Aibu ya mwaka yampata Lissu!

Aibu ya mwaka yampata Lissu!

Du watani zangu mnauana kwa hoja, du hii nchi imeishauzwa na aliyeinunua kapoteza hati miliki.
 
Baada ya upotoshaji mkubwa kufanywa bungeni na watu wasio itakia nchi yetu mema wakiwa wameongozwa na Tundu Lissu, sasa watu hao wamepata aibu ya mwaka baada ya Ikulu kusambaratisha upotoshaji wao. Tundu Lissu na genge lake la waongo wamekuwa wakipotosha bungeni kuwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar haupo kisheria kisa hakuna hati ya muungano huo, jambo ambalo limepingwa vikali na Ikulu tena kwa kutoa uthibitisho wa uwepo wa hati ya muungano. Lissu na genge lako la wahuni, tafuteni uongo mwingine, maana wa hati ya muungano hauna tena soko.
Nashangazwa na aibu ya mwaka kabla ya siku mbili zilizoahidiwa hazijafika! Wewe umeshaoneshwa hizo hati za muungano? Kwa nini tusizisubiri ili tujue mbivu na mbichi ni zipi? Je Msekwa naye ambaye hajawahi kuziona tuseme mwongo? Nadhani tuzisubiri kama zipo tutaziona tu!!
 
je hati hiyo hipo? kama hipo ni halali? kama halali muungano ni halali? lishajibiwa moja bado mawili, hati ni halali? kwa mujibu wa copy niliyoiona mimi imefaxiwa saa 9:55 leo tarehe 14 mwezi wa 4, sijajuwa haswaa imetoka wapi ahhhhh kunawalakini hapo
 
Baada ya upotoshaji mkubwa kufanywa bungeni na watu wasio itakia nchi yetu mema wakiwa wameongozwa na Tundu Lissu. Sasa watu hao wamepata aibu ya mwaka baada ya Ikulu kusambaratisha upotoshaji wao.

Tundu Lissu na genge lake la waongo wamekuwa wakipotosha bungeni kuwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar haupo kisheria kisa hakuna hati ya muungano huo. jambo ambalo limepingwa vikali na Ikulu tena kwa kutoa uthibitisho wa uwepo wa hati hiyo ya muungano.

Lissu na genge lako la wahuni, tafuteni uongo mwingine, maana wa upotoshaji juu hati ya muungano hauna tena soko.

Nyumbu wewe sasa ndio umeandika nini?:what:😕
 
Hoja muhimu kuliko zote, hata kama hati ipo, je, lipo wapi azimio la baraza la mapinduzi kuidhinisha muungano? Kama halipo zanziba hawakuridhia muungano kihalali
 
je hati hiyo hipo? kama hipo ni halali? kama halali muungano ni halali? lishajibiwa moja bado mawili, hati ni halali? kwa mujibu wa copy niliyoiona mimi imefaxiwa saa 9:55 leo tarehe 14 mwezi wa 4, sijajuwa haswaa imetoka wapi ahhhhh kunawalakini hapo

mkuu hapa cjakuelewa vizuri,
 
Yani kama sio Lissu hiyo hati isingetolewa milele!naona waliifuata UN usiku baada ya makombora toka kwa wakili msomi
 
Hati ya Muungano inaonesha nchi zilizoungana ni Tanganyika na Zanzibar. Lissu hapo ana point nzuri sana. Jee, Tanganyika iko wapi?

Dada yangu hilo ndio swali la msingi, wapi Tanganyika? Kimsingi hakuna asiyetaka muungano kama inavyopotoshwa,ila lazima uwe wa maridhiano na mfumo unaokubalika kila upande na sii ujanja ujanja au kuburuzana kwa matakwa ya baadhi ya watu.

Sent from my iPad using JamiiForums
 
Baada ya upotoshaji mkubwa kufanywa bungeni na watu wasio itakia nchi yetu mema wakiwa wameongozwa na Tundu Lissu. Sasa watu hao wamepata aibu ya mwaka baada ya Ikulu kusambaratisha upotoshaji wao.

Tundu Lissu na genge lake la waongo wamekuwa wakipotosha bungeni kuwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar haupo kisheria kisa hakuna hati ya muungano huo. jambo ambalo limepingwa vikali na Ikulu tena kwa kutoa uthibitisho wa uwepo wa hati hiyo ya muungano.

Lissu na genge lako la wahuni, tafuteni uongo mwingine, maana wa upotoshaji juu hati ya muungano hauna tena soko.

Hoja ya Lisu inasimama vile vile. Kuwepo kwa hati ni jambo moja na kuridhiwa kwa hati ni jambo la pili. Hoja ya Lisu ni kuwa makubaliano hayo ya Muungano hayakuridhiwa kule Zanziber. Kama imeridhiwa Zanziber nayo itoe hati hiyo ya Muungano kama wanayo. Kama hawana basi ujue kuwa hakuna uhalali wa Muungano huo. Hata kama watakuwa nayo je uliridhiwa na Wazanziber? Hilo ndilo linaloukosesha Muungano uhalali wa Kisheria. Lisu hoja yake inasimama vile vile. Swala siyo kuwepo au kutokuwepo kwa hati bali hati hiyo iliridhiwa na vyombo vya sheria vilivyokuwepo wakati huo? Mwanasheria wa Zanziber ailiwahi kuiona hati hiyo? Hebu uliza kabla ya kurukia hoja hewani na ukaambulia manyoa ukidhani umekamata ndege.
 
Aibu yako mwemyewe, bila lissu hiyo hati wangeitoa?lissu anajua pa kuwatekenya mmekubali kuitoa sasa nani kapata aibu kama sio wewe?kaoge kwanza.
 
Hati ya Muungano inaonesha nchi zilizoungana ni Tanganyika na Zanzibar. Lissu hapo ana point nzuri sana. Jee, Tanganyika iko wapi?

Kama alihitaji hati ili ahoji Tanganyika iko wapi, basi nadhani upeo wake wa kufikiri ni mdogo!! Ina maana bado kuna mtu ambae hajui Tanganyika ilipo?
 
Yani kama sio Lissu hiyo hati isingetolewa milele!naona waliifuata UN usiku baada ya makombora toka kwa wakili msomi

Lissu na genge lake walikuwa wana pigia kelele jambo dogo sana.

Hivi hati ya muungano ni kitu cha serikali kuficha!?

Haya sasa imewekwa hadharani. Imeongeza na kupunguza nini?

Hapo kubwa ni kuumbuka kwa wale wote wenye viherehere waliosema hati hiyo haipo.
 
Hoja muhimu kuliko zote, hata kama hati ipo, je, lipo wapi azimio la baraza la mapinduzi kuidhinisha muungano? Kama halipo zanziba hawakuridhia muungano kihalali

Je wananchi waliridhia Pemba na Unguja ziungane ziwe Zanzibar?
 
Watanzania wengine Hamna Shukrani, asingekuwa Tundu Lisu mngeiona hati ya Muungano lini, na sasa ikulu imesema itapelekwa hadi kuwekwa makumbusho watanzania muweze kuiona, huoni Lisu ameweka historia mpya kwenye nchi hii! Mtoa post hujitabui kabisaaa.
 
Baada ya upotoshaji mkubwa kufanywa bungeni na watu wasio itakia nchi yetu mema wakiwa wameongozwa na Tundu Lissu. Sasa watu hao wamepata aibu ya mwaka baada ya Ikulu kusambaratisha upotoshaji wao.

Tundu Lissu na genge lake la waongo wamekuwa wakipotosha bungeni kuwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar haupo kisheria kisa hakuna hati ya muungano huo. jambo ambalo limepingwa vikali na Ikulu tena kwa kutoa uthibitisho wa uwepo wa hati hiyo ya muungano.

Lissu na genge lako la wahuni, tafuteni uongo mwingine, maana wa upotoshaji juu hati ya muungano hauna tena soko.

Lissu ameshinda kesi kwani kadhibitisha kama serikali inayotuongoza nimatapeli,kwa serikali kutoa hati nyegine baada ya ile walioitoa mwanzo imedhibitisha kuwa serikali imekubali kwamba ile ya mwanzo ilikuwa "fake"..

Cha kujiuliza hapa kwanini serikali imewadangaenye raia wake kwa kitu ambacho ni haki yao,je wananchi tutaamini vipi kama hii hati ya pili nayo sio "fake"

CCM inaleta siasa ya uchwara,siasa za vichochoroni,siasa za kusutana,watanzania tumechoka na siasa kama hizo tuanataka kusikia hoja za msingi kuhusu mungano huu sio kusutana..

Naona serikali ya CCM imejipalia makaa,kutoa hiyo hati ya pili haitosimamisha watanzania kudai haki yao,wako wanaotaka Tanganyika yao na wako wanotaka zanzibar yao,it is too little too late,,,,
 
Hoja ya Lisu inasimama vile vile. Kuwepo kwa hati ni jambo moja na kuridhiwa kwa hati ni jambo la pili. Hoja ya Lisu ni kuwa makubaliano hayo ya Muungano hayakuridhiwa kule Zanziber. Kama imeridhiwa Zanziber nayo itoe hati hiyo ya Muungano kama wanayo. Kama hawana basi ujue kuwa hakuna uhalali wa Muungano huo. Hata kama watakuwa nayo je uliridhiwa na Wazanziber? Hilo ndilo linaloukosesha Muungano uhalali wa Kisheria. Lisu hoja yake inasimama vile vile. Swala siyo kuwepo au kutokuwepo kwa hati bali hati hiyo iliridhiwa na vyombo vya sheria vilivyokuwepo wakati huo? Mwanasheria wa Zanziber ailiwahi kuiona hati hiyo? Hebu uliza kabla ya kurukia hoja hewani na ukaambulia manyoa ukidhani umekamata ndege.

Maridhiano ya kuunganisha nchi zetu mbili yalikubaliwa enzi na waasisi wa mataifa yetu walikuwa kama wawakilishi wetu katika kutuunganisha kisheria.

Tangu wakati huo wote, sidhani kama kulikuwa na haja ya mtendaji yeyote wa serikali kuchimba chimba au kuuchokonoa muungano wetu tena kwa kuangalia hati ya muungano.

Sasa ulitaka mwanasheria wa Zanzibar aone hati ili iweje? Au ulitaka hati hiyo iwepo Zanzibar ili iweje? Cha msingi maridhiano ya nchi zetu tu, makaratasi ya muungano hayana maana yoyote kwetu.
 
Back
Top Bottom