pascaldaudi
JF-Expert Member
- Mar 25, 2009
- 534
- 96
'Ndugu zangu wa Tanga kila siku nawasikia wapinzani wanakuja kwenu kuwaomba kura na kuwaahidi eti elimu na afya itakuwa bure hayo si ya kweli wameishiwa sera ndio maana kila siku wanasema hayo hayo," alisema Dk Bilal.
Unajua elimu ya bure ni moja ya sera iliyoiangusha KANU Kenya maana wao walisema haiwezekani, NARC wakaitumia hiyo nafasi, hivi hawajifunzi hawa watu, yaani,Swali la msingi yeye elimu yake hakusoma bure?
Baba yake alikuwa na ela za kumsomesha,ebue aende Namtumbo aendeleze fani yake ya Nuclear
Dk Bilal alisema watajenga viwanda ili kuumarisha uchumi wa Taifa na kuwapa ajira vijana na bidhaa hizi zitasafirishwa kwenda nje ya nchi kupitia bandari ya Tanga na serikali itaongeza mapato yake na kutekeleza ahadi zake.
Dk Bilal asema kusomesha bure ni ndoto za mchana Send to a friend Thursday, 07 October 2010 08:12 0diggsdigg
Salim Mohamed na Raisa Said, Tanga
MGOMBEA mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk Mohamed Bilal amewataka wananchi wa Mkoa wa Tanga kuwapuuza wapinzani kwa wanasema kwamba wakiingia madarakani wataoa huduma ya elimu na afya bure kwa kuwa mpango huo ni sawa na ndoto za mchana.
Dk Bilal aliyasema hayo jana katika mkutano wa kampeni wa chama chake uliofanyika katika uwanja wa Tangamano pamoja na mambo mengine alisema wananchi wa Tanga wakiwapeleka madarakani wataiboresha huduma ya usafiri wa Reli.
'Ndugu zangu wa Tanga kila siku nawasikia wapinzani wanakuja kwenu kuwaomba kura na kuwaahidi eti elimu na afya itakuwa bure hayo si ya kweli wameishiwa sera ndio maana kila siku wanasema hayo hayo," alisema Dk Bilal.
Dk Bilal alisema watajenga viwanda ili kuumarisha uchumi wa Taifa na kuwapa ajira vijana na bidhaa hizi zitasafirishwa kwenda nje ya nchi kupitia bandari ya Tanga na serikali itaongeza mapato yake na kutekeleza ahadi zake.
Alisema CCM imetekeleza ilani yake ya uchaguzi tangu uchaguzi wa kwanza wa mwaka 1995 na kuweza kufikia asilimia 98 na bado asilimia 2 tu ili iweze kufikia malengo yake na kuwataka wananchi wa mkoa huo kuwapa kura nyingi siku ya uchaguzi.
Alisema chama cha CCM kina uzoefu wa kuiongoza nchi na kudai kuwa ndio maana wanaomba tena wachaguliwe.
Source mwananchi (Dk Bilal asema kusomesha bure ni ndoto za mchana)
Dr. Bilal yeye ndiye amefilisika kisiasa kwa sababu kama misamaha ya kodi kwa wachimbaji madini wakubwa ikiondolewa tu tutaokoa shilingi bilioni 700 kila mwaka. Angetafakari hilo tu asingeweza kuthubutu kusema haya:-
Ajue tunahitaji bilioni 38 tu kuwaongezea wanafunzi wa vyuo vikuu ili wakasome kwa furaha na bilioni 400 tu kufanikisha mpango wa elimu ya msingi hadi kidato cha sita kuwa bwerere............katika bilioni 700 bado tuna mabaki mengi ya kuwalipa waalimu, kuwajengea nyumba, kulipia huduma za afya na kuwa bure na kukarabati vyuo vyetu ambavyo vimechoka sana.
Lakini Dr. Bilal ni wa kumpuuza tu kwa mtu aliyekwenda kusomea nuklia tekinolojia miaka ya sitini halafu huku akijua nchi yake haikuwa na uwezo wa kuiendeleza inatuthibitishia ya kuwa siyo mtu wa mikakati ya muda mrefu na kwa CCM kumwona ni "mwenzao" basi CCM wote wamepofuka na ndio maana utajiri wa nchi wanawakabidhi wageni badala ya wazawa.