Wanasema sikuhizi ukimwi ni kama mafua,
Usiamini, wanaosema ni wale wasio ugua..
Wewe ukihisi unataka kuwamaliza mabinti wazuri wote, tambua Mungu hajachoka kuwaumba..
Ukitaka kila anayekuchekea upite nae, utakosa wa kulia nae wakati ambao hakuna utani wa kukuchekesha, umekonda unagofya
Kama wewe fahari yako ni kuwasimulia wana jinsi unavyo waumiza..
Kesho itakosekana leso kwaajili ya machozi ya dada yako, kwa kuumizwa vilevile..
Leo wanakusifia kwa kupiga kila mitandaoni huko
Siku nyingine watakusifia kwa kumaliza uji bila kutapika, stuka...
Sikia mwanangu, Zipu mbovu..
Watu wanaumwa na wana hasira kwa kuambukizwa.
Na furaha yao iliyobaki ni kuusambaza ugonjwa katika namna ileile waliyoipata wao.
Wewe jifanye kanyaga twende, tutakuzika na kilo 13, kama kiroba cha sukari..
Chagua manzi moja isiyokupa miwasho na fangasi, ishi nayo afu fanya maisha..
Nawahusia na kuihusia nafsi yangu..