Aibu kubwa kwa polisi - hadi sasa wachoma makanisa Zenj na waliomteka Ulimboka hawajakamatwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aibu kubwa kwa polisi - hadi sasa wachoma makanisa Zenj na waliomteka Ulimboka hawajakamatwa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Jul 11, 2012.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Leo hii ni karibu miezi miwili na nusu tangu makanisa yachomwe huko Zanzibar na 'watu wasiojulikana'. Na vile vile ni karibu wiki tatu tangu Dr Ulimboka akamatwe na 'watu wasiojulkana na kupigwa vibaya.

  Matukio yote mawili jeshi letu la polisi lilidai kuwa lingefanya uchunguzi wa kina na kuwakamata wahusika na kuwapeleka katika vyombo vya sheria, lakini hata mtu mmoja hajakamatwa.

  Hii jamani siyo aibu kubwa kwa jeshi letu la polisi ambalo juzi tu waziri wao, Dr Nchimbi alijidai ni jeshi makini na kwamba yoyote asiyeliamini ana matatizo?

  Zanzibar ni sehemu ndogo sana na watu wachache ambao wengi wanajijua. Inakuwaje hadi sasa polisi imeshindwa kuwakamata wahusika wa uchomaji wa makanisa?

  Au sasa tuanze kuamini yanayozungumzwa sana, tena sana mitaani kwamba kuna mkono wa serikali katika matukio yote mawili, na polisi kazi yake ni kuilinda tu serikali kwa maovu hayo?
   
 2. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Nimesoma jana JF kuwa Erick Shigongo ameshikwa, sijui kwanini? Jee, inaweza kuwa anahusika na hayo matukio?
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Jul 11, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Unajua mwizi anapopigwa na wananchi, polisi hajui amkamate nani ikiwa mwizi huyo amekufa au amefariki.

  Sasa kwa hili la makanisa ile ni kama riot imetokea, inaweza nkuwa vibaka,au hao uamsho ambao wamekanusha pia inawezekana ni vikosi kazi mbaya vya serikali ,ili kuwadhibiti watu flani kwa kuwasingizia, ila WaZanzibari ni wamoja hivyo hilo limefeli, la Ulimboka hatujui kinachoendelea kwani waliokuwa na Dr katika hatua za mwanzo wapo, mawasiliano yapo, maana kama simu ya Uli ilipotea data za simu yake zinakuwepo katika kampuni ya simu ,alimpigia nani alipigiwa na nani kwa wakati huo aliotoweka.

  Huwezi kupata mazungumzo lakini wapi na wapi alipiga na kupokea simu utaweza kuzijua namba zilizohusika kama CDM wana mshiko ndani ya makampuni ya simu wanaweza kujua alizungumza na kupigiwa na namba ipi au zipi.
   
 4. kibol

  kibol JF-Expert Member

  #4
  Jul 11, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 3,138
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180
  watajikamataje wenyewe ilihali jeshi lenyewe linaendeshwa na vichwa sampuli ya ZOMBA.
   
 5. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #5
  Jul 11, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,199
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Kamuulize mkuu wa kitengo cha mabwepande jack zoka
   
 6. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #6
  Jul 11, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Haaahaaa! Asije akawa amewaandika waheshimiwa kwenye vile vigazeti vyake. On a serious note, mbona polisi ina suasua kufanya kazi yake kwenye baadhi ya matukio?
   
 7. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #7
  Jul 11, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Kama serikali ikiamua, inaweza kabisa kutumia mkono wake mrefu kuwakamata wahusika wote. Kimya kingi kina mshindo mkuu. Hii haijakaa vizuri
   
 8. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #8
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  iliwachukua miaka 10 majasusi wa CIA kumnasa na kumuua Osama Bin Laden.

  Iliwachukua miezi kadhaa hadi tarehe 31 Mei 2012 kwa Jeshi la polisi kumkamata aliyemuua Mwenyekiti wa chadema Arumeru. Muuaji Alikuwa kakimbilia Singida.

  Wahalifu wote wana mbinu zao hakuna muda maalum kwa chombo cha dola wa kumkamata mhalifu. Ni mapema sana kusema polisi wameshindwa kuwasaka na kuwanasa.
   
 9. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #9
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  kama ni taarifa zinazoweza kulisaidia jeshi la polisi ni vema zikapolekwa sehemu husika kwa ajili ya kusaidia uchunguzi..... kwa yule mwenye taarifa kwa kina.
   
 10. mangikule

  mangikule JF-Expert Member

  #10
  Jul 11, 2012
  Joined: Jun 11, 2012
  Messages: 3,177
  Likes Received: 1,259
  Trophy Points: 280
  Thubutuu!! Polisi awakamate TISS!! haiwezekani!!
   
 11. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #11
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Uchunguzi duniani kote sio suala la serikali kuamua .....

  Ningekuelewa kidogo ungesema ni suala la wananchi kuamua kuisaidia serikali kuipa ushirikiano wa kuwakamata wahalifu kwani wahalifu tunaishi nao kwenye jamii.
   
 12. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #12
  Jul 11, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Kwani kwetu hapa sifa za amani na utulivu ana jipa nani? wananchi wanasifiwa popote pale au ni nyinyi waheshimiwa tu ndio mnahusika na kutunza amani na utulivu? Kama wananchi wanatoa michango yao, ina maana so far hakuna hata mwananchi mmoja aliyetoa mwelekeo wa wahusika wa matukio hayo yote?
   
 13. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #13
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Hakuna iliye juu ya sheria ni mashaka yako tu.

  TISS imeundwa kisheria hivyo kinyume chake ni kukiuka sheria..... polisi hawawezi kushindwa kuwakamata.

  Tumeshuhudia wanajeshi (JWTZ) na TISS wamekamatwa na kufikishwa mahakamani.

  post yako inataka kuonyesha kuwa TISS wanaweza kufanya lolote na wasiguswe na sheria si kweli.
   
 14. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #14
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135


  Anaweza kuwepo polisi mmoja mmoja aliyekosa wajibu kama ilivyo kwa mchungaji, askofu, sheikh na Imam kukosa wajibu wake lakini hiyo haina maana kwamba nyumba za ibada makanisa na misikiti sio mahali patakatifu.

  Ingependeza kama wewe mwenyewe ungetoa mfano wa ushiriki wako wa kutoa ushirikiano kwa polisi.... ulikwenda kituo kipi cha polisi, kwa kesi ipi na ulikutana na nani kwa ushaidi upi, na kunyimwa haki yako.

  kusimulia hadithi za wengine ndiko kunatupeleka hadi kwenye magomvi mengi kama ya kidini na kikabila.
   
 15. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #15
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135

  Utani kama huu ndio unatufanya kutia mashaka dhidi ya tuhuma za Zoka... kujenga hoja kutatusaidia kuamini
   
 16. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #16
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135


  Utani kama huu ndio unatufanya kutia mashaka dhidi ya tuhuma za Zoka... kujenga hoja kutatusaidia kuamini dhidi yake.....utani unaongeza mashaka.

  Tuhuma zinazoacha shaka hata mahakamani hutupwa
   
 17. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #17
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  sio rahisi kuandika jambo zuri dhidi ya jeshi la polisi kama unalichukia, post imejaa kulichukua jeshi lote na kila Afisa wa jeshi sio fear hata kidogo.

  Ni juzi tu polisi walikuja kuniokoa mimi na familia yangu tulipovamiwa na majambazi wakafanikiwa kumuua mmoja na kukamata wawili.
   
 18. KASHOROBANA

  KASHOROBANA JF-Expert Member

  #18
  Jul 11, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,249
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  HAPO UJUE WAO NDO WAHUSIKA WAKUBWA AU NI INSTRUCTION FR TISS/ UWT NA HATA WANASHINDWA WAMBANE NANI?? aaaahh
   
 19. C

  Careboy wamuntere Senior Member

  #19
  Jul 11, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 163
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna kitu ambacho watu hawajui, Polisi ni chombo ambacho kina professional ethics zake, na sio kila anayekamatwa na polisi kwa tuhuma basi ni muhalifu ndo maana upelelezi unafanyika ili kupata ushahidi, tukumbuke sheria zetu zinasema mtuhumiwa anahaki zake hadi pale tuhuma zitakapothibitishwa zidi yake, na hata kama kuna watu wamekamatwa hawawezi kutangazwa kwenye vyombo vya habari kwa sababu upelelezi wake unaweza kuwa mgumu, sasa tujiulize hivi tunauelewa wa kutosha kweli?

  Au tunafuata mkumbo tu wa kisiasa kulaumu? Mimi ninachojua polisi ktk mambo ya uchunguzi inafanya kazi kwa usiri mkubwa kwa lengo la kuwalinda mainformer, na vilex2 kulinda haki za watuhumiwa.

  Sasa mnapotaka itangaze kila kitu mnataka kuingilia kazi za vyombo vya dola? kama ni hivyo basi nawashauri muingie kazi za polisi ili muone utendaji wake ulivyo. tukumbuke Polisi sio wanasiasa.
   
 20. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #20
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Ukiona mtu anachukia Polisi na vyombo vya dola ujuwe huyo ni mhalifu sugu.
   
Loading...