MtamaMchungu
JF-Expert Member
- Apr 10, 2011
- 10,089
- 15,023
Maridhiano ya kuunganisha nchi zetu mbili yalikubaliwa enzi na waasisi wa mataifa yetu walikuwa kama wawakilishi wetu katika kutuunganisha kisheria.
Tangu wakati huo wote, sidhani kama kulikuwa na haja ya mtendaji yeyote wa serikali kuchimba chimba au kuuchokonoa muungano wetu tena kwa kuangalia hati ya muungano.
Sasa ulitaka mwanasheria wa Zanzibar aone hati ili iweje? Au ulitaka hati hiyo iwepo Zanzibar ili iweje? Cha msingi maridhiano ya nchi zetu tu, makaratasi ya muungano hayana maana yoyote kwetu.
nyie kalieni mjadala wa hati wakati mjadala ushaanza na jamaa wa serikali mbili wameshaelekea kuwazidi kwa hoja tangu mjadala umeanza jana.Maswali yalikuwa matatu
1. Je hati hiyo ipo?
2. Je hati hiyo ni halali? (hili ndio swali gumu kabisa. uhalali ni pamoja na waliosaini kuwa na mamlaka ya kufanya hivyo)
3. Je muungano ni halali.
Maridhiano ya kuunganisha nchi zetu mbili yalikubaliwa enzi na waasisi wa mataifa yetu walikuwa kama wawakilishi wetu katika kutuunganisha kisheria.
Tangu wakati huo wote, sidhani kama kulikuwa na haja ya mtendaji yeyote wa serikali kuchimba chimba au kuuchokonoa muungano wetu tena kwa kuangalia hati ya muungano.
Sasa ulitaka mwanasheria wa Zanzibar aone hati ili iweje? Au ulitaka hati hiyo iwepo Zanzibar ili iweje? Cha msingi maridhiano ya nchi zetu tu, makaratasi ya muungano hayana maana yoyote kwetu.
Baada ya upotoshaji mkubwa kufanywa bungeni na watu wasio itakia nchi yetu mema wakiwa wameongozwa na Tundu Lissu. Sasa watu hao wamepata aibu ya mwaka baada ya Ikulu kusambaratisha upotoshaji wao.
Tundu Lissu na genge lake la waongo wamekuwa wakipotosha bungeni kuwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar haupo kisheria kisa hakuna hati ya muungano huo. Jambo ambalo limepingwa vikali na Ikulu tena kwa kutoa uthibitisho wa uwepo wa hati hiyo ya muungano.
Lissu na genge lake la wahuni watafute uongo mwingine, maana huu wa upotoshaji juu ya hati ya muungano hauna tena soko. Tuipe pongezi Ikulu kwa kukata mzizi wa fitina.
Hata hivyo kama ikulu ingekuwa makini, isingesubiri hadi maswali yame mengi kiasi hiki, inaonekana kabisa kuna utata fulani kuhusu hiyo hati. Sijawahi kuwa na wasi wasi kuhusu hilo, lakini sasa nina wasi wasi
Lissu hawezi ingia mitini. Alichokifanya ni kutafuta njia ya kumtoa nyoka pangoni ili ampige rungu la kichwa. Kumbuka wajumbe wengi wa CCM walikuwa wanazungumzia misingi ya kuanzishwa muungano ilindwe kulingana na makubaliano ya awali ya waasisi wake. Sasa ndio ( kama hati hiyo ni halali) tutakapo ona kuwa muungano huu uliopo sasa ambao serikali ya Zanzibar imeshajitenga kuwa sio misingi ile ya awali kwa hiyo yale aliyosema Warioba ndiyo yanayopaswa kufanywa sasa katika kuunda katiba mpya.
Nakuhakikishia usione Lissu na wenzie wanacheka ukadhani ni machizi, wameshajua wapi pa kuwapiga bao. Maana sidhani kama hayo yaliyofanyika siku za karibuni yako kwenye hati ya makubaliano ya awali. Tatizo la wale wanaofata msimamo wa Chama na kutukana na kuzomea wanaiga style ya kasuku tuu.
Sent from my iPad using JamiiForums
kwanini hawakuiweka kabla?..Na wewe ulivyo na akili ndogo kiasi hicho na wenyewe waliposema kuwa wataiweka makumbusho ili kila mwananchi aione wanamaana gani?na kwann hawakuweka tangu awali wanasubiria mpaka lisu awachokonoe ndo waionyeshe, hilo ni swali la msingi sana kujiuliza na sio kutuletea hapa vihoja visivyonamsingi najua umetumwa na ccm..!!just first think big kijana kabla hujawasilisha chochote hapa
soma article za mwanzo zinaeleza wazi kuwa katiba ya tanganyika ndo itatumika kama ya muungano,kisha zanzibar itakua na katiba yake kwa ajili ya wananchi wa zanzibar ambayo itakuwa na serikali yenye mamlaka kamili ndani ya zanzibar.Lissu hajaumbuka maccm ndiyo yanaumbuka maana yaliyofichwa miaka 50 salsa adhalani .watuonyeshe kwenye muungano kama Zanzibar ni nchi; na Tanganyika ilienda wapi?
Lissu hajaumbuka maccm ndiyo yanaumbuka maana yaliyofichwa miaka 50 salsa adhalani .watuonyeshe kwenye muungano kama Zanzibar ni nchi; na Tanganyika ilienda wapi?
Hivi hi Tanganyika ambayo watu wanaidai irudi nani anaweza kutuambia uhalali wake, makubaliano ya kuifanya inchi hii itwe Tanganyika yalifanyika wapi na nani walikuwa washiriki wake? je wananchi walihusishwa katika mchakato wa kupata jina Tanganyika? kwa Zanzibar labda kwa sababu yenyewe imepata uhuru wake kwa mapinduzi lakini hi Tanganyika nani anaweza kutusaidia mkataba wa kuifanya inchi iitwe Tanganyika ulifanyika wapi?
Hivi ni nani amekwambia kuna mwana CCM alikuwa anataka kuona hati ya muungano!!!?
Binafsi sina haja ya hayo makaratasi ambayo yanaitwa hati.
Kubwa ambalo nipo interested nalo ni udugu, umoja, mshikamano na maridhiano yetu kama Watanzania. Hili ndio la muhimu na la msingi.
Serikali ya tz haiwezi kuyumbishwa na wehu akina lissu na genge la wahuni wenzake