Ciril
JF-Expert Member
- Jan 10, 2011
- 8,558
- 7,156
Leo hii ni karibu miezi miwili na nusu tangu makanisa yachomwe huko Zanzibar na 'watu wasiojulikana'. Na vile vile ni karibu wiki tatu tangu Dr Ulimboka akamatwe na 'watu wasiojulkana na kupigwa vibaya.
Matukio yote mawili jeshi letu la polisi lilidai kuwa lingefanya uchunguzi wa kina na kuwakamata wahusika na kuwapeleka katika vyombo vya sheria, lakini hata mtu mmoja hajakamatwa.
Hii jamani siyo aibu kubwa kwa jeshi letu la polisi ambalo juzi tu waziri wao, Dr Nchimbi alijidai ni jeshi makini na kwamba yoyote asiyeliamini ana matatizo?
Zanzibar ni sehemu ndogo sana na watu wachache ambao wengi wanajijua. Inakuwaje hadi sasa polisi imeshindwa kuwakamata wahusika wa uchomaji wa makanisa?
Au sasa tuanze kuamini yanayozungumzwa sana, tena sana mitaani kwamba kuna mkono wa serikali katika matukio yote mawili, na polisi kazi yake ni kuilinda tu serikali kwa maovu hayo?
Vyombo vya usalama vikiamua vinaweza tatizo ni vile vinafanya kazi kwa mashinikizo/maagizo kutoka juu kwa manufaa ya walio juu(viongozi Wa juu Serikalini)