Airtel ndiyo mtandao wa ovyo zaidi Tanzania

Restless Hustler

JF-Expert Member
Apr 9, 2017
4,742
17,983
Jina langu Ni la Kimasai. Nilipiga simu customer service Airtel akapokea maza Mwenye lafudhi ya kichaga, nikaeleza shida yangu. Akaniambia nitaje namba ya simu, nikamuambia sijaishika maana lain bado mpya. Nikamuuliza wewe si unaona hapo lakini?

Akaniuliza wewe ni Masai wa wapi hujui hata namba yako?🙄 Nikamuuliza umasai unahusikaje hapa? Akanipandishia sauti, akaanza akanifokea hadi nikachukia. Nikamumbia acha kunikashifu mimi siyo Mtoto wako. Akaniambia ahsante kwa kuchagua Airtel, Nakutakia mchana mwema. Nikamuambia fala Wewe 😅

Alafu siyo Mara ya kwanza kuzinguana nao.

Kuna kipindi nilikuwa napewa vocha (elfu 30 kila mwezi) na Ofisini nilipokuwa nafanya kazi na ilikuwa inawekwa Kama muda wa maongezi. Sasa ikawa Mara nyingi kila nikiwekewa hiyo vocha, baada ya sekunde chache nikijiunga kifurushi naambiwa salio lako halitoshi! Kuangalia salio nakuta 29,600(wamekata 400).

Awali Niliwapigia wakaniambia Kuna huduma ya burudani umejiunga wakanielekeza namna ya kujitoa, nikapiga menyu yao Nashangaa inaonyesha hakuna huduma niliyojiunga! Nikawa mpole, nikatafuta Tsh 400 ili ifike elfu 30 nijiunge kifurushi cha mwezi.

Mwezi uliyofuata Airtel wakarudia Tena kukata Tsh 400, nilpowapigia sababu Ni zilezile. Kwa ufupi Ndiyo ukawa Mchezo wao.

Mara mwisho nikawapigia wakaniambia Nilikuwa nimewasha data kabla ya kujiunga. Nikawaambia Siyo kweli Maana hii lain haikuwa hewani na sasaiv ipo kwenye Simu ndogo isiyo na internet, Sasa data nimeiwasha saa ngapi? Huyo dada akaanza kunifokea, Hadi nikaamua kubadilishana lain ya kupokelea vocha ofisni.

Kwa ufupi Airtel ni kampuni isiyo na customer service Representatives na ni wezi wakubwa.
 
Haya makampuni karibia yote yana hizo tabia za kukata salio.Mimi kila nikiweka salio napokea jumbe kwamba nimeungwa kwenye huduma za shilingi 100 au 200.

Wanaelekeza mwisho kama hautaki huduma hiyo jiondoe kwa namba (mfano)*149*83#.Cha ajabu,unafuata walichokuelekeza hadi mwisho na hawakuondoi.Na linakuwa zoezi la kukukata salio kila mara.Huu ni uhuni wenye mchanganyiko wa wizi.
 
Jina langu Ni la Kimasai. Nilipiga simu customer service Airtel akapokea maza Mwenye lafudhi ya kichaga, nikaeleza shida yangu. Akaniambia nitaje namba ya simu, nikamuambia sijaishika maana lain bado mpya. Nikamuuliza wewe si unaona
Nakubaliana na wewe kuhusu huduma kwa wateja yao, mimi nilijitowa airtel zamani sana, nikajitowa na voda, wote hao kwa ajili ya customer service zao.

Tigo customer care wako vizuri sana, naona ndiyo bora zaidi, zamani ndiyo walikuwa wabovu zaidi. Sasa Tigo wanaongoza kwa huduma kwa wateja. No doubt.
 
Jina langu Ni la Kimasai. Nilipiga simu customer service Airtel akapokea maza Mwenye lafudhi ya kichaga, nikaeleza shida yangu. Akaniambia nitaje namba ya simu, nikamuambia sijaishika maana lain bado mpya. Nikamuuliza wewe si unaona hapo lakini?
Umenikumbusha machungu sana kuna kidada hicho Cha Airtel kichaga Cha kipumbavu sana sana. Airtel kampuni ya hovyo.
 
Haya makampuni karibia yote yana hizo tabia za kukata salio.Mimi kila nikiweka salio napokea jumbe kwamba nimeungwa kwenye huduma za shilingi 100 au 200.Wanaelekeza mwisho kama hautaki huduma hiyo jiondoe kwa namba (mfano)*149*83#.Cha ajabu,unafuata walichokuelekeza hadi mwisho na hawakuondoi.Na linakuwa zoezi la kukukata salio kila mara.Huu ni uhuni wenye mchanganyiko wa wiz

Wakikata TSH 200 kwa watu milioni 2 wanapata 400 milioni ya dhulma
 
Nakubaliana na wewe kuhusu huduma kwa wateja yao, mimi nilijitowa airtel zamani sana, nikajitowa na voda, wote hao kwa ajili ya customer service zao.

Tigo customer care wako vizuri sana, naona ndiyo bora zaidi, zamani ndiyo walikuwa wabovu zaidi. Sasa Tigo wanaongoza kwa huduma kwa wateja. No doubt.
Nitajaribu
 
Jina langu Ni la Kimasai. Nilipiga simu customer service Airtel akapokea maza Mwenye lafudhi ya kichaga, nikaeleza shida yangu. Akaniambia nitaje namba ya simu, nikamuambia sijaishika maana lain bado mpya. Nikamuuliza wewe si unaona hapo lakini...
Mamlaka yenye dhamana na mawasiliano imetutelekeza, Haya makampuni yanafanya kama yanavyotaka.
 
Tatizo ni kwamba wafanyakazi wengi wa call centre kwenye haya makampuni ya simu wana sifa zifuatazo:

1. Mshahara na maslahi duni, hii hupelekea kukosa motisha.

2. Waliofeli ngazi za elimu hivyo wamekata tamaa ya maisha, sijataja hii kwa nia mbaya bali effect ya watu wa namna hii imeonekana kwa polisi, watu wa huduma za afya, makarani, walimu n.k
 
Nakubaliana na wewe kuhusu huduma kwa wateja yao, mimi nilijitowa airtel zamani sana, nikajitowa na voda, wote hao kwa ajili ya customer service zao.

Tigo customer care wako vizuri sana, naona ndiyo bora zaidi, zamani ndiyo walikuwa wabovu zaidi. Sasa Tigo wanaongoza kwa huduma kwa wateja. No doubt.
Kumbe na wewe unapenda mtandao pendwa wa 0713 😂🤣
 
Back
Top Bottom