Aibu ya mwaka yampata Lissu!

Aibu ya mwaka yampata Lissu!

tumezubaishwa kiaina na serikali hii ya sisiemu
tumetekwa fikra zetu bila hata ya kujijua
tuko shimoni twazama pasipo kujigundua tutatokaje?
tumewekwa sehemu isiyohusika yaani matopeni bila kujijua
kwanini hawa sisisemu walificha hiyo HATI YA MUUNGANO
wanaipalilia kama kaaranga kikaangoni kwanini walitunyima
haki ya kuiona mapema eti wanasema wanaitunza kutunza gaini
je zile sahihi za nyerere/karume ni kweli original kama sio FEKI
TUMEZUGWA KIAINA WATANGANYIKA TUAMKE HAKUNA CHA HATI
ACHA KUWASEMA KINA LISSU KUWA NI WAONGO NA WANAFIKI
HAWANA UONGO WOWOTE ULE WANACHOSEMA WANAKIJUA
NA IPO SIKU UTAONA MATUNDA YAO USIWE MTU WA POROJO
ZAMA KWA KINA UJUE KUWA NCHI ISHABEMBENDWA

Hatutaki kuja kuona matunda wakati tunayo matunda muungano tunajitafunia tuu
 
Baada ya upotoshaji mkubwa kufanywa bungeni na watu wasio itakia nchi yetu mema wakiwa wameongozwa na Tundu Lissu. Sasa watu hao wamepata aibu ya mwaka baada ya Ikulu kusambaratisha upotoshaji wao.

Tundu Lissu na genge lake la waongo wamekuwa wakipotosha bungeni kuwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar haupo kisheria kisa hakuna hati ya muungano huo. Jambo ambalo limepingwa vikali na Ikulu tena kwa kutoa uthibitisho wa uwepo wa hati hiyo ya muungano.

Lissu na genge lake la wahuni watafute uongo mwingine, maana huu wa upotoshaji juu ya hati ya muungano hauna tena soko. Tuipe pongezi Ikulu kwa kukata mzizi wa fitina.

Mkuu hukufuatilia hotuba ya Lissu inaonekana Ikulu kumejaa vilaza sasa naamini serikali ya CCM haitatufikisha pema bali pabaya. Lissu aliuliza mambo matatu 1 Hati ya Muungano ipo? 2. Iwapo ipo je ni halali? 3. Iwapo hati ni halali je huo Muungano wenyewe ni halali? Iwapo Ikulu wamesema ipo sio tatizo swali la tatu je huo Muungano wenyewe ni halali? Iwapo ni halali iko wapi hati ya sheria toka bunge la Zanzibar kuonyesha Zanzibar ilikubali iwapo Bunge halikupitisha iko wapi Presidantial Decree ya Karume kukubali Zanzibar kuungana na Tanganyika? Maana lazima pawe na hiyo document ambayo pia ni sheria. Iwapo haipo toka Bunge la wawakilishi au presidential decree basi muungano ni batili kwasababu yawezekana Karume alikubali kinyume cha sheria yaani under duress au alikuwa coerced na Julius Nyerere ukizingatia ni Nyerere ndiye alimuweka Karume madarakani kwasababu aliyepindua serikali ya sultani alikuwa ni John Okello toka Uganda kwahiyo Karume alikubali kama pay back kwa Tanganyika kwa kumzuia Okello kuchukua madaraka na kumuweka Karume.
 
Kama alihitaji hati ili ahoji Tanganyika iko wapi, basi nadhani upeo wake wa kufikiri ni mdogo!! Ina maana bado kuna mtu ambae hajui Tanganyika ilipo?

Hakika upeo wako ni mdogo


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Maridhiano ya kuunganisha nchi zetu mbili yalikubaliwa enzi na waasisi wa mataifa yetu walikuwa kama wawakilishi wetu katika kutuunganisha kisheria.

Tangu wakati huo wote, sidhani kama kulikuwa na haja ya mtendaji yeyote wa serikali kuchimba chimba au kuuchokonoa muungano wetu tena kwa kuangalia hati ya muungano.

Sasa ulitaka mwanasheria wa Zanzibar aone hati ili iweje? Au ulitaka hati hiyo iwepo Zanzibar ili iweje? Cha msingi maridhiano ya nchi zetu tu, makaratasi ya muungano hayana maana yoyote kwetu.

Pumba!!! wenzetu hati kama hiyo inawekwa makumbusho kila raia aione,acha mwanasheria mkuu wa nchi
 
Aibu wanaendelea kuipata maccm na serikali yake, hati walizificha za nini kama zilikuwa halali?
 
Je muungano huu ni halali?
Hati hii ni halali?
Sahihi ya nyerere ni halisi?
Sahihi ya karume ni halisi?

Nyie chagadema ni kama mwanamke mwenye gubu. Mwanzo ataomba hiki, ukimpa ataomba kile, na mwisho wa yote ataondoka tu! Mini kabaang shida sana.
 
Hivi ukipokea 'fax' bado inakuwa ni nakala halisi yenye rangi?
Kama 'fax' ilipokelewa tarehe 14 Aprili 2013 kwanini walikuwa hawaitoi?
Baada ya upotoshaji mkubwa kufanywa bungeni na watu wasio itakia nchi yetu mema wakiwa wameongozwa na Tundu Lissu. Sasa watu hao wamepata aibu ya mwaka baada ya Ikulu kusambaratisha upotoshaji wao.

Tundu Lissu na genge lake la waongo wamekuwa wakipotosha bungeni kuwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar haupo kisheria kisa hakuna hati ya muungano huo. Jambo ambalo limepingwa vikali na Ikulu tena kwa kutoa uthibitisho wa uwepo wa hati hiyo ya muungano.

Lissu na genge lake la wahuni watafute uongo mwingine, maana huu wa upotoshaji juu ya hati ya muungano hauna tena soko. Tuipe pongezi Ikulu kwa kukata mzizi wa fitina.
 
soma article za mwanzo zinaeleza wazi kuwa katiba ya tanganyika ndo itatumika kama ya muungano,kisha zanzibar itakua na katiba yake kwa ajili ya wananchi wa zanzibar ambayo itakuwa na serikali yenye mamlaka kamili ndani ya zanzibar.

Article za makubalino zimetaja wazi uwepo wa serikali ya zanzibar katika muungano na haijataja uwepo wa serikali ya Tanganyika tena.
Kwamaana serikali ya Tanganyika imo ndani ya serikali ya Tanzania.

Zanzibar ikiwa na serikali kamili ndio matatizo lukuki yataonekana maan vyanzo vyao vya mapato havipo kabisa, labda mnataka kutuletea magenge ya mamafia zanzibar kiwe kituo cha madawa, na magendo kama ilivyo sasa.
 
We mtoa mada rudisha 7000 uliyopewa naana katika wapotoshaji ni wewe.

Lissu ukitaka kutuonesha anayo aibu wewe lete ushahidi wa hati halali kama ipo!!!

Ikulu hii ambayo mwaka 1993 iliiridhia Zanzibar kujiunga OIC kisha ikaikana unataka tuiamini.
 
Bado sana kipropaganda! Endelea kujifunza,wenzenu zamani walikuwa wanapelekwa Urusi kusomea hizi mambo za propaganda.
 
Back
Top Bottom