Airtel na KWANJUKA tunaibiwa

Uswe

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,204
626
Mpendwa mteja
Namba yako XXXXXXX imechaguliwa kushindania Tsh1,000,000 za leo.
Tuma 'KWANJUKA' kwenda 15656 SASA!
Time: XXXXXX XXXX

Airtel wamenitumia hiyo message, hii ni mara ya tatu napata hiyo message, kuna mtu keshawahi kushirikki akapata hiyo 1M?
 
Mkuu, Jaribu kutafuta andiko kama lako, lipo hapa jamvini na wadau wamechangia huko. Itakusaidia kupata maoni na mtazamo wa wana wJF kuhusu hilo.
 
Mkuu, Jaribu kutafuta andiko kama lako, lipo hapa jamvini na wadau wamechangia huko. Itakusaidia kupata maoni na mtazamo wa wana wJF kuhusu hilo.
asante ngoja niltafuta, ila ungeniangushia link, ningeshukuru sana, ila good advice wacha nisearch
 
Jamani jamani makampuni ya mawasiliano yatatumaliza na vipromotion vyao kumbe upatu. Ukifuatilia mchakato mzima unaotumika kumpata mshindi ni wizi mtupu kwa kivuli cha bahati nasibu.

Unaambiwa sms moja unakatwa sh 520.

Wakati umefika sasa makampuni ya mawasiliano wajifunze kutoka kwa makampuni ya vinywaji wao bahati nasibu zao ziko fair kabisa.

Wekeni zawadi zenu kuanzia kiwango cha chini hadi hayo mamilioni kwenye vocha mtu akiingiza vocha akikutana na milioni zake poa lakini sii huu wizi wa kutuma sms kwa mf, mimi nimetuma sms 500 nina pointi labda laki 2 wewe leo unatuma sms moja tu unapata hayo mamilioni kama wanajua inakuwa hivyo wasiwe wanatutumia hivyo visms vya hamasa kwani wateja wote nchi nzima kila mmoja akituma sms1 tu mshindi atapatikana ni mtazamo wangu tu
 
yaani wamezidi. Hata Voda, usumbufu na vijisms kila mara. Kama ni bahati nasibu watangaze kwingine siyo kutusumbua na simu zetu. Huduma isiwe kero!s
 
Airtel ni wezi, wamenitumia sms ikisema

"Shinda point 100! Chris Tucker katembelea Tanzania mwaka gani?
1=2008
2=2009
Tuma 1 au 2 kwenda 15656"

Nami kwa kujiamini kabisa nikatuma jibu "1" kwa maana alikuja kwenye mkutano wa Leon H. Sullivan VIII uliofanyika 2-6/June/2008. Baadaye nikapata sms;

"Wrong answer, but don't worry, more questions are comming and they are giving SUPER points! Continue answering for the 1 mil. TSH! You have 330pts!"

kilichonishangaza zaidi hii kuwa nimekosa jibu! HAWA AIRTEL NI WEZI kwani wameni KWANJUA Tshs 520!
Nakumbuka huyu jamaa ni comedian siku ile kwenye mkutano alipopewa nafasi aliongea kama ana rap, maneno mareefu kama reli!

Kama tumetuma watu 500,000 x 520 = 260,000,000/= zimepatikana for free!
 
You are reaping the fruits for not examining their degree of frankness!
 
Kwani umeambiwa wahindi wamekuja kucheza kiduku si umehamia mwenyewe!! Banjuka
 
Airtel ni wezi, wamenitumia sms ikisema

"Shinda point 100! Chris Tucker katembelea Tanzania mwaka gani?
1=2008
2=2009
Tuma 1 au 2 kwenda 15656"

Nami kwa kujiamini kabisa nikatuma jibu "1" kwa maana alikuja kwenye mkutano wa Leon H. Sullivan VIII uliofanyika 2-6/June/2008. Baadaye nikapata sms;

"Wrong answer, but don't worry, more questions are comming and they are giving SUPER points! Continue answering for the 1 mil. TSH! You have 330pts!"

kilichonishangaza zaidi hii kuwa nimekosa jibu! HAWA AIRTEL NI WEZI kwani wameni KWANJUA Tshs 520!
Nakumbuka huyu jamaa ni comedian siku ile kwenye mkutano alipopewa nafasi aliongea kama ana rap, maneno mareefu kama reli!

Kama tumetuma watu 500,000 x 520 = 260,000,000/= zimepatikana for free!

Usishangae, wanawekeza kwenye uroho wetu wa kupenda vitu chap chap. Kwa wenye upeo hawezi hata kukuelewa unalalamika nini maana hizo msg huwa zinakuwa crap na kufutwa mara moja.
Acheni njia za bahati nasibu kupata mali, fanya kazi.
 
Back
Top Bottom