tena, marehemu. Hawamuoni. Bora wangetii kauli za vijana wao, akasemee madudu yake nje ya CCM, sasa madhali wanamwona ni almasi basi itakula kwao, Wewe ngojea tu.
 
Jee kuna sababu yoyote ya maana kwa kutumia huduma ya mtu halafu usimlipe?
 
Kwa nchi kama China Mafisadi hunyongwa..hivi haoni aibu.
Mkuuu tatizo la TZ hatuna wazalendo wa ukweli ndiyo maana kesi nyingi hata za ushindi wa wazi serikali inashindwa Hi ni sababu iliyo nifanya nimeombe atumie abinadamu ili atusame BURE tuu !!!!!
 
Back
Top Bottom