Rais Dk. Mwinyi asema mbio za marathon zina faida ya kiafya, ajira na uchumi

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
738
479
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema mbio za Marathon zina faida ya kiafya, ajira na uchumi .

Rais Dk. Mwinyi amesema hayo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika msimu wa tatu wa mbio za Zanzibar International Marathon kuanzia kilometa 5, 10 na 21 zilizoshirikisha wakimbiaji wa nchi mbalimbali za Afrika Mashariki, Ulaya na Amerika leo tarehe 29 Oktoba 2023 eneo la Forodhani, Mkoa wa Mjini Magharibi

Aidha Rais Dk. Mwinyi ameeleza katika kuvutia wageni kipindi chote cha msimu mdogo wa watalii tuwe tuna utalii wa matukio ikiwemo Tamasha la ZIFF, Sauti za Busara, pamoja na matukio ya kimichezo ikiwemo mbio za Zanzibar International Marathon kwa kuhamasisha kufurika wageni vipindi vyote msimu mkubwa na mdogo wa utalii.

Vilevile Rais Dk. Mwinyi ametoa wito kwa wananchi kufanya mazoezi kila wakati kwa kujiunga na vikundi vya mazoezi kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiiza yakiwemo shinikizo la damu, kisukari, magonjwa ya moyo, saratani, kiharusi na mengineyo.

Pia viongozi mbalimbali wa Serikali wa SMT na SMZ pamoja na wadau wa taasisi binafsi na michezo wameshiriki mbio hizo.

29 Oktoba, 2023.

Forodhani, Mkoa wa Mjini Magharibi.View attachment 2796975View attachment 2796976
IMG-20231029-WA0021.jpg
IMG-20231029-WA0020.jpg
IMG-20231029-WA0023.jpg
IMG-20231029-WA0024.jpg
IMG-20231029-WA0028.jpg
IMG-20231029-WA0027.jpg
IMG-20231029-WA0025.jpg
IMG-20231029-WA0026.jpg
IMG-20231029-WA0029.jpg
IMG-20231029-WA0030.jpg
IMG-20231029-WA0015.jpg
IMG-20231029-WA0017.jpg
IMG-20231029-WA0022.jpg
IMG-20231029-WA0016.jpg
IMG-20231029-WA0018.jpg
IMG-20231029-WA0013.jpg
 

Attachments

  • IMG-20231029-WA0013.jpg
    IMG-20231029-WA0013.jpg
    62.8 KB · Views: 2
Wenzetu Kenya marathon ni dili, wengi wanetajirika na kupata umaarufu kwa majina na picha zao kutumika kwenye matangazo ya biashara.
 
Back
Top Bottom