Aidan Khenan achangia kwa mara ya kwanza Bungeni, asema hana mashaka na uzoefu wa Tulia Ackson katika nafasi ya Naibu spika

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,426
7,736
Mbunge wa Nkasi Kaskazini kupitia CHADEMA, Aidan Khenan leo alikuwa wa kwanza kuomba kuuliza swali baada ya Dkt. Tulia Ackson kuomba kura kuwania nafasi ya wabunge kuchagua kuwa naibu spika.

Nalo swali lake lilikuwa kama ifuatavyo

========

Aida Khenan: Mheshimiwa spika nakushukuru, napenda kuuliza swali moja kwa dada yangu Tulia Akson, mbunge wa Mbeya Mjini. Mheshimiwa Spika sina mashaka na uzoefu wa mgombea kwenye nafasi anayoiomba. Natambua kwamba nafasi hiyo ndiyo aliyokuwa nayo kwenye bunge lililopita

Mheshimiwa mgombea miongoni mwa changamoto zilizokuwepo bunge lililopita ni pamoja na changamoto ya muda kwa wabunge kuchangia ndani ya bunge jambo ambalo kwa wananchi pia ilikuwa ni changamoto kidogo, ningependa kujua, umejipangaje juu ya kuweza kuwapa nafasi au muda wa kutosha wabunge ili waweze kuwakilisha mawazo ya wananchi waliowaamini bila kuathiri kanuni?

Spika Ndugai: Bado natafakari, hili swali sio swali! Mheshimiwa Dkt. Tulia Akson majibu tafadhali.

Tulia Ackson: Mheshimiwa spika, mimi kama msaidizi wako mkuu ni wajibu wangu kukushauri katika yale mambo ambayo yatanipata kutoka kwa wabunge kwa maana ya hoja zao za mambo wanayotaka yabadilike lakini kwa jibu la moja kwa moja muda tumeuweka sisi wenyewe wabunge kwenye kanuni ambazo tunao uwezo wa kuzibadili muda wowote tukiona inafaa.
 
Inaonekana huyu mbunge jina la "Chadema" litambeba sana huko bungeni.

Kila atachofanya utasikia mbunge wa Chadema...mbunge wa Chadema.

Hii inazidi kudhihirisha nguvu na mvuto kilichonacho chama chake cha Chadema.
 
..nadhani wanajitahidi sana kumpa nafasi ya kuuliza maswali ili kuonyesha kwamba wanawa-accomodate wapinzani.

..tatizo ni kwamba mbunge mmoja wa upinzani kati ya wabunge 300+ wa chama tawala, ni sawa kikombe cha maji dhidi ya bahari.
 
Tatizo ni kuwa hana uwezo hata wa kupanga hoja. Swali la kwanza anaomba aongezewe muda wa kuongea wakati hata huu alionao hana uwezo wa kuutumia. Huyu anangoja afukuzwe ili apate la kuongelea.

Hivi orodha ya wabunge wote wa kutoka vyama rafiki imetoka?

Amandla...
 
Mbunge wa Nkasi Kaskazini kupitia CHADEMA, Aidan Khenan leo alikuwa wa kwanza kuomba kuuliza swali baada ya Dkt. Tulia Ackson kuomba kura kuwania nafasi ya wabunge kuchagua kuwa naibu spika.

Nalo swali lake lilikuwa kama ifuatavyo

========

Aida Khenan: Mheshimiwa spika nakushukuru, napenda kuuliza swali moja kwa dada yangu Tulia Akson, mbunge wa Mbeya Mjini. Mheshimiwa Spika sina mashaka na uzoefu wa mgombea kwenye nafasi anayoiomba. Natambua kwamba nafasi hiyo ndiyo aliyokuwa nayo kwenye bunge lililopita

Mheshimiwa mgombea miongoni mwa changamoto zilizokuwepo bunge lililopita ni pamoja na changamoto ya muda kwa wabunge kuchangia ndani ya bunge jambo ambalo kwa wananchi pia ilikuwa ni changamoto kidogo, ningependa kujua, umejipangaje juu ya kuweza kuwapa nafasi au muda wa kutosha wabunge ili waweze kuwakilisha mawazo ya wananchi waliowaamini bila kuathiri kanuni?

Spika Ndugai: Bado natafakari, hili swali sio swali! Mheshimiwa Dkt. Tulia Akson majibu tafadhali.

Tulia Ackson: Mheshimiwa spika, mimi kama msaidizi wako mkuu ni wajibu wangu kukushauri katika yale mambo ambayo yatanipata kutoka kwa wabunge kwa maana ya hoja zao za mambo wanayotaka yabadilike lakini kwa jibu la moja kwa moja muda tumeuweka sisi wenyewe wabunge kwenye kanuni ambazo tunao uwezo wa kuzibadili muda wowote tukiona inafaa.
Chadema wanasubiri nini kumfuta uanachama huyo ajuza?
 
Tatizo ni kuwa hana uwezo hata wa kupanga hoja. Swali la kwanza anaomba aongezewe muda wa kuongea wakati hata huu alionao hana uwezo wa kuutumia. Huyu anangoja afukuzwe ili apate la kuongelea.

Hivi orodha ya wabunge wote wa kutoka vyama rafiki imetoka?

Amandla...
Wafute mbunge wa kuchonga kutoka CCM.
 
Anatafuta kiki na asipotumia nafasi hiyo vizuri atakua amefeli sana maishani maana ni mbunge mwenye priority namba1 bungeni kuliko wabunge wote ni mbunge ambae atakua anasikilizwa zaidi kuliko wabunge wengne

Atumie nafas kiukamilifu
 
Tatizo ni kuwa hana uwezo hata wa kupanga hoja. Swali la kwanza anaomba aongezewe muda wa kuongea wakati hata huu alionao hana uwezo wa kuutumia. Huyu anangoja afukuzwe ili apate la kuongelea.

Hivi orodha ya wabunge wote wa kutoka vyama rafiki imetoka?

Amandla...

..ushauri wangu kwa huyu mama ni kwamba asikubali kutumika.

..pia aelewe kwamba yeye peke yake hawezi kuwa mbadala wa kambi rasmi ya upinzani bungeni.

..ukweli ni kwamba bunge la 12 ni bunge la chama kimoja, and there is nothing Hon.Aida Khenan can do to change that.
 
Hilo la kutumika mbona dhahiri tayari amekubali? Angalia kura alizopiga?

Kama angekuwa kweli ana msimamo, angeitumia hiyo nafasi ya kuthibitisha kuwa yeye ni mpinzani wa kweli. Mpinzani wa kweli angepiga kelele na kuwakumbusha wabunge wenzake kuhusu "dhulma" ambayo chama chake kimefanyiwa katika uchaguzi uliopita na kusababisha awe peke yake.

..hisia zangu ni kwamba hata maswali anayouliza anapewa na ccm.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom