Air Tanzania ingeshusha viwango vya nauli, tungesafirisha Watanzania wengi ndani na nje ya nchi

Dar-Dodoma nilipe sijui 325,000 wallah nitakufa. Shabiby na Kibinyiko zile za Alfajili ni Tshs 20,000/= halafu unapita Pwani Kibaha, Morogoro kisha Dodoma. Upo angani unapita wapi. Sikataki kupanda mwewe ila kwa route za humu ndani hapa kbs biashara ya kupunguziana K-Vant na mbuzi choma. Pandeni tu. Wengine tutakufa na IT na Mafusso kwa route za ndani. Ama magari ya Magazeti yale ya Posta.

Wangekua na bei rafiki Amini route za ndani wangeuza sana lakini bei zao ndio shimo lao na hapo sijui hua wanafikiria nini kupanga hizo gharama?
 
Nimeshuhidia mara zaidi ya 4 ndege inatua uwanja wa Dodoma ikiwana abiria wasiozidi 4, kuna siku ilitua na abiria wanne
Bro kuna siku nilikuwa nafanya booking ya ndege Go and Return Dar to Dom, gharama yake ilikuwa ni milioni moja na laki 2. Ndege ilikuwa kwenda inapita Kigoma na kurudi pia inapitia Kigoma so jamaa wakachaji nauli ya Dar - Kigoma - Dom - Kigoma - Dar, hiyo ilikuwa ni nauli ya mtu mmoja tuu na safari yetu tulikuwa watatu, ikabidi tupande ndege ya ardhini V8 ambayo kwenda na kurudi ni lita 220 tuu na tunauwezo wa kutembea dar to dom kwa masaa matano. Serikali inabidi iangalie bei za ATCL siyo rafiki kabisa kwa watanzania wa uchumi wa kati
 
Bro kuna siku nilikuwa nafanya booking ya ndege Go and Return Dar to Dom, gharama yake ilikuwa ni milioni moja na laki 2. Ndege ilikuwa kwenda inapita Kigoma na kurudi pia inapitia Kigoma so jamaa wakachaji nauli ya Dar - Kigoma - Dom - Kigoma - Dar, hiyo ilikuwa ni nauli ya mtu mmoja tuu na safari yetu tulikuwa watatu, ikabidi tupande ndege ya ardhini V8 ambayo kwenda na kurudi ni lita 220 tuu na tunauwezo wa kutembea dar to dom kwa masaa matano. Serikali inabidi iangalie bei za ATCL siyo rafiki kabisa kwa watanzania wa uchumi wa kati
Mwaka upi komanyahenry ⁉️
 
Ambaye hawezi kulipa nauli apande bodaboda
Wewe usidhani wote wana uwezo kama wako.....Air Tanzania ni shirika la hovyo kabisa kuwahi kutokea, na ndio maana most of them wanaamua kupanda BUS, tiketi very cheap ukilinganisha na hilo lindege lao.

Mwanza to dar

Wakati wa fastjet ilikuwa ni neema kubwa kwa watanzania...but now 😡.....Mwanza to dar 300,000 na ushee....while BUS sio chini ya 65,000....huoni kuwa a very big difference?
 
Ni upumbavu tu...nauli ya bus 45,000 mpaka 60,000 to dar alafu umshawishi apande air Tanzania nauli 300,000 na usheee!!! Tena ni One way!!!!!
 
ATC si kwa ajili ya wanyonge thus kwao ni heri waondoke na siti tupu.Kumbe wangezipigia promo kwa bei ya chini zingejaa
 
mwaka 2014 , nilisafiri paris -dar nakirudi paris kwa 400 USD kwa kipindi kile ilikuwa sawa kama na laki 8 hivi, ila mwaka ule ule Dar Bukoba kwa ndege Air Tanzania kwenda tu Bukoba ilikuwa laki 5 na nusu
 
Ndugu yangu amesikitika sana hata sasa, kwamba bado kuna matukio ya wizi wa vitu vya abiria katika mabegi yao baada ya upekuzi kiwanja cha ndege Dar es Salaam maarufu JNIA ! Kama kwa watanzania wanaibiwa hivi pamoja na kamera zote inakuwaje kwa watalii wanaibiwa ⁉️

Ndugu yangu alitoka Dar -Dodoma kwa ndege ya shirika la ATCL. Pia turejea tukio kama hili kupitia >>> Wizi huu uwanja wa ndege aibu
 
Nashindwa elewa kwanini wasifate mfumo wa budjet airlines kama fastjet, ryan etc

Sent from my TECNO W2 using JamiiForums mobile app
Tatzo ni unapofanya biashara ua uber kwa kutumia V8...hzo ndege ni za hali ya juu sana..luxury....wangenunua za kawaida...hzo ndege hata wazungu wenyew wanazishangaa.ni toleo latest kabisa..sasa kwa biashara ya kwenda arusha or moro or mwanza ni matumiz mabaya ya hzo ndege..hzo ndege zaitaj safar safar kweli.
 
Mkuu uko sahihi. Wajifunze kwa shirika letu la Tanesco, kabla ya kuja na mpango wa makusudi wa kuongeza idadi ya wateja umeme ulikuwa ni anasa lakini baada ya kupanua wigo wa wateja wao ambapo sasa almost 80 percent of the households wana access ya umeme tumeona bei zikishuka na kuwa affordable kwa wengi. Atcl igeni hiyo itawasadia maana wengi tunatamani tupande ndege zenu kikwazo ni gharama.
80% ya kaya wana access ya umeme Tanzania? sikujua hilo hakika au ni uko Dar peke yake
 
Bodaboda kwa maana ya usafiri wa Pikipiki? Kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine, mfano Dar - Katavi?

Hauwezi kuwa unamaanisha mkuu.
Sasa kama aliwahi kuwaambia watu wa kigamboni wapige mbizi,anashindwaje kuwaambia waTZ hivyo?
Serikali haijawahi kuwa na huruma wala kuwapenda wanyonge,
Ndio mana ikazifutilia mbali kampuni za kizalendo na kuingia kukamua raia yenyewe
 
Back
Top Bottom