Elections 2010 Aibu!!! Dk Bilal asema kusomesha bure ni ndoto za mchana

Kwani dokta bilal ni wachama gani?
Hawa sisim wanamatatizo gani si wapige sera zao kazi kurekebisha za wenzao tuuu mbona wao wanaahadi kibao na hata moja hawataweza kutekeleza si walikuwepo na bado wapo madarakani hawa!??????

Nadhani yuko CCM, ila najua akishapata madaraka tu atabadilika na kuwa "CUF ndani ya CCM", CUF ile ya Zanzibar, siyo ya huku kwetu Bara
 
Huo ndio msimamo wa chama CCM kisichokuwa na jipya...just astray...Just like a stray bullet that can land on anything
 
Mimi nashangaa sana kuna watu ambao wanaamini kuwa kama jambo fulani hawezi kulifanya au ni gumu kwake kulifanya,basi huzani jambo hilo ni gumu kufanywa na kila mtu na hujitahidi kuaminisha wengine kuwa jambo hilo haliweze kufanyika!Haya ni mawazo mgando.Kuna watu siku za nyuma walikuwa wanaamini haitakuja kuwezekana kwenda mwezini,lakini mbona watu walifika mwezini?
 
Very pure and simple, hivi mnamwelewa hata Bilal anachongea, kama anaongelea akiwa usingizini, hajui nyakati, pointless, mindless, sijui Dr gani hawa, watu wamemchoka, sijui anaota, anaimba, hajui jinsi watu walivyomkinai, mwaka huu CCM wamechemsha, nikija kwa Makamba huyu ndiyo jackass, CCM bye byeeeeeeeeeeee, CHANGE IS COMING SOON, PIPO PAWAAAAAAAAAAAA wenyewe wanajua



Dk Bilal asema kusomesha bure ni ndoto za mchana Send to a friend Thursday, 07 October 2010 08:12 0diggsdigg

Salim Mohamed na Raisa Said, Tanga

MGOMBEA mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk Mohamed Bilal amewataka wananchi wa Mkoa wa Tanga kuwapuuza wapinzani kwa wanasema kwamba wakiingia madarakani wataoa huduma ya elimu na afya bure kwa kuwa mpango huo ni sawa na ndoto za mchana.

Dk Bilal aliyasema hayo jana katika mkutano wa kampeni wa chama chake uliofanyika katika uwanja wa Tangamano pamoja na mambo mengine alisema wananchi wa Tanga wakiwapeleka madarakani wataiboresha huduma ya usafiri wa Reli.


'Ndugu zangu wa Tanga kila siku nawasikia wapinzani wanakuja kwenu kuwaomba kura na kuwaahidi eti elimu na afya itakuwa bure hayo si ya kweli wameishiwa sera ndio maana kila siku wanasema hayo hayo," alisema Dk Bilal.

Dk Bilal alisema watajenga viwanda ili kuumarisha uchumi wa Taifa na kuwapa ajira vijana na bidhaa hizi zitasafirishwa kwenda nje ya nchi kupitia bandari ya Tanga na serikali itaongeza mapato yake na kutekeleza ahadi zake.

Alisema CCM imetekeleza ilani yake ya uchaguzi tangu uchaguzi wa kwanza wa mwaka 1995 na kuweza kufikia asilimia 98 na bado asilimia 2 tu ili iweze kufikia malengo yake na kuwataka wananchi wa mkoa huo kuwapa kura nyingi siku ya uchaguzi.

Alisema chama cha CCM kina uzoefu wa kuiongoza nchi na kudai kuwa ndio maana wanaomba tena wachaguliwe.
Source mwananchi (Dk Bilal asema kusomesha bure ni ndoto za mchana)
 
Nimemuona sehemu eti amehudhuria maziko huko Muheza yaani wanapotaka kura bwana wanajishusha kweli ngoja wapate hata huo mkusanyiko wa msiba ungeweza kutawanywa watu wakamsikilize makamu wa Rais
 
Back
Top Bottom