Fahamu kuhusu vifaa vya kuokoa maisha kwenye maji/ meli (Life Saving Appliances)

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
4,930
12,474
Vifaa vya uokoaji maisha kwenye meli ni zana ambazo zimetengenezwa kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu meli au waliopata ajali kwenye maji.

Usafiri wa maji tumekuwa tukiutumia kila mara na ni muhimu katika maisha yetu.

Kwenye sekta ya bahari usalama ni kipaumbele cha Kwanza (Safety is our safety priority). Vifuatavyo ni vifaa vya kuokoa maisha na namna vitumikavyo.

1.Life Jacket
Hili limetengenezwa kwa ajili ya kumfanya mtu aelee akivaa na endapo ataingia kwenye maji lisimuumize mhusika. Kila chombo kinatakiwa kiwe na life jacket sawa na idadi ya watu wanaopakiwa,ya ziada na asilimia 10 ya idadi ya jacket iwe ni za watoto kulingana na idadi ya abiria wapakiwao.

images.jpeg

Life jacket linatakiwa liwe na reflector, filimbi, taa na kamba.

2. Life ring/Life Buoy (Boya)
Hili boya lenye umbo la duara ambalo hutumika kwa kumrushia mtu aliyezama ili ashikilie na kuelea, watu walio kwenye maji pia hushikilia pembeni na kuelea wanapo subiri msaada wa boti ya uokoaji. Hili pembezoni lina kamba za kushikilia ambazo kwenye boya moja mnashikia watu wa 4.
images (1).jpeg


3.Life raft
Hiki ni kifaa ambacho hutumika endapo kuna dharura ya meli kuzama, kuwaka moto au kuhama Meli. Kuna aina mbili za life raft nazo ni Rigid life raft na Inflatable Life raft.

I.Rigid life raft
Hili limetengenezwa kwa material magumu na utumikaji wake hurushwa kwenye maji na watu hushikilia pembeni kusubiri msaada wa uokoaji. Uwezo wake ni watu 8 na kuendelea.

images (2).jpeg


II. Inflatable life raft
Hili ni life raft ambalo limefungwa kwenye kitu mithili ya pipa, na linapotumika hurushwa kwenye maji na kufunguka lenyewe kwa kutumia mekanism ya Hydrostatic Pressure Release unit.

Baada ya kufunguka huwa kama boti, na huudumia watu 6 na kuendelea. Watu huingia kwenye life raft na hupata kukaa kusubiri Msaada.

Picha ya Inflatable Life raft ambalo halijafunguka.
images (3).jpeg


Picha ya ambalo limefunguka baada ya kutupwa kwenye maji.

images (4).jpeg


4.Life boat
Hii ni boti ya ukoaji ambayo huwekwa pembeni ya meli au kivuko hutumika wakati wa tahadhari au ajali yoyote. Hii inashuka majini kwa kushusha kawaida au kutumia mota.
Hii boti inakuwa na injini na inakuwa imefungwa pande zote au ipo wazi.

images (5).jpeg


5. Survival Suits
Kwenye maji licha ya kutumia vifaa vya kusaidia kuelea, kwenye maji watu bado walikuwa wakifa kutokana na baridi Kali. Ndipo kukatengenezwa suti ambazo ni kama ovalori humsaidia mtu kutopoteza joto na baridi. Pia zipo zenye uwezo wa kuelea kutokana na kuwa na boya.
images (6).jpeg


6.Pyrotechnic devices
Hivi ni vifaa ambavyo hutumika kutoa ishara za hatari au dharura baharini. Hivi ni kama zile baruti ambazo huchomwa na kutoa ishara ya rangi,sauti na kuwaka moto.

Baharini kuna aina mbalimbali za pyrotechnics kadri ya matumizi.

I. Rocket Parachute Flare
Hii hutumika kuonyesha ishara wakati wa mchana na usiku, pia ina uwezo wa kuonekana umbali mrefu zaidi. Huwa katika rangi nyeupe na nyekundu.

images (7).jpeg


II. Hand flare
Hii ikichomwa huonyesha rangi ya orange au nyekundu, hutumika kutoa taarifa kwa umbali mfupi.Inaweza ikaungua kwa muda wa dakika moja mpaka kumalizika na unatakiwa uweke sehemu inayoonekana.

images (8).jpeg


III. Buoyant smoke signals
Hii inatumika kutoa ishara baina ya boti iliyozama na inayookoa endapo eneo lenye tatizo. Hii uwasha na utoa mwanga mkali mwekundu na husaidia kutoa taarifa ya eneo lenye ngazi au kuona sehemu yenye tatizo wakati wa uokoaji.

images (9).jpeg


Hivyo ndio baadhi ya vifaa vya uokoaji na matumizi yake, wengi tunaweza tukawa tunaviona ila hatukujua umuhimu na matumizi. Usalama kwenye chombo cha majini ni jukumu letu sote.

"Acta non verba"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom