yaani hiyo yako imenikumbusha siku fulani. nimeenda zangu kwa wakwe zangu asubuhi kuacha gari mwenyewe nasafiri. nipo nasalimiana na mama mkwe, simu inaingia, kupokea ni mdada fulani kaanza na matusi hata hajanisalimu. namwuliza wewe nani ananiambie nimwulize mwenye hiyo namba aliyopiga.... madai yake namba anayopiga ni ya mumewe na jana hajalala home..... palikuwa patamu.
mbaya zaidi hiyo siku nilikuwa naenda sehemu kusimamia harusi, na hapo nimekuja kuacha gari kwa wakwe, nipo na wazazi wa bibi harusi wananisubiri tuondoke na gari lao. ile siku nzima nilikuwa natukanwa na namba tofauti tofauti. kwanza nilikuwa namwonea huruma sana huyo dada, lakini nikajua kuwa ni mshari. yule baba wa bibi harusi akaniambia nimpe namba ampigie yule dada, sasa kwa vile ni mzee fulani nikamwambia aache tu asije akapokea matusi akashindwa kusherehekea harusi ya binti yake. Baadae karibia tunaingia kanisani akanipigia mkaka, naye ananiomba nimwachie mume wa watu arudi kwa mkewe...... nikamwambia sasa kwa kirefu sana huyo kaka kuwa huyo mume hata sijawahi kumsikia, na namba wanayopiga ni yangu...... naona yule kaka alinielewa wakamsaka yule kaka sijui hata kilichoendelea, lakini sikupata tena simu yake.
baada ya siku 2 nikataka kumpigia yule dada kumwambia mbona hajaniomba msamaha kwa yale matusi yote.......nikaamua kumpotezea