Aina 8 za wapangaji katika nyumba za kupanga

Aina 8 za wapangaji katika nyumba za kupanga

2) Walio na matatizo na kila mtu
emoji35.png
emoji34.png

Hawa muda wote hua na hasira hasira, kisirani, wame nuna-nuna bila sababu kuanzia asubuhi mpaka usiku. Hawapokeai wala kutoa salamu. Hua wanasubiri mtu ajikoroge tu aisome. Usiingie tisini zao, wapotezee uishi kwa amani.

hii nimeiona sana: mtu hamjagombana lakini arudi home wala hakusalimii mpaka umuanze; na hata ukimuanza anaitikia kama hataki
 
Ila kuna wengine haipiti week moja bila kutia timu mlangoni kwako kupiga mizinga ya hela, mpaka unajikuta unamdai hela ya kodi ya miaka miwili au mitatu. Wana maneno mazuri ya kupigia mizinga halafu utamsikia "ondoa shaka, we ondoa shaka kijana, tutakatana kwenye kodi tu,tuko pamoja"

hii ya mizinga imenikuta sana nyumba nilioanzia
 
Inapofikia muda unahitaji kuanza maisha ya kujitegemea, na unahitaji sehemu/chumba chenye unafuu kwenye suala zima la gharama/kodi, kimbembe hua kwenye utafutaji wa sehemu hio. Hasa pale ukizingatia sehemu unazozipata haziji na taarifa au huduma muhimu.

Hongera kama unasehemu ya kujitegemea kuishi, na hawa ndio aina ya wapangaji ambao tegemea kukutana nao kama unahamia kwenye nyumba ya kupanga.

1) Mashujaa wa kufanya ibada wasiotoa nafasi ya kulala..
Hawa watu, mmh. Shukuru kama hawatakua chumba cha jirani kwako, au lasivyo kulala itakua mtihani kwako. Wanaweza kusali, kuimba na kulia kuanzia asubuhi mpaka asubuhi nyingine bila kituo cha mapumziko, kizaazaa ukijifanya kulalamika tu, kichambo utakachopata sio cha nchi hii. [emoji22] [emoji25]

2) Walio na matatizo na kila mtu[emoji35] [emoji34]
Hawa muda wote hua na hasira hasira, kisirani, wame nuna-nuna bila sababu kuanzia asubuhi mpaka usiku. Hawapokeai wala kutoa salamu. Hua wanasubiri mtu ajikoroge tu aisome. Usiingie tisini zao, wapotezee uishi kwa amani.

3) Wanao kopa/kuazima kila kitu[emoji30] [emoji31]
Hutaki kukutana na hawa jamaa. Kukopa/Kuazima ni kama ibada kwao. Hukopa au kuazima kila kitu, kuanzia vyombo vya ndani, hela, mpaka viungo vya chakula. Halafu cha kukera sasa hua hawana cha kukuazima wewe.

4) Wanao ishi kama vivuli[emoji19] [emoji52]
Hujui kama yupo au hayupo, kwasabu muda wote mlango wao umefungwa. Utakutana nao pale baba/mama mwenye nyumba akiitisha kikao cha wapangaji tu.

5) Wanaopata wageni kila kukicha[emoji126] [emoji125]
Muda mwingine unaweza ukajiuliza kama unaishi kwenye nyumba ya kupanga au gesti. Hawa wapangaji hupata wageni kila kukicha, akitoka huyu kaingia mwingine. Ila hayakuhusu.

6) Wazee wa mziki mnene/pasua vichwa[emoji449] [emoji351] [emoji445]
Asubuhi mpaka jioni unalia mziki mkubwa kama mpo club, sauti full, utahisi speaker za redio zimewekwa chumbani kwako vile. Akiamka vibaya jamaa mnaweza kusikilizishwa mwimbo mmoja kuanzia asubuhi mpaka usiku mpaka mkazijua verse na chorus zote.

7) Wanandoa wanaogombana kila kukicha[emoji144] [emoji143]
(Acha nisitolee ufafanuzi hili, nisije kuwekwa kwenye kikaango humu[emoji124] [emoji124] [emoji124] ).

8) Wajuaji wa kila kitu, hata wasivojua[emoji15]
Hawa hupenda kuongea kuhusu kila kitu, topic ikianza tu lazima anacho cha kuongelea hata kama hawana ufahamu nayo. Jaribu kujiepusha nao hasa wakianza maswala ya siasa, mtakesha.

9) Shushushu/Kiherehere wa baba mwenye nyumba[emoji18]
Kama utashangaa jinsi gani baba mwenye nyumba hupata taarifa juu ya chochote kinachotokea ndani ya nyumba, hata kama hakuepo au haishi humo, tambua kuna huyo funza anaepeleka taarifa kwa maslahi ya kupata favor za mshua.

10) Baba/Mama mwenye nyumba[emoji123]
Sio lazima aishi hapo, wengine huishi sehemu nyingine. Kuna wengine wasela, utawaona mwisho wa mwezi mpaka mwisho wa mwezi. Ila kuna wengine haipiti week moja bila kutia timu mlangoni kwako kupiga mizinga ya hela, mpaka unajikuta unamdai hela ya kodi ya miaka miwili au mitatu. Wana maneno mazuri ya kupigia mizinga halafu utamsikia "ondoa shaka, we ondoa shaka kijana, tutakatana kwenye kodi tu,tuko pamoja".


kuna wengine anataka ajue kila kilicho chako na issue zako ; then anaenda kukuanika kwa majirani umbea umbea tu!
 
Hahaha ndo ukubwa huo mkuu, tunaruka viunzi vingi mtaani aisee, kama tupo vitani

Mi ninapoishi kwa sasa ; kuna mama mmoja mme wake bodaboda ; kadri siku zinavyoenda anajitahidi kuelezea mambo yake na ya mmewe (ukweli na uwongo) kwa mke wangu ili mke wangu amwambie issue zake na zangu: lakini kila akijitahid anagonga Mwamba. Alifikia hatua ya kumuuliza mke wangu vitu alivyozawadiwa kwenye kitchen party kwa malengo ya kujua mimi nimenunua nini pale kwa vitu tunavyomiliki. Akaishiwa kudanganywa tu. Aisee ni shida
 
Mi ninapoishi kwa sasa ; kuna mama mmoja mme wake bodaboda ; kadri siku zinavyoenda anajitahidi kuelezea mambo yake na ya mmewe (ukweli na uwongo) kwa mke wangu ili mke wangu amwambie issue zake na zangu: lakini kila akijitahid anagonga Mwamba. Alifikia hatua ya kumuuliza mke wangu vitu alivyozawadiwa kwenye kitchen party kwa malengo ya kujua mimi nimenunua nini pale kwa vitu tunavyomiliki. Akaishiwa kudanganywa tu. Aisee ni shida
Ah hatari hio sasa mkuu, hilo ni jipu aisee. Wakum kwepa kama gonjwa la zinaa huyo mama
 
Mtoto Wa mwenye nyumba 4yrs,alikua mtundu balaaaa!!bhas Mzee baba nimejipinda nikajaza maji pipa akaja akatia sabuni!!daaah nilimvizia nikamkamata nikampa Yale makonzi ya kusugua kichwa na Bonge LA banzi mgongoni!!mamake kuja juu wapangaji wote wakamcharukia wakamwambia mwanao kazidi tumemchoka na wewe unamdekeza!!itabid awe mpole, na yule Mtoto alikua akijua nipo anakua km piritoni!!
ndugu ulifanya kama wale walimu wa bukoba.
 
Namba 4 ndo Mimi huyo.Kama leo kuna mpangaji mgeni kaamua kunigongea nikaitika kanisalimu nikaitika nikiwa ndani.Hajaniona wala,so hanijui.
yaani na usije ukatoka mkuu,mimi ilinicost.Huyo dada ni type no 3 mbaya zaidi haheshimu privacy ya mtu unaeza ukasikia hodii saa sita usiku af ukitoka utumbo anaokueleza utatamani umchape vibao. Nilimtolea uvivu siku moja hadi leo hanisemeshi nadhani hana hamu na mimi [emoji38][emoji38]
 
Dah nyumba hizi hatari mi nilipanga kwenye nyumba moja,mama Mwenye nyumba alikuwa anaishi hapo,hataki umzidi kwa chochote,cyo kuvaa,kula, yaan maish kwa ujumla,atataka kujua kila cku unapik nn,km ni zaid yk anabadilisha ili tu usimzidi,siku ukimzidi tu ni mvimbo mwanzo Mwisho,na alivyo Bonge sasa dah kwa kweli yataka Moyo hasa ukiwa na watoto
 
Back
Top Bottom