Airtel sasa ni wezi?

Vijisenti

JF-Expert Member
Mar 11, 2011
544
328
Hawa Airtel sasa wananipa mashaka, nimeweka tsh 2000 nimeongea sek kama 20 imekata na hela imeisha,
nikaweka tsh 1000 nimeongea sekunde chache imebaki tsh 71. Hiyo sh 71 haitaki kwenda kokote hata
kwenye Airtel yenyewe eti huna salio la kutosha! Jamani inakuwaje kwa mtandao mkubwa kama huu?

Huduma kwa wateja toka saa 12 wanahudumia wateja wengine, nimekaa hewani nusu saa nasubiri nimechoka. Sasa ndo kabisaaa kila nikipiga jaribu baadaye huwezi kuunganishwa wanaongea na wateja wengine!

Huu ni wizi mkubwa hata mimi nimekumbana na hilo kwa asubuhi hii nimeweka vocha ya sh 1000 napiga simu naambiwa salio lako halitoshelezi napiga huduma kwa wateja naambiwa tunahudumia wateja wengine kwa sasa toka saa moja asubuhi.Bado niko ktk duka nililonunua vocha kila mteja anayekuja anasema usiku nimezima simu ikiwa na salio zaidi ya sh 2000 cha kushangaza asubuhi nakuta hakuna salio nikamuuliza wewe unatumia mtandao gani akasema airtel

Mimi nilidhani ni kwangu tu sababu siitumii sana hiyo airtel. Kweli tunaibiwa sana aisee

Nimeongea na rafiki yangu ambaye ni Mdau wa Kampuni hiyo ya Wahindi... ameniambia kuwa wana-experience tatizo kubwa la OVERCHARGING...Mpaka sasa hawajajua cause ni nini??? Mteja akipiga LOCAL CALL ana-charge-wa kama vile amepiga INTERNATIONAL...Kama ccr airtel angeingia huku akatujuza ingekuwa poa... ewe ccr airtel uko wapi...

Hao wacheze na watu wao wa IT hata yule ambaye hajapiga simu anachajiwa kama alikuwa anaongea na majini au?? Kama ni dili wamechezewa ili kuichafua kampuni ili wakimbiwe na wateja wahamie kwenye mitandao yao inakuwaje??????

Mimi nilidhani ni kwangu tu sababu siitumii sana hiyo airtel. Kweli tunaibiwa sana aisee
Na mimi dada, naona turudi kwenye nyumba yetu ileile ndogo, Maana tumehamia huku nyumba kubwa
Mchwa wameanza kula nguo zetu. Nimeweka vocha za 3000 imeliwa chini ya dk 1.

Hata mimi naona bora turudi kwenye kale kagari ketu kadogo hili libasi naona spidi zake kwenye kona dereva analala na 180 sijui kama tutafika salama bora kale kagari ketu slowly but sure!!!!!!

network mbovu haifanyi vizuri kuna mikaruzo kwenye sauti alafu mara kimyaa husikii wala unayeongea nae hasikii.juzi ukituma msg inakwambia failed na ukiingia net haifanyi kazi.niliwapigia nimesubiri dakika arubaini.walicho nijibu kuna tatizi la kiufundi.dah yaani ti.. ndio safi.

Loh mumeniamsha kutoka usingizi mzito maana mimi huwa naweka kama 20000 na wala siangalii natwanga tu. Ila juzi nikaona sijakaa vizuri imekata nikashangaa sana.

Mi wamenila 16,000 jana nikapagawa. Leo wametuma sms kuwa wanarudisha refund, ndo naisubiria hapa kwa hamu, ila isije ikawa mambo ya yesu mpaka leo hajarudi, lakini bado tunamsubiri kwa hamu!

Hawa Airtel sasa wananipa mashaka, nimeweka tsh 2000 nimeongea sek kama 20 imekata na hela imeisha,

nikaweka tsh 1000 nimeongea sekunde chache imebaki tsh 71. Hiyo sh 71 haitaki kwenda kokote hata

kwenye Airtel yenyewe eti huna salio la kutosha! Jamani inakuwaje kwa mtandao mkubwa kama huu?

Huduma kwa wateja toka saa 12 wanahudumia wateja wengine, nimekaa hewani nusu saa nasubiri nimechoka. Sasa ndo kabisaaa kila nikipiga jaribu baadaye huwezi kuunganishwa wanaongea na wateja wengine!

kama ndio hivyo wewe uwe unaweka miatano tano..

sina uhakika sana na hilo la airtel, ntalifanyia uchunguzi. nna wasiwasi na uhusiano wako na hiyo picha yako hapo

wanachangia pesa kutatua tatizo la umeme nanikwamitandao yote mpaka ikifika dec tatizo la umeme litakuwa historia kwa wale wote waliostukia ishu hii mnaombwa muwe kmya na muendelee kuweka vocha kutoa ni moyo

@&&#)(YZ zao, wamekula elfu tano yangu asubuhi asubuhi nikashindwa kuwasiliana na familia,nilweka vocha usiku wakanipa ofa eti kuanzia saa tano hadi saa kumi na mbil asubuhi, nimeamka saa kumi na moja kupiga wakalamba elfu tano yangu chini ya dakika moja, nimeingáta line yao ila nimekumbuka kesho nina apointment muhimu na namba inayojulikana ni hiyo ya airtel, anyway ndio wanaelekea kunipoteza hivyo

Mi nimeweka Tsh 10,000, nimeongea sekunda chache zikaisha zote. Something is very wrong with their system au staff wao wa IT wanafanya ujanja wa kuibia wateja, kwnai nilipongeza Tsh 10,000 nyingine wakanikata kikawaida. Itakuwa wanaibia wateja kidokidogo then wanaresale hizo credit. Na kama ulivyosema namba huduma kwa wateja haipatikani.

Back
Top Bottom