Aibu!!! Dk Bilal asema kusomesha bure ni ndoto za mchana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aibu!!! Dk Bilal asema kusomesha bure ni ndoto za mchana

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by pascaldaudi, Oct 7, 2010.

 1. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Dk Bilal asema kusomesha bure ni ndoto za mchana Send to a friend Thursday, 07 October 2010 08:12 0diggsdigg

  Salim Mohamed na Raisa Said, Tanga

  MGOMBEA mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk Mohamed Bilal amewataka wananchi wa Mkoa wa Tanga kuwapuuza wapinzani kwa wanasema kwamba wakiingia madarakani wataoa huduma ya elimu na afya bure kwa kuwa mpango huo ni sawa na ndoto za mchana.

  Dk Bilal aliyasema hayo jana katika mkutano wa kampeni wa chama chake uliofanyika katika uwanja wa Tangamano pamoja na mambo mengine alisema wananchi wa Tanga wakiwapeleka madarakani wataiboresha huduma ya usafiri wa Reli.


  'Ndugu zangu wa Tanga kila siku nawasikia wapinzani wanakuja kwenu kuwaomba kura na kuwaahidi eti elimu na afya itakuwa bure hayo si ya kweli wameishiwa sera ndio maana kila siku wanasema hayo hayo," alisema Dk Bilal.

  Dk Bilal alisema watajenga viwanda ili kuumarisha uchumi wa Taifa na kuwapa ajira vijana na bidhaa hizi zitasafirishwa kwenda nje ya nchi kupitia bandari ya Tanga na serikali itaongeza mapato yake na kutekeleza ahadi zake.

  Alisema CCM imetekeleza ilani yake ya uchaguzi tangu uchaguzi wa kwanza wa mwaka 1995 na kuweza kufikia asilimia 98 na bado asilimia 2 tu ili iweze kufikia malengo yake na kuwataka wananchi wa mkoa huo kuwapa kura nyingi siku ya uchaguzi.

  Alisema chama cha CCM kina uzoefu wa kuiongoza nchi na kudai kuwa ndio maana wanaomba tena wachaguliwe.
  Source mwananchi (Dk Bilal asema kusomesha bure ni ndoto za mchana)
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Dr. Bilal yeye ndiye amefilisika kisiasa kwa sababu kama misamaha ya kodi kwa wachimbaji madini wakubwa ikiondolewa tu tutaokoa shilingi bilioni 700 kila mwaka. Angetafakari hilo tu asingeweza kuthubutu kusema haya:-

  Ajue tunahitaji bilioni 38 tu kuwaongezea wanafunzi wa vyuo vikuu ili wakasome kwa furaha na bilioni 400 tu kufanikisha mpango wa elimu ya msingi hadi kidato cha sita kuwa bwerere............katika bilioni 700 bado tuna mabaki mengi ya kuwalipa waalimu, kuwajengea nyumba, kulipia huduma za afya na kuwa bure na kukarabati vyuo vyetu ambavyo vimechoka sana.

  Lakini Dr. Bilal ni wa kumpuuza tu kwa mtu aliyekwenda kusomea nuklia tekinolojia miaka ya sitini halafu huku akijua nchi yake haikuwa na uwezo wa kuiendeleza inatuthibitishia ya kuwa siyo mtu wa mikakati ya muda mrefu na kwa CCM kumwona ni "mwenzao" basi CCM wote wamepofuka na ndio maana utajiri wa nchi wanawakabidhi wageni badala ya wazawa.
   
 3. tempo_user1

  tempo_user1 Senior Member

  #3
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kauli hizi za akina Bilal hakika sitawapigia kura ccm hata kwa bakora, Bilal sasa anazeeka vibaya
   
 4. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Kwani dokta bilal ni wachama gani?
  Hawa sisim wanamatatizo gani si wapige sera zao kazi kurekebisha za wenzao tuuu mbona wao wanaahadi kibao na hata moja hawataweza kutekeleza si walikuwepo na bado wapo madarakani hawa!??????
   
 5. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Swali la msingi yeye elimu yake hakusoma bure?
  Baba yake alikuwa na ela za kumsomesha,ebue aende Namtumbo aendeleze fani yake ya Nuclear
   
 6. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #6
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  anasema ni ndoto coz anaelewa wakisomesha bure watapata wapi hela ya kujineemesha,anawaza mbali ndo maana anasema hivyo,si unajua bajet ya elimu wanaimega kimtindo?
   
 7. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Unajua elimu ya bure ni moja ya sera iliyoiangusha KANU Kenya maana wao walisema haiwezekani, NARC wakaitumia hiyo nafasi, hivi hawajifunzi hawa watu, yaani,

  1. madini
  2. makaa ya mawe,
  3. mbuga
  4. ardhi safi yenye rutuba,
  5. mabonde na mito
  6. maziwa
  7. ............
   
 8. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #8
  Oct 7, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mimi nilidhani wakati wa serikali kujenga viwanda uliishapita? Au wanataka kuturudisha tena kwa Mwalimu?

  Amandla.......
   
 9. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #9
  Oct 7, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,356
  Likes Received: 3,123
  Trophy Points: 280
  kuna dr.mmoja tu yaani DR.SLAA wengine wote fotokopi km akina dr.bilal,dr kikwete yaani madokta uchwara ambao hawaamini ktk ustawi wa taifa hili...yaani hawaamini kuwa wanawasamehe wezi wa mali za nchi hawaamini kuwa tanzanite inapatikakana tz tu........tukiwa na watu wenye imani ya namna hii kamwe hatuwezi kusogea hata chembe kimaendeleo kwani hawana upeo wa kutuongoza na wala hawana ufahamu na wameishiwa kifikra
   
 10. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #10
  Oct 7, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Hivi hamjiulizi Bilal hiyo kauli kaitolea wapi??
   
 11. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #11
  Oct 7, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kumbe Dk bilal naye ni fisadi!, yaani raslimali zote tulizonazo, mpaka wazungu wanatushangaa, wewe mpaka bush kuja Tanzania siyo mchezo, nchi imejaa utajiri wa hali ya juu,
   
 12. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #12
  Oct 7, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Ni viongozi ambao mwisho wao wa kufikiri umegota!!!! Hili jamabo wenzetu wanalifanya na ni msingi mkubwa ssaana wa maendeleo kwa taifa..... hivi huyu Bilali mbona anajikomelea nguo nzitonzito ni miwani nyeusi tii anamatatizo gani?
   
 13. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #13
  Oct 7, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Lakini ingekuwa vyema kama tungeambiwa hiyo elimu na huduma za afya za bure zingegharimiwa vipi. tusipende mno majibu mepesi kwa maswali magumu.

  Amandla.......
   
 14. d

  dotto JF-Expert Member

  #14
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  .... huyu mbovu naye. dawa ni kuweka pembeni hawa wazee. pesa za kumwaga kwenye kampeni zipo ila za watoto wa kidanganyika ndoto. Mabango ya kampeni TAnzania nzima wametoa wapi!!. Ruzuku ya CCM inakura kodi kiasi gani.HUu ni uwendawazimu!! Kula kichwa cha CCM mpe Dr.Slaa ushindi. HAKIKISHA HAWA WAZEE WENYE FIKRA MGANDO HAWARUDI TENA MPAKA BAADA YA MIAKA 300 IJAYO. TUNATAKA IBAKI HISTORIA. WEKA CCM MAKUMBUSHO - KOFIA ZAO NA TSHIRT.
   
 15. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #15
  Oct 7, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Watu ambao hata tsh 10,000 ni kama dhahabu...afu unaenda kuwaambia wawapuuze wanaosema watawasaidia..?
  Kweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa...
  Hicho chama sio tena kwa manufaa ya walalahoi tena...!
   
 16. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #16
  Oct 7, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  jamani hizi ni ahadi za chadema zilizotekelezwa japo si na chadema ili ujue zinatekelezeka
  1.chuo kikuu cha dodoma
  2.kufuta kodi ya kichwa.
  3.kutokuhamia dodoma.
  4.kujenga shule za sekondari kila kata
  naomba tuendeleze........................................................hapo hawajashika madaraka.

  na hizi ni za ccm ambazo hazitekelezeki.
  1.maisha bora kwa kila mtanzania.
  2.kuhamia dodoma.
  3.hakuna mtoto atakaekosa elimu kisa mzazi wake hana hela
  endelezeni wajameni ili tujue kama chadema wanaweza kutoa elimu bure au la nawakilisha.
   
 17. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #17
  Oct 7, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Hawa wazee wa CCM akili zao zimeoza kweli.

  Vipi, aliposema hizo pumba Wagosi walishangilia?

  (Siyo kosa lake. Amezoea kula urojo na juisi za miwa pale Mkunazini. Hajui hata kama Tanzania Bara kuna utajiri wa madini na maliasili nyingi zinazoliwa na mafisadi)
   
 18. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #18
  Oct 7, 2010
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  hawa nao tushawachoka. Wanaona watz wote ni mazuzu kama wao. Ahadi zao ni nyingi mno na mikakati ya kuzitekeleza hakuna. Yaani ahadi kwao zimekuwa kama daraja la kuvuka uchaguzi na ushindi. Kikwete kaahidi meli, viwanja vya ndege, bajaj 400 ..nk..
   
 19. E=mcsquared

  E=mcsquared JF-Expert Member

  #19
  Oct 7, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 221
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Ndugu yangu hoja zako zinaniumiza sana, almost nalia hapa nilipo. Lakini hata wewe pia naona namna ulivyo mzalendo na pia ulivyo na uchungu na nchi yako.

  Motto wetu naomba uwe huu: OKTOBA 31 TUPELEKE IKULU DR SLAA HATUHITAJI KUMUONA MTAANI TENA, HATUNA SHIDA NAYE MTAANI, AENDE AKAKAE HUKO!
   
 20. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #20
  Oct 7, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  It is very unfortunate a person with the ambition of becoming a president has put for himself such low limitations. It is only those with poor mentality that they set barriers against their potentials, the rich do not have the words impossible, cannot be done, it is beyond our ability and like negative words in their vocabraly.
  They only think and ask the questions that start with a how or why, etc..... POOR YOU DR BILAL, I should believe you uttering these words to please your incompetent boss and not from your heart.
   
Loading...