Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,447
- 7,822
Mbunge wa Nkasi Kaskazini kupitia CHADEMA, Aidan Khenan leo alikuwa wa kwanza kuomba kuuliza swali baada ya Dkt. Tulia Ackson kuomba kura kuwania nafasi ya wabunge kuchagua kuwa naibu spika.
Nalo swali lake lilikuwa kama ifuatavyo
========
Aida Khenan: Mheshimiwa spika nakushukuru, napenda kuuliza swali moja kwa dada yangu Tulia Akson, mbunge wa Mbeya Mjini. Mheshimiwa Spika sina mashaka na uzoefu wa mgombea kwenye nafasi anayoiomba. Natambua kwamba nafasi hiyo ndiyo aliyokuwa nayo kwenye bunge lililopita
Mheshimiwa mgombea miongoni mwa changamoto zilizokuwepo bunge lililopita ni pamoja na changamoto ya muda kwa wabunge kuchangia ndani ya bunge jambo ambalo kwa wananchi pia ilikuwa ni changamoto kidogo, ningependa kujua, umejipangaje juu ya kuweza kuwapa nafasi au muda wa kutosha wabunge ili waweze kuwakilisha mawazo ya wananchi waliowaamini bila kuathiri kanuni?
Spika Ndugai: Bado natafakari, hili swali sio swali! Mheshimiwa Dkt. Tulia Akson majibu tafadhali.
Tulia Ackson: Mheshimiwa spika, mimi kama msaidizi wako mkuu ni wajibu wangu kukushauri katika yale mambo ambayo yatanipata kutoka kwa wabunge kwa maana ya hoja zao za mambo wanayotaka yabadilike lakini kwa jibu la moja kwa moja muda tumeuweka sisi wenyewe wabunge kwenye kanuni ambazo tunao uwezo wa kuzibadili muda wowote tukiona inafaa.