Indume Yene
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 2,950
- 711
Hii sasa thihaka kwa waathirika wa meli iliyozama Zanzibar! Ndugu zangu nikiwa naangalia taarifa ya habari ITV, nimeona waokoaji wakilalamika kuwa baharini kuna miili ya watu wengi tu ila wanashindwa kufanya uokozi sababu hawana vifaa!!!
Jamani, meli yenyewe inasadikiwa kuzama kwa uzembe halafu wanasema vifaa vya uokoaji havipo. Vifaa vyenyewe ni gloves, machela, mafuta ya boti n.k. Jamani wahusika (serikali) acheni mzaha na wananchi. Hivi haya magloves ni tofauti na yale yanayodaiwa na madaktari? Hii nchi jamani acheni masihara hali siyo kabisa!!
Hili suala halitakiwi kuzungumzwa tena hapa maana liko mahakamani. Dr. Ulimboka alikuwa akipigania moja ya vitu kama hivyo...such as gloves na kadhalika zote. Hilo suala lilipelekwa mahakamani hatutakiwi kudiskasi kwa mujibu wa ibara ya 1.8.2.5 ya mwaka 1853 iliyotungwa na na kupitishwa na Bunge la Msoga.