Aina za majini na kazi zake

Aina za majini na kazi zake

Hakuna ukweli YESU alimtoa PEPO jamaa 1 akayaamuru yaingie kwa Nguruwe elf 2 wakafia Baharini....sasa kama elf 2 walikufa sababu ya kuingiwa na mapepo nivipi wewe unaekula kilo1
Kumbe hao wa zamani walishakufa wa sasa awana noma ngoja tuendelee kufukuza majini hapa kwa Nathaniel banana anajua kutoa kitu safi kabisa
 
Pia nilipata habari kuwa ukiwa mfugaji wa hiyo kitu majini hayakusogelei, mkuu Mshana Jr maelezo kidogo tafadhali! Asante
Acheni hizi Stori za kwenye Kahawa....hakuna kitu kama hicho.. unazungumzia mambo ya Ulimwengu wa Roho wa NURU na tambua Ulimwengu wa Roho Aidha wa NURU au GIZA unanguvu kuliko huu wa Mwili tunaoishi sisi
 
Mshanajr kuna watu wanasema ukipiga[emoji241] hii kitu majini ayakufati kuna Ukweli hapo?????

Pia nilipata habari kuwa ukiwa mfugaji wa hiyo kitu majini hayakusogelei, mkuu Mshana Jr maelezo kidogo tafadhali! Asante
Huyu mdudu na yale madude ni kama paka na panya ndo maana hata katika mambo ya kishirikina material ya Noah hutumika kama kinga
 
Hakuna haja tena ya kutoa tafsiri ya majini kwakuwa tayari tumeshalidajili hili kwenye post iliyopita kwamba majini ni viumbe roho waliofukuzwa toka mbinguni na kutupwa ulimwengu wa giza.

Mada hii ni maalum kwa ajili ya kutambua aina za majini na kazi zake
Kuna wakati katika jamii unaweza kumshangaa mtu au hata kugombana naye kutokana na tabia zake na mambo yake huyu si wa kulaumu sana saa nyingine si yeye bali ni jini, hata hapa JF tunao wengi tuu.

Kimsimgi wapo majini tofauti tofauti zaidi ya 60 lakini kazi zao kwa sehemu kubwa zinaingiliana hivyo nitaweka baadhi tu ambayo kwa kiasi kikubwa ndio hubeba mambo mengi fuatana nami.

1. SUBIANI - hili ni jini linalosababisha ajali na lenye kuzuia hedhi kwa mwanamke, lina penda sana damu hasa hiyo ya hedhi.

View attachment 342303

2.MURAFARI- hili ni jini la kuzuia mafanikio ya kimaisha kielimu na hata kipato, ukitupiwa hili jini utahangaika sana na maisha.

3.LATIFU- jini la mateso ufukara na matumizi ya hovyo unakuwa ni mtumwa wa kupata kupoteza na kutumia bila tija.

4.JAHARI-jini jizi la biashara, unafanya Sana biashara lakini huoni ustawi wala mafanikio yoyote.

View attachment 342305

5.HASINANI- Jini la fujo ulevi wa kila aina bhangi sigara madawa pombe nk

6.JUBE- Jini la utasa, hili unaweza kutupiwa tu na mbaya wako au ukiwa mtoa mimba au mpiga puchu mahiri.

7.RUYATI- ndoto mbaya, ukiacha ndoto maono au ndoto ujumbe , hizi ndoto za kutisha husababishwa na jini ruyati.

8.TAJARUNI-hili ni la utajiri wa masharti ya kutoa kafara la ndugu na kufanya ngono na mzazi au mwanao.

9. WAIDADAT- jini linalomfanya mwanaume aige mambo yote ya kike kuanzia tabia mpaka mavazi.

View attachment 342307

10. ALIBADIRI- Ukitupiwa hili kwa sababu yoyote ile hasa kutenda uovu huponi.

11.ANZURA -kuzuia ndoa hasa kwa wanawake, utakuta binti mzuri kakamilika kila idara lakini anaishia kuposwa tuu.

12.MAIMUNA- jini mfarakano wa kuleta magomvi kwenye ndoa hatimaye kuvunjika.

13 . MAKATA- Jini makata ni noma hili likiingia kwenye familia au ukoo basi vifo vitafululiza mpaka mbaki wachache kabisa.

View attachment 342306

14.TARIK- jini hili hufarakanisha marafiki watu wanaofanya biashara pamoja kwenye vyama nk nk..likishaingia mahali hili lazima kinuke.

15. JINI WIVU KIJICHO NA ROHO YA KWANINI-hili bwana hili popote litakapoona new post ni mtu fulani sikilizia mashambulizi yatakayofuata.

[emoji15] [emoji15] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Katika mambo yote hayo hakuna jini lolote linalofaidika na chochote bali kumletea shida mwanadamu ili afarakane na mola wake
Kumbuka kuna majini ya kutupiwa kutumwa na yale yanayofanya kazi yenyewe kwa utashi wao.

==========================
NB: Picha zimewekwa ili kuleta uhalisia zaidi ingwa zinaweza zilihusiane moja kwa moja na Majina ya viumbe hawa.
Naona unatrotia cheo cha shekh yahya
 
Ni mule mule kwakuwa ile nguvu ya kisomo hutokana na majini
Nb; kuna kisomo cha albadili/albadiri na kuna jini la albadiri ambalo hilo huua moja kwa moja lakini kisomo cha albadiri si lazima ufe unaweza kuchanganyikiwa na kuwa chizi au kichaa
kwa blahblah tu hujambo,albadiri ndiyo nini?..sema ahlul badr,majina ya maswahaba wa mtume waliokufa vita vya badr,leo imekua aina ya jini!!?
 
AL BADIRI NI JINI? Mbona kuna kisomo kinaitwa Al badiri husomewa wezi wanaoiba au hata kama mmezuishana mambo makubwa inasomwa hiyo albadiri na aliemuongo ndio inamshika na kumdhuru aidha kwa kufa au kuwa kichaa...hebu nifafanulie.
AHL-BADRI;

sio JINI.... ni kisomo cha kumpa mashitaka/malalamiko Mwenyezi Mungu kwa mujibu wa Imani ya Kiislamu!!

neno "Ahl-Badri" maana yake ni watu wa Badri au watu waliopigana VITA YA BADRI katika historia Uislamu!!

Hiki kisomo kama ukisikia kinasomwa au kama ukikiona kitabu chake basi hua kinataja MAJINA YA WATU WOTE WALIOSHIRIKI VITA YA BADRI!!

mtu anaposema Alibadir basi ana maanisha ni kisomo tu na sizani kama kina mahusiano na majini!! ni kama maombi ya mtu aliyedhulumiwa... kama wewe unayesoma iki kisomo kumkusudia mtu ambaye hana hatia huwa inakudhuru wewe mwenyewe...

Ingekua Alibadiri ni jini basi nahisi wengi tungekufa au kuwa vichaa... maana ingekua ni kama aina flani ya ushirikina tuliouzoea mtu anakudhuru kwa husda zake tu!!

kama nimekosea au nimewakwaza watu basi naomba mnisamehe!!

#Peace
 
kwa blahblah tu hujambo,albadiri ndiyo nini?..sema ahlul badr,majina ya maswahaba wa mtume waliokufa vita vya badr,leo imekua aina ya jini!!?
Ni hili tu au una lingine? Kumbuka gari ni moja lakini make ziko elfu nyingi....usinichagize hapa katafute ukweli uongeze maarifa
 
AHL-BADRI;

sio JINI.... ni kisomo cha kumpa mashitaka/malalamiko Mwenyezi Mungu kwa mujibu wa Imani ya Kiislamu!!

neno "Ahl-Badri" maana yake ni watu wa Badri au watu waliopigana VITA YA BADRI katika historia Uislamu!!

Hiki kisomo kama ukisikia kinasomwa au kama ukikiona kitabu chake basi hua kinataja MAJINA YA WATU WOTE WALIOSHIRIKI VITA YA BADRI!!

mtu anaposema Alibadir basi ana maanisha ni kisomo tu na sizani kama kina mahusiano na majini!! ni kama maombi ya mtu aliyedhulumiwa... kama wewe unayesoma iki kisomo kumkusudia mtu ambaye hana hatia huwa inakudhuru wewe mwenyewe...

Ingekua Alibadiri ni jini basi nahisi wengi tungekufa au kuwa vichaa... maana ingekua ni kama aina flani ya ushirikina tuliouzoea mtu anakudhuru kwa husda zake tu!!

kama nimekosea au nimewakwaza watu basi naomba mnisamehe!!

#Peace
Amanito kuna mahali nimefafanua kuhusu hilo na pia angalia nilichoandika kuhusu jini albadiri (naandika kiswahili )kwamba ni jini la kifo....tofauti na albadiri kisomo kama ulivyo fafanua hapo....
 
Hivi hakuna majini ambayo yana majina ya Kikristu?
Samahani lakini..!!
Mkuu majina ya Watu hayahusiani ni Imani yeyeto.Majina ni ya Mashariki ya kati Na Ulaya.
Historia ya uchawi Na majinni imeandikwa katika nchi za mashariki ya kati Na Lugha zinazo tumika ni Kiarabu,kiajemi (kifarsi)Na kihibru(kiyahudi). Hayo majina ya majinni ya yameitwa kutokana Na lugha zao. Ukiandika kitabu kuhusu maajabu ya Rufiji majina ya Kindengereko yatakuwemo.
 
lingine lipi?!!
hujui kitu wewe,danganya poyoyo wenzio
Haya maneno ni ya kawaida sana kwangu kuyasikia, kwa umri wangu na wako tumepishana mbali sana bado unahitaji kukua na kujifunza mengi zaidi...
Kwa miaka yako 28 huwezi ukawa unajua mengi bado ya kawaida hata ya kiroho pia
Kumuita mtu popoyo ni rahisi zaidi kuliko kuthibitisha, kwahiyo siwezi kuhemka katika hili kwakuwa najua kuwa hujui na ninachokijua kichakuchukua miaka mingi kuweza kukijua
 
jini albadir ndiyo kakwambia nina miaka 28!?..kakudanganya,pia umri sio kujua,unaweza ukaisha miaka alfu lakin ukafa kichwan hakuna cha maana afadhal ya tikiti maji
 
AHL-BADRI;

sio JINI.... ni kisomo cha kumpa mashitaka/malalamiko Mwenyezi Mungu kwa mujibu wa Imani ya Kiislamu!!

neno "Ahl-Badri" maana yake ni watu wa Badri au watu waliopigana VITA YA BADRI katika historia Uislamu!!

Hiki kisomo kama ukisikia kinasomwa au kama ukikiona kitabu chake basi hua kinataja MAJINA YA WATU WOTE WALIOSHIRIKI VITA YA BADRI!!

mtu anaposema Alibadir basi ana maanisha ni kisomo tu na sizani kama kina mahusiano na majini!! ni kama maombi ya mtu aliyedhulumiwa... kama wewe unayesoma iki kisomo kumkusudia mtu ambaye hana hatia huwa inakudhuru wewe mwenyewe...

Ingekua Alibadiri ni jini basi nahisi wengi tungekufa au kuwa vichaa... maana ingekua ni kama aina flani ya ushirikina tuliouzoea mtu anakudhuru kwa husda zake tu!!

kama nimekosea au nimewakwaza watu basi naomba mnisamehe!!

#Peace
HIVI MIMI NDIVYO NINAVYOELEWA PIA, Ukiangalia sentence yangu ina alama ya kuuliza? nilikuwa namuuliza kaka Mshana AL BADIRI Pia ni jinni????? ILA ASANTE KWA UFAFANUZI NA KWA FAIDA YA WENGINE.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom