Rais Mwinyi asema darajani ni sehemu kuu ya biashara Zanzibar

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
741
479
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar sehemu kuu ya biashara ni Darajani hivyo Serikali imeanza na ujenzi wa maduka ya kisasa Darajani Bazaar, eneo la kuegeshea magari la kisasa, pamoja na vituo vya kisasa vya mabasi.

Amesema lengo la Serikali ni kuwa na sehemu ya mji wa kisasa utakaotoa huduma zote kwa wananchi ikiwemo usafiri wa umma wa mabasi na vituo vyake, maegesho ya magari ya kisasa pamoja na biashara.

Rais Dk. Mwinyi amesema hayo alipoweka jiwe la Msingi Mradi Maegesho ya Magari Malindi kuelekea shamrashamra za Miaka 60 viwanja vya Malindi Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe: 21 Desemba, 2023.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi ameeleza kuwa yanayofanyika ni kwa nia njema kulinda urithi wa dunia kwa maeneo yote ya Mji Mkongwe kwa kuzingatia masharti na taratibu za Shirika la Umoja wa Mataifa UNESCO kwa utekelezaji wa miradi maendeleo nchini.

Vilevile Rais Dk. Mwinyi amesema Serikali ya awamu ya nane itaendelea kujenga miradi mikubwa ya maendeleo na kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025.

Halikadhalika mradi huo wa kisasa wa maegesho ya magari unajengwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 6 na magari zaidi ya miambili yataegeshwa kwa wakati mmoja.
IMG-20231221-WA0009.jpg
IMG-20231221-WA0018.jpg
IMG-20231221-WA0017.jpg
IMG-20231221-WA0016.jpg
IMG-20231221-WA0012.jpg
IMG-20231221-WA0015.jpg
IMG-20231221-WA0014.jpg
IMG-20231221-WA0014.jpg
IMG-20231221-WA0010.jpg
IMG-20231221-WA0011.jpg
IMG-20231221-WA0008.jpg
IMG-20231221-WA0007.jpg
IMG-20231221-WA0006.jpg
IMG-20231221-WA0004.jpg
IMG-20231221-WA0005.jpg
IMG-20231221-WA0003.jpg
IMG-20231221-WA0002.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom