Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,716
- 729,889
Hakuna haja tena ya kutoa tafsiri ya majini kwakuwa tayari tumeshalidajili hili kwenye post iliyopita kwamba majini ni viumbe roho waliofukuzwa toka mbinguni na kutupwa ulimwengu wa giza.
Mada hii ni maalum kwa ajili ya kutambua aina za majini na kazi zake
Kuna wakati katika jamii unaweza kumshangaa mtu au hata kugombana naye kutokana na tabia zake na mambo yake huyu si wa kulaumu sana saa nyingine si yeye bali ni jini, hata hapa JF tunao wengi tuu.
Kimsimgi wapo majini tofauti tofauti zaidi ya 60 lakini kazi zao kwa sehemu kubwa zinaingiliana hivyo nitaweka baadhi tu ambayo kwa kiasi kikubwa ndio hubeba mambo mengi fuatana nami.
1. SUBIANI - hili ni jini linalosababisha ajali na lenye kuzuia hedhi kwa mwanamke, lina penda sana damu hasa hiyo ya hedhi.
2.MURAFARI- hili ni jini la kuzuia mafanikio ya kimaisha kielimu na hata kipato, ukitupiwa hili jini utahangaika sana na maisha.
3.LATIFU- jini la mateso ufukara na matumizi ya hovyo unakuwa ni mtumwa wa kupata kupoteza na kutumia bila tija.
4.JAHARI-jini jizi la biashara, unafanya Sana biashara lakini huoni ustawi wala mafanikio yoyote.
5.HASINANI- Jini la fujo ulevi wa kila aina bhangi sigara madawa pombe nk
6.JUBE- Jini la utasa, hili unaweza kutupiwa tu na mbaya wako au ukiwa mtoa mimba au mpiga puchu mahiri.
7.RUYATI- ndoto mbaya, ukiacha ndoto maono au ndoto ujumbe , hizi ndoto za kutisha husababishwa na jini ruyati.
8.TAJARUNI-hili ni la utajiri wa masharti ya kutoa kafara la ndugu na kufanya ngono na mzazi au mwanao.
9. WAIDADAT- jini linalomfanya mwanaume aige mambo yote ya kike kuanzia tabia mpaka mavazi.
10. ALIBADIRI- Ukitupiwa hili kwa sababu yoyote ile hasa kutenda uovu huponi.
11.ANZURA -kuzuia ndoa hasa kwa wanawake, utakuta binti mzuri kakamilika kila idara lakini anaishia kuposwa tuu.
12.MAIMUNA- jini mfarakano wa kuleta magomvi kwenye ndoa hatimaye kuvunjika.
13 . MAKATA- Jini makata ni noma hili likiingia kwenye familia au ukoo basi vifo vitafululiza mpaka mbaki wachache kabisa.
14.TARIK- jini hili hufarakanisha marafiki watu wanaofanya biashara pamoja kwenye vyama nk nk..likishaingia mahali hili lazima kinuke.
15. JINI WIVU KIJICHO NA ROHO YA KWANINI-hili bwana hili popote litakapoona new post ni mtu fulani sikilizia mashambulizi yatakayofuata.
Katika mambo yote hayo hakuna jini lolote linalofaidika na chochote bali kumletea shida mwanadamu ili afarakane na mola wake
Kumbuka kuna majini ya kutupiwa kutumwa na yale yanayofanya kazi yenyewe kwa utashi wao.
==========================
NB: Picha zimewekwa ili kuleta uhalisia zaidi ingwa zinaweza zilihusiane moja kwa moja na Majina ya viumbe hawa.