Aibu ya mwaka yampata Lissu!

Aibu ya mwaka yampata Lissu!

Naamini kuna na wengine ambao kama ulivyo wewe, hamkumwelewa Tundu Lissu alikuwa anasema nini. Ila kwa tuliomwelewa anachokifanya kinakubalika.

Kupatikana kwa hati ya Muungano siyo kitu kigumu kiasi cha serikali bila aibu kudai iko UN! Kwamba mnataka tueleweje? Ukipangishwa nyumba Mkataba anakaa nao mwenye nyumba au?

Chochote ambacho kilisemwa ni baada ya kigugumizi cha Serikali kuitoa hati hiyo, hata pale ambapo iliombwa na Kamati za bunge maalum la katiba! Ni serikali ya ajabu na iliyojaa upuuzi inayoweza kufanyia mzaha hata swala kama hilo. Vinginevyo ni wazi kuwa nia ya serikali haikuwa njema kwa kuificha hati hiyo.

Hata sasa, pamoja na kutolewa kwa hati hiyo kila mwenye akili timamu anapaswa kujiuliza hati hiyo ilikuwa wapi? Na huko ilikokuwa ilikuwa inafanyiwa nini ndo itolewe leo? Ni kweli Watanzania wanapaswa kuiamini hati hiyo? je! HATI HIYO ILIYOTOLEWA PAMOJA NA KUFICHWA KOTE HUKO NI HATI HALISI NA HALALI?

Nasikitika tu kuwa pamoja na mwamko walio nao Watanzania wengi, bado kuna wanaofikiria kama wewe out there!
cha kuongezea kwa nini hati hiyo ilifichwa mpaka kamati zimemaliza kujadili hizo kanuni mbili ? ndo wazitoe sasa jibu ni moja hawakutaka mapungufu yaliyomo katika mkataba huo yajadiliwe na kamati!!!!!!
 
Mkataba wa muungano uko wazi kuhusu muungano kwa sababu unaonyesha wazi muungano ni wa tanganyika na zanzibar ,hawa waliodai hati wametumia akili sana. Wanajua popote watakapoionyesha wataambiwa wadau wa muungano ni watanganyika na wazanzibar na sio watanzania na wazanzibari. Unapotamka muungano ni lazima uangalie mkataba ni nchi gani ziliungana ,unapoitoa nchi moja unavunja makubaliano na kuifanya nchi moja ni koloni la menzake.rais gani wa muungano wa serikali mbili hana ardhi zanzibar?
 
aliyepata aibu ni serikali. Kwa nini haikutoa hiyo hati mapema? Imeombwa mara mia kidogo lakini mara tunaambiwa iko UN, mara mahakama kuu - yaani usanii tu. Maji yamefika shingoni ndo wanaileta. Wao ndo wamepta aibu
 
Hati ya Muungano inaonesha nchi zilizoungana ni Tanganyika na Zanzibar. Lissu hapo ana point nzuri sana. Jee, Tanganyika iko wapi?

Ziliungana hapo awali zote zikafutika na kuunda Tanzania,, kwa hiyo huwezi kuiona Tanganyika,,, mi sijui huyo mwenzake ameibuka kutoka wapi na nani aliruhusu,,, kama nia ni kulinda muungano, nadhani hilo ndo lilipaswa kuwa swali la msingi na sio kulipa kisasi eti na sisi tunataka Tanganyika yetu lkn tutaulinda muungano,,, huo ni unafiki na hakuna kitu kama hicho,,kila mtu akishajitambua hakuna muungano hapo
 
Tusubiri tuone hii movie itaishaje, japo naamini mambo kama haya yanatakiwa kuwa dynamic
Lissu hawezi ingia mitini. Alichokifanya ni kutafuta njia ya kumtoa nyoka pangoni ili ampige rungu la kichwa. Kumbuka wajumbe wengi wa CCM walikuwa wanazungumzia misingi ya kuanzishwa muungano ilindwe kulingana na makubaliano ya awali ya waasisi wake. Sasa ndio ( kama hati hiyo ni halali) tutakapo ona kuwa muungano huu uliopo sasa ambao serikali ya Zanzibar imeshajitenga kuwa sio misingi ile ya awali kwa hiyo yale aliyosema Warioba ndiyo yanayopaswa kufanywa sasa katika kuunda katiba mpya.
Nakuhakikishia usione Lissu na wenzie wanacheka ukadhani ni machizi, wameshajua wapi pa kuwapiga bao. Maana sidhani kama hayo yaliyofanyika siku za karibuni yako kwenye hati ya makubaliano ya awali. Tatizo la wale wanaofata msimamo wa Chama na kutukana na kuzomea wanaiga style ya kasuku tuu.


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Unachemka, nakubaliana na wewe kuwa wananchi waamue iwapo wanataka muungano ama lah.
Ila Uhalali wa sahihi za Karume na Nyerere ili kujustfy muungano jambo hilo linatakiwa kujibiwa na wale waliokuwa wanahitaji hizo nyaraka.
Nyerere na Karume were right na sijaona kosa lao, ila wenye uchu wa madaraka ndio wametufikisha hapa.
Kwani Nyerere au Karume Ndio walinunua Tanzania? Kwani sahihi zao zina kitu gani cha kufanya Muungano ni halali?

Watanzania wapige kura watakao onekana ni wengi ndo tuamini Muungano vinginevyo sahihi ya nyerere na Karume havitoshi kuhalalisha muungano.
 
Hakuna chochote unachojua, nani alihitaji hio document na kunyimwa? anyway hio hapo na nyingine itawekwa maktaba what next then? unafuata mkumbo wewe, zile hati si bendera au shilingi
aliyepata aibu ni serikali. Kwa nini haikutoa hiyo hati mapema? Imeombwa mara mia kidogo lakini mara tunaambiwa iko UN, mara mahakama kuu - yaani usanii tu. Maji yamefika shingoni ndo wanaileta. Wao ndo wamepta aibu
 
Kama ujui kusoma hilo sio tatizo langu.

Jambo la kufanya ni kuwalaumu wazazi wako ambao wameshindwa kukusomesha.

Who knows, huenda hata wazazi wako hawakwenda shule so hawakuona umuhimu wa ikukupeleka shule.

Jenga hoja acha matusi.
Ujue kuwa wapo wasomi na viongozi wengi ambao wazazi wao hawakwenda shule rasmi. Hivi unafahamu kwamba kuna maeneo mengi nchini ambayo shule zilichelewa kujengwa? Acha maneno ya hovyo
 
Wakuu kweli kimewaka.. Ila wac wac wangu mimi pangu pakavu ni hzo nyaraka (hati) za muungano ni halali, na kama ni halali je itifaki ama makubaliano yaliafikiwa ama kuwekwa na waasisi wetu/Hayati Nyerere na Hayati karume ndani ya hati iyo yanatekelezeka..?
No matter Ugali uko Temeke, Mboga zpo kibasila km njaa ipo utaliwa tu.. Na waliokuwa wakihalalisha muungano pasi na uhalisia wake sasa watautaftia mfukoni..

Kama inje' injeee kama Dani' ndaniii na sio inje Dani inje dani.. Wakuu naomba kuwakilisha.
 
kwani imethibitishwa kuwa niyenyewe?acha kukurupuka, lisu sio mwendawazimu he knows his steps. mtaumbuka tu na usanii weno huo!
 
tundu lissu na genge lake la waongo wamekuwa wakipotosha bungeni kuwa muungano wa tanganyika na zanzibar haupo kisheria kisa hakuna hati ya muungano huo. Jambo ambalo limepingwa vikali na ikulu tena kwa kutoa uthibitisho wa uwepo wa hati hiyo ya muungano.
aibu ya kwenu nyinyi wewe mbulumundu! Kama ndio yenyewe mliificha weeee, kwa miaka 50 tena kama chupi ili mje mlazimishwe kuivua na huyo lissu?
 
[COLOR=#ff0000 said:
PATIENT ZERO[/COLOR];9251858]Kama ujui kusoma hilo sio tatizo langu.

Jambo la kufanya ni kuwalaumu wazazi wako ambao wameshindwa kukusomesha.

Who knows, huenda hata wazazi wako hawakwenda shule so hawakuona umuhimu wa ikukupeleka shule.

Wakati mwingine majina husema mengi zaidi ya tunayoweza kusema, sasa wewe hii maneno ya zero zero ndo uliona ni jina kweli?
 
MKUU KATIKA HILIN HAKUNA MSHINDI.
hapa cha kufanya ni kuondoa na kutatua kabisa kero za muungano.
 
tumezubaishwa kiaina na serikali hii ya sisiemu
tumetekwa fikra zetu bila hata ya kujijua
tuko shimoni twazama pasipo kujigundua tutatokaje?
tumewekwa sehemu isiyohusika yaani matopeni bila kujijua
kwanini hawa sisisemu walificha hiyo HATI YA MUUNGANO
wanaipalilia kama kaaranga kikaangoni kwanini walitunyima
haki ya kuiona mapema eti wanasema wanaitunza kutunza gaini
je zile sahihi za nyerere/karume ni kweli original kama sio FEKI
TUMEZUGWA KIAINA WATANGANYIKA TUAMKE HAKUNA CHA HATI
ACHA KUWASEMA KINA LISSU KUWA NI WAONGO NA WANAFIKI
HAWANA UONGO WOWOTE ULE WANACHOSEMA WANAKIJUA
NA IPO SIKU UTAONA MATUNDA YAO USIWE MTU WA POROJO
ZAMA KWA KINA UJUE KUWA NCHI ISHABEMBENDWA
 
Hakuna aliesema kama hati haipo ,unafikiri kwa akili zako za kukopa kama wangenyamaza kimya Je ingelikuja juu ?
Ni bora wangekomaa na ile fake na mambo yakafifia kiulaini lakini kuileta hapo na kuisambaza ,hicho ndicho kinachotakiwa kwani yale mapandikizi ya mambo ya Muungano ndipo yatakapokoma. Umesikia Jusa akihoji ni kwa makubaliano yepi na nani aliruhusu kuingiza mambo ya ajabuajabu ,Je hati ya Muungano iliruhusu kutendwa hayo kiholela ,je kama kuna taratibu ambazo zilibidi zifuatwe kwa mujibu wa hati hiyo zilifuatwa ? Usishangilie wakati hata mechi haijaanza.
 
Ebu nisaidieni ipi saini halali yakarume hapo?
 

Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1397573551.617596.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1397573551.617596.jpg
    35.4 KB · Views: 101
....mmmmhhhhh...mtoa mada unapotoa mada jaribu kuunganisha name matukio ya nyuma alafu endeleza.....usije rukia Gari kwa mbele pole.........naipenda Tanganyika
 
cha kuongezea kwa nini hati hiyo ilifichwa mpaka kamati zimemaliza kujadili hizo kanuni mbili ? ndo wazitoe sasa jibu ni moja hawakutaka mapungufu yaliyomo katika mkataba huo yajadiliwe na kamati!!!!!!


Haswaaaa! hilo ndo jibu. Na ni hapo ninapotaka Watanzania waone ni jinsi gani hii serikali pamoja na chama chake kilivyojaa hila, na kisivyojali chochote isipokuwa maslahi yao na watoto wao. Mnafikiri wanataka muwanyang'anye nafasi ya kurithishana vyeo kama kwenye nchi za kifalme?
 
Back
Top Bottom