AIG ni miongoni mwa kampuni 50 bora duniani 2016

Jun 8, 2016
11
0
Jarida liitwalo MIT Technology Review iliyojikita na uchambuzi ya masuala ya elimu ya kiteknolojia imeorodhesha listi ya makampuni bora 50 yanayofanya vizuri duniani kwa mwaka 2016. Uchambuzi huu umezingatia fursa zinazojitokeza katika makampuni haya ambayo yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutoa fursa za kimaendeleo kama vile ajira, biashara na ukuaji wa sekta ya mawasiliano ya kiintaneti.

Moja ya kampuni hizi ambayo imeshikilia nafasi ya 47 ni AFRICA INTERNET GROUP (AIG) ambayo imejikita katika mapinduzi na maendeleo ya biashara za kielektroniki (e-commerce) barani Afrika kwa kipindi cha miaka 4 hadi sasa. AIG ni kampuni ya kwanza kuanzishwa barani Afrika katika sekta ya e-commerce ambayo ina thamani ya dola za kimarekani zaidi ya billion 1 iliyosambaa katika nchi 26 Afrika hadi sasa.

AIG inadhaminiwa na kampuni kubwa kama vile: Axa, Goldman Sachs, MTN na Orange. AIG inatazamiwa kuwa ndio mlango wa maendeleo ya kiuchumi barani Afrika kupitia njia za maendeleo ya kimtandao.
 
mnh intel wa 49 na kama Apple hayumo. kama hao amazon innovation zao nyingi zinafeli sokoni angalia vitu kama amazon fire smartphone,

kumetumika vigezo gani?
 
AIG wana matatizo right now, kwanza AIG haipo tena wamebadili kila kitu kinaitwa Jumia now. Wameunga makumpuni yote sasa ni Jumia (Kaymu,HelloFood,Vendito na kampuni kama 5 zengine) yamekuwa Jumia, hii ni katika kujaribu kupunguza gharama za uendeshaji nadhani.

Jumia (Africa) imeingiza hasara ya $18 hadi mwezi wa tatu mwaka huu. Wamepunguza budget ya matangazo ambayo imepelekea mauzo kushuka sana.

Kampuni mama Rocket Internet hisa zinaporomoka ni kama 1/3 ya thamani yake ya 2014, jumla kampuni zake zimepata hasara ya zaidi ya $1 Billion 2015.

FSvxshC.jpg
 
Back
Top Bottom