Ahsanteni sana Marando, Prof. Safari kwa kutuonyesha undani wa Chadema

Na watu hawajui, JF sio mahala pa kuleta makala ndefu utadhani hotuba ya bajeti ya serikali..hapa ni sehemu ya kuleta hoja iliyochambuliwa na kufupishwa ili ipatiwe nyama na wachangiaji. Sasa huyu kilaza kaleta kurasa saba za gazeti la uhuru hapa.
 
Issue inayokandia CDM nikisoma naishia kucheka tu manake inapigwa na kupingwa hadi raha..... Jamani hebu tuwe wasikivu kwa kila hoja sio kusifia tu mazuri kama kua mabaya yarekebishwe... Japo Mtoa mada ni noma manake kaandika Mambo mengi sana hata mie nimesikia kuchoka mapema time za kutumia Internet isije ikaishia kwa hoja moja tu kuna vitu vingi vya kuperuzi......
 
Ungeweka kama ile speech ya Mulugo kwa Summary " ai willi stati wisi indrodaktioni, mein bode end theni i willi konkuludi". Unasema yale yale ya mwaka 2010, lete jambo jipya basi. Sijui kama hata CCM wenzio wataisoma mpaka mwisho
 
Issue inayokandia CDM nikisoma naishia kucheka tu manake inapigwa na kupingwa hadi raha..... Jamani hebu tuwe wasikivu kwa kila hoja sio kusifia tu mazuri kama kua mabaya yarekebishwe... Japo Mtoa mada ni noma manake kaandika Mambo mengi sana hata mie nimesikia kuchoka mapema time za kutumia Internet isije ikaishia kwa hoja moja tu kuna vitu vingi vya kuperuzi......
Unapoteza muda wako tu,kuna hoja gani hapo? Akili ndogo ni kushambulia majina tu basi, au na wewe una akili ndogo Mkuu? Kama una muda wa kutosha soma mpaka mwisho si ndio matumizi ya mtandao, ukiishiwa vocha ongeza nyingine ebo!!!
 
Hii ni sredi au tredi? Kwanza cheo chako hakifanani na ulichoandika hata kidogo ndio maana chama chenu kinakosa mvuto kwasababu ya vihiyo kama wewe wenye vichwa vilivyojaa siasa za majitaka. Hapa tunategemea great minds na si big heads. Masikini CCM yetu ndo inazama.....!
 
SIKU moja baada ya Jeshi la Polisi Tanzania kuyasambaratisha maandamano ya kutaka kushinikiza kuachiliwa huru kwa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda na wafuasi wake wanaokabiliwa na kesi mahakamani, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kiliongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kuunga mkono udini, vurugu na uhalifu mwingine.

Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho, Profesa Abdallah Safari na Mabere Marando, walidai kuwa serikali imeshindwa kushughulikia kwa miongo mingi madai ya waislamu, hatua iliyochochea vurugu katika miji ya Zanzibar na Dar es Salaam!

Marando kwa mfano alisema serikali imewahi kuzua kuwa chama cha Civic United Front (CUF) ni cha kiislamu, na sasa inaeneza propaganda kwamba Chadema nayo ni ya wakristo hususan wakatoliki.

Wakizuungumza kwa kupokezana kama walivyonukuliwa na baadhi ya magazeti, Marando na Safari waliilaumu serikali kwa kutuma polisi kuzima maandamano na kuwakamata watu wanaokimbia ili kukwepa wasitiwe mbaroni.

Baadhi ya malalamiko waliyodai yanapuuzwa na serikali ni kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi Tanzania Bara, Tanzania kujiunga na Umoja wa Nchi za Kiislamu Duniani (OIC) na kushinikiza kipengele cha dini katika sensa ya watu na makazi.

Wakizungumzia kutoweka kwa Kiongozi wa Jumuiya ya Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Uamsho) ambaye hatimaye alipochoka kujificha akajitoa mwenyewe mafichoni, Sheikh Faridi Hadi Ahmed, viongozi hao waandamizi wa Chadema waliishangaa serikali eti kwa kutojua alikokwenda!

“Inakuwaje serikali ijidanganye kuwa haijui alipo na kusababisha vurugu, uchomaji moto na kuharibu mali na hata kifo cha polisi Saidi Abdulrahmani aliyepigwa mapanga kuhusiana na tukio hilo? Alihoji Marando, ‘shushushu’ wa zamani wa Idara ya Usalama wa Taifa ambaye hivi leo ni Mkuu wa Kitengo cha Intelijensia cha Chadema.

Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nafuatilia kauli na matendo mbalimbali yanayofanywa na viongozi wa Chadema wakiongozwa na gwiji la siasa za ghiliba, uzushi, uongo, uchochezi na kila aina ya vurugu na uvunjaji wa sheria kwa makusudi lililopewa kazi ya kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho baada ya kushindwa useja wa Kanisa Katoliki, Dk. Wilbroad Slaa.

Wapambe linaowaongoza katika kufanya hivyo ni pamoja na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Taifa ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo jijini Dar es Salaam, John Mnyika; Mjumbe wa Kamati Kuu na Mbunge wa zamani wa Arusha Mjini, Godbless Lema na ‘vichwa maji’ wengine wa kisiasa kama Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Nyamagana mkoani Mwanza, Ezekiel Wenje na kadhalika.

Naweza kusema bila ya kumung’unya maneno kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema kwa Tanzania Bara ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ndiye kiongozi mwandamizi peke yake aliyejaliwa angalau kidogo tone la hekima, busara, adabu na siasa za kistaarabu.

Anazungumza kwa utafiti, tafakuri, nidhamu na hatetei uongo wala kukumbatia uzushi eti ili mradi tu unakinufaisha chama chake hata kama ni hatari kubwa kwa Watanzania wengine.

Ukimwondoa Zitto peke yake, wote waliobaki wanapapasa kila kona ili kusaka mlango wa kuwatoa. Wanafanya kila aina ya siasa chafu ikiwemo uviziaji wa matukio bila kuangalia au kujali kitu chochote.

Ndiyo maana kila ‘wanachogusa’ wanadhania ‘mlango wa kuwatoa’ kisiasa iwe kwa ghiliba, uzushi, uongo, uchochezi, hadaa, umbeya ama uchonganishi na hatimaye sasa wanashabikia au kuchekelea mpaka uhuni, vurugu, wizi, uvunjaji wa sheria kwa makusudi na uvunjifu wa amani!

Sikutarajia hata kidogo kuwaona wanasheria wa siku nyingi akiwemo mpaka profesa, tena ni wanasiasa ambao ni Wajumbe wa Kamati Kuu ya chama chao wakishabikia hali hiyo badala ya kutumia midomo yao kuikaripia, kuisuta, kuikemea, kuilaani na sema vingine vyovyote ujuavyo.

Haiwezekani kwa viongozi wa juu kiasi kile katika chama kinachodai kutawala nchi mwaka 2015 wakawa kama zezeta wa kisiasa.

Haiwezekani wakaunga mkono uhuni, wizi ama uhalifu mwingine wowote unaofanywa na mtu yeyote bila ya kujali itikadi yake ya kisiasa, dini yake, kabila lake, familia yake, ukoo wake au eneo gani analotoka hapa nchini.

Haiwezekani mwanasiasa wa siku nyingi kama Marando aliyewahi hadi kuwa Mwenyekiti wa Taifa na Katibu Mkuu wa chama cha siasa hivi leo ashabikie uozo na vurugu za kijinga.

Haiwezekani eti kila kundi au mtu anapozuka tu asubuhi na kutaka chochote, wakati wowote na kwa namna yoyote ile basi serikali ikubali na kutekeleza matakwa yake yote, vilevile na bila kuangalia na hata kujali athari zake kwa taifa ama wananchi wengine.

Haiwezekani kwa mfano wakitokea wendawazimu wachache siku moja wakaamka asubuhi na bangi zao vichwani, wakafunga barabara kwa maandamano, wakachoma moto majengo na magari ya watu, kupora maduka na kufanya uhalifu mwingine washinikiza majambazi wote waliofungwa jela waachiliwe huru eti serikali isikilizwe matakwa yao na kuyatekeleza.

Haiwezekani hata siku moja kuwa likitokea kundi la watu au taasisi yoyote ikaleta madai ya kutaka serikali ifute dini zote za kigeni, iruhusu matambiko kwenye ofisi zake kama Ikulu, wizarani au kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya na gharama zote zilipwe na Halmashauri za Wilaya au Manispaa waliko kwa sababu ni sehemu ya ibada zao basi waruhusiwe.

Haiwezekani kwamba wakitokea watu wakataka kuwa mahakama za ngazi zote nchini ziwe pia na ofisi za maaskofu, wachungaji, mapadri, mapasta, wainjilisti, makatekista au viongozi wengine wa kikristu na gharama zote ziwe mikononi mwa serikali basi wasikilizwe na hasa madai yao hayo yakidumu kwa miongo mingi.

Haiwezekani eti wasiposikilizwa kwa miongo hiyo basi watafute kisingizio chochote cha kuingia barabarani na kuandamana, kufanya vurugu na kushinikiza serikali itekeleze kwa asilimia 100 matakwa yao yote.

Mfano uliotolewa wa madai “ya miongo mingi” ya waislamu ya kutaka Mahakama ya Kadhi (Tanzania Bara) hata Marando na Safari wanafahamu kuhusu undani na ukweli. Wanaelewa kuwa tayari chombo hicho kimeshaundwa, lakini wakorofi wachache wanaendelea kusema vinginevyo na kulazimisha mambo yaliyopo nje ya Katiba ya nchi hii.

Mahakama ya Kadhi ni taasisi inayowahusu waislamu na uislamu peke yake na si wananchi wote. Haihusiani kwa namna yoyote ile na kundi jingine lolote, hivyo haiwezekani iwe ni sehemu ya Mahakama Kuu ya Tanzania wala Mahakama ya Rufani.

Inatakiwa iwe taasisi isiyokuwa ya kiserikali na gharama zake zote zitolewe, zisimamiwe na kuratibu kwa kuzingatia sheria, misingi na taratibu za dini hiyo yenyewe na siyo serikali.

Ibara ya 3(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 Toleo la 2005 inayotumika sasa inasema: “Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, isiyokuwa na dini, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa” (mwisho wa kunukuu).

Hapa maneno “isiyokuwa na dini” yana maana kwamba haifungamani na imani yoyote ile ya kiroho, hivyo haiwezekani kuwa serikali isimamie ama kuendesha taasisi yoyote ile ya kidini isipokuwa watu wake, kila mmoja kwa imani yake anaruhusiwa kuabudu au kuamini dini yoyote.

Hiyo ndiyo ibara inayoharamisha Mahakama ya Kadhi kusimamiwa, kuendeshwa na hata kugharamiwa na serikali, badala yake kazi hizo zote zinapaswa zifanywe na waislamu kwa kuzingatia misingi na kanuni zinazohusu uislamu.

Aidha, ibara hiyohiyo ndiyo pia inayoharamisha kwa namna zote Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kujiunga na Umoja wa Nchi za Kiislamu Duniani (OIC). Ndiyo ileile iliyozuia na kuharamisha kuwepo na dodoso la dini katika sensa ya watu na makazi kutokana na sababu zilezile zinazozuia Mahakama ya Kadhi kusimamiwa, kuendeshwa na hata kugharamiwa na serikali.

Mtu ambaye anaingia mitaani kuandamana kwa vurugu, wizi, uhuni, uvunjaji wa sheria na kuhatarisha amani ya watu wengine akishinikiza kuvunjwa kwa katiba, kisha wakatokea wanasheria na kutetea ujinga huo hawawezi kueleweka vinginevyo ila ni ulevi wa kisiasa, kuchanganyikiwa kimtazamo ama udhaifu wa kufikiri na kupembua mambo ya msingi kwa nchi yao!

Kuhusu madai eti kwamba serikali imewahi kusema CUF ni chama cha kiislamu na halafu sasa inasema Chadema ni cha wakristo hususan wakatoliki pia nazo ni tuhuma za kughushi, kubuni na uongo.

Ni mkutano gani wa serikali ambako Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Waziri, Naibu Waziri, Mkuu wa Mkoa ama Mkuu wa Wilaya aliyasema maneno hayo na alikuwa nani na lini kama siyo uzushi, umbeya na uzandiki wao wenyewe midomoni mwao?

Kana kwamba haitoshi, nawashangaa Marando na Safari kuisingizia serikali eti kwamba ilisababisha kuzuka vurugu, uchomaji moto barabarani, wizi na uharibifu wa mali kwa kutojua alikokuwa Kiongozi wa Jumuiya ya Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Umasho), Sheikh Faridi Hadi Ahmed!

Hivi ni kazi ya vyombo vya dola kumlinda kila sekunde, dakika au saa ya uhai wake utadhani Rais, Makamu wa Rais au Waziri Mkuu? Kama anaondoka nyumbani kwake, anakwenda safari zake anapaswa aige serikali ili impe ulinzi au amuage mkewe na watoto wake?

Aidha, nashindwa kabisa kumwelewa mwanasheria Safari anapotaka eti mhalifu akikimbia asikamatwe. Hivi kama akivamiwa yeye, akafanyiwa ukatili wowote unaoitwa jinai, kisha mhalifu akakimbia hawezi kumkimbiza wala kupiga kelele zozote za kuomba msaada ili akamatwe eti kwa sababu amekimbia?

Kwa nini uprofesa wake wa sheria anataka kuufananisha na uprofesa wa mitishamba kama alionao Maji Marefu ama aliokuwa nao marehemu ‘Profesa’ Vulata?

Mbali na Safari, kwa nini pia Marando anataka ajidhalilishe kiasi kile utadhani mwanasheria wa maigizo au ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Deiwaka wa Makaburini?

Mwisho kabisa ni je; inakuwaje Chadema waunge mkono uhuni, vurugu, wizi na uvunjifu wa amani? Hawa ni kweli wanastahili kupewa madaraka ili walete serikali inayotetea wezi, wahuni, wachochezi huku wakichekelea umwagaji wa damu?

Nawaomba wananchi wote bila kujali itikadi za kisiasa kwamba kamwe wasiruhusu utawala ambao utawaacha wakichinjwa kama kuku wa kitoweo, kuchomewa nyumba zao, maduka yao, maghala yao, misikiti yao au makanisa yao; halafu mhalifu eti akishakimbia inakuwa marufuku kumkimbiza ama kumtia mbaroni.

Itakuwa marufuku kumkimbiza au kumkamata kibaka aliyepora mtaani, jambazi aliyevamia popote na kuvunja, kuiba na hata kufanya mauaji yoyote.

Huo ndio undani na ukweli wa Chadema uliobainishwa na Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho, Mabere Marando na Profesa Abdallah Safari na mimi nasema “ahsanteni sana”.

Mungu Ibariki Tanzania!

Mwandishi wa makala hii ni Katibu Msaidizi, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ya CCM. Anapatikana kwa Simu Na. 0659 220 220 na 0762 633 244

nivigumu kejenga hoja na hasira. hapo umefeli kabisa.
 
security guard

Mkuu kumbe hujawajua hawa CDM na hasa MABERE MARANDO, ni kwamba jambo lolote la kinafiki mbele ya Watanzania kupitia CDM huwa linaachiwa Mabere Marando na mfano mzuri ni hili la vurugu za waislamu na lingine ni lile lililohusu kauli ya MABERE huyo huyo kuwa CCM wamenunua nchini ISRAELI kifaa cha kuingilia mawasiliano ya simu za mkononi. Huyu siyo mwanasiasa wala Mwanasheria bali mpayukaji tu anayejidai kujua siasa za uongo kumbe feki tu huyu MJALUO.

Hivi Mwigulu na wenzake waliotumiana meseji kwa namba za Kina Mnyika bado hawajaenda mahakamani tuu?
 
Summarize this story!!!!! Hamna aliyekuwa anayaonea haya maswali kwenye mitihani ya kiingereza na kiswahili atusaidie summary?
 
SIKU moja baada ya Jeshi la Polisi Tanzania kuyasambaratisha maandamano ya kutaka kushinikiza kuachiliwa huru kwa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda na wafuasi wake wanaokabiliwa na kesi mahakamani, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kiliongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kuunga mkono udini, vurugu na uhalifu mwingine.

Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho, Profesa Abdallah Safari na Mabere Marando, walidai kuwa serikali imeshindwa kushughulikia kwa miongo mingi madai ya waislamu, hatua iliyochochea vurugu katika miji ya Zanzibar na Dar es Salaam!

Marando kwa mfano alisema serikali imewahi kuzua kuwa chama cha Civic United Front (CUF) ni cha kiislamu, na sasa inaeneza propaganda kwamba Chadema nayo ni ya wakristo hususan wakatoliki.

Wakizuungumza kwa kupokezana kama walivyonukuliwa na baadhi ya magazeti, Marando na Safari waliilaumu serikali kwa kutuma polisi kuzima maandamano na kuwakamata watu wanaokimbia ili kukwepa wasitiwe mbaroni.

Baadhi ya malalamiko waliyodai yanapuuzwa na serikali ni kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi Tanzania Bara, Tanzania kujiunga na Umoja wa Nchi za Kiislamu Duniani (OIC) na kushinikiza kipengele cha dini katika sensa ya watu na makazi.

Wakizungumzia kutoweka kwa Kiongozi wa Jumuiya ya Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Uamsho) ambaye hatimaye alipochoka kujificha akajitoa mwenyewe mafichoni, Sheikh Faridi Hadi Ahmed, viongozi hao waandamizi wa Chadema waliishangaa serikali eti kwa kutojua alikokwenda!

"Inakuwaje serikali ijidanganye kuwa haijui alipo na kusababisha vurugu, uchomaji moto na kuharibu mali na hata kifo cha polisi Saidi Abdulrahmani aliyepigwa mapanga kuhusiana na tukio hilo? Alihoji Marando, ‘shushushu' wa zamani wa Idara ya Usalama wa Taifa ambaye hivi leo ni Mkuu wa Kitengo cha Intelijensia cha Chadema.

Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nafuatilia kauli na matendo mbalimbali yanayofanywa na viongozi wa Chadema wakiongozwa na gwiji la siasa za ghiliba, uzushi, uongo, uchochezi na kila aina ya vurugu na uvunjaji wa sheria kwa makusudi lililopewa kazi ya kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho baada ya kushindwa useja wa Kanisa Katoliki, Dk. Wilbroad Slaa.

Wapambe linaowaongoza katika kufanya hivyo ni pamoja na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Taifa ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo jijini Dar es Salaam, John Mnyika; Mjumbe wa Kamati Kuu na Mbunge wa zamani wa Arusha Mjini, Godbless Lema na ‘vichwa maji' wengine wa kisiasa kama Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Nyamagana mkoani Mwanza, Ezekiel Wenje na kadhalika.

Naweza kusema bila ya kumung'unya maneno kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema kwa Tanzania Bara ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ndiye kiongozi mwandamizi peke yake aliyejaliwa angalau kidogo tone la hekima, busara, adabu na siasa za kistaarabu.

Anazungumza kwa utafiti, tafakuri, nidhamu na hatetei uongo wala kukumbatia uzushi eti ili mradi tu unakinufaisha chama chake hata kama ni hatari kubwa kwa Watanzania wengine.

Ukimwondoa Zitto peke yake, wote waliobaki wanapapasa kila kona ili kusaka mlango wa kuwatoa. Wanafanya kila aina ya siasa chafu ikiwemo uviziaji wa matukio bila kuangalia au kujali kitu chochote.

Ndiyo maana kila ‘wanachogusa' wanadhania ‘mlango wa kuwatoa' kisiasa iwe kwa ghiliba, uzushi, uongo, uchochezi, hadaa, umbeya ama uchonganishi na hatimaye sasa wanashabikia au kuchekelea mpaka uhuni, vurugu, wizi, uvunjaji wa sheria kwa makusudi na uvunjifu wa amani!

Sikutarajia hata kidogo kuwaona wanasheria wa siku nyingi akiwemo mpaka profesa, tena ni wanasiasa ambao ni Wajumbe wa Kamati Kuu ya chama chao wakishabikia hali hiyo badala ya kutumia midomo yao kuikaripia, kuisuta, kuikemea, kuilaani na sema vingine vyovyote ujuavyo.

Haiwezekani kwa viongozi wa juu kiasi kile katika chama kinachodai kutawala nchi mwaka 2015 wakawa kama zezeta wa kisiasa.

Haiwezekani wakaunga mkono uhuni, wizi ama uhalifu mwingine wowote unaofanywa na mtu yeyote bila ya kujali itikadi yake ya kisiasa, dini yake, kabila lake, familia yake, ukoo wake au eneo gani analotoka hapa nchini.

Haiwezekani mwanasiasa wa siku nyingi kama Marando aliyewahi hadi kuwa Mwenyekiti wa Taifa na Katibu Mkuu wa chama cha siasa hivi leo ashabikie uozo na vurugu za kijinga.

Haiwezekani eti kila kundi au mtu anapozuka tu asubuhi na kutaka chochote, wakati wowote na kwa namna yoyote ile basi serikali ikubali na kutekeleza matakwa yake yote, vilevile na bila kuangalia na hata kujali athari zake kwa taifa ama wananchi wengine.

Haiwezekani kwa mfano wakitokea wendawazimu wachache siku moja wakaamka asubuhi na bangi zao vichwani, wakafunga barabara kwa maandamano, wakachoma moto majengo na magari ya watu, kupora maduka na kufanya uhalifu mwingine washinikiza majambazi wote waliofungwa jela waachiliwe huru eti serikali isikilizwe matakwa yao na kuyatekeleza.

Haiwezekani hata siku moja kuwa likitokea kundi la watu au taasisi yoyote ikaleta madai ya kutaka serikali ifute dini zote za kigeni, iruhusu matambiko kwenye ofisi zake kama Ikulu, wizarani au kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya na gharama zote zilipwe na Halmashauri za Wilaya au Manispaa waliko kwa sababu ni sehemu ya ibada zao basi waruhusiwe.

Haiwezekani kwamba wakitokea watu wakataka kuwa mahakama za ngazi zote nchini ziwe pia na ofisi za maaskofu, wachungaji, mapadri, mapasta, wainjilisti, makatekista au viongozi wengine wa kikristu na gharama zote ziwe mikononi mwa serikali basi wasikilizwe na hasa madai yao hayo yakidumu kwa miongo mingi.

Haiwezekani eti wasiposikilizwa kwa miongo hiyo basi watafute kisingizio chochote cha kuingia barabarani na kuandamana, kufanya vurugu na kushinikiza serikali itekeleze kwa asilimia 100 matakwa yao yote.

Mfano uliotolewa wa madai "ya miongo mingi" ya waislamu ya kutaka Mahakama ya Kadhi (Tanzania Bara) hata Marando na Safari wanafahamu kuhusu undani na ukweli. Wanaelewa kuwa tayari chombo hicho kimeshaundwa, lakini wakorofi wachache wanaendelea kusema vinginevyo na kulazimisha mambo yaliyopo nje ya Katiba ya nchi hii.

Mahakama ya Kadhi ni taasisi inayowahusu waislamu na uislamu peke yake na si wananchi wote. Haihusiani kwa namna yoyote ile na kundi jingine lolote, hivyo haiwezekani iwe ni sehemu ya Mahakama Kuu ya Tanzania wala Mahakama ya Rufani.

Inatakiwa iwe taasisi isiyokuwa ya kiserikali na gharama zake zote zitolewe, zisimamiwe na kuratibu kwa kuzingatia sheria, misingi na taratibu za dini hiyo yenyewe na siyo serikali.

Ibara ya 3(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 Toleo la 2005 inayotumika sasa inasema: "Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, isiyokuwa na dini, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa" (mwisho wa kunukuu).

Hapa maneno "isiyokuwa na dini" yana maana kwamba haifungamani na imani yoyote ile ya kiroho, hivyo haiwezekani kuwa serikali isimamie ama kuendesha taasisi yoyote ile ya kidini isipokuwa watu wake, kila mmoja kwa imani yake anaruhusiwa kuabudu au kuamini dini yoyote.

Hiyo ndiyo ibara inayoharamisha Mahakama ya Kadhi kusimamiwa, kuendeshwa na hata kugharamiwa na serikali, badala yake kazi hizo zote zinapaswa zifanywe na waislamu kwa kuzingatia misingi na kanuni zinazohusu uislamu.

Aidha, ibara hiyohiyo ndiyo pia inayoharamisha kwa namna zote Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kujiunga na Umoja wa Nchi za Kiislamu Duniani (OIC). Ndiyo ileile iliyozuia na kuharamisha kuwepo na dodoso la dini katika sensa ya watu na makazi kutokana na sababu zilezile zinazozuia Mahakama ya Kadhi kusimamiwa, kuendeshwa na hata kugharamiwa na serikali.

Mtu ambaye anaingia mitaani kuandamana kwa vurugu, wizi, uhuni, uvunjaji wa sheria na kuhatarisha amani ya watu wengine akishinikiza kuvunjwa kwa katiba, kisha wakatokea wanasheria na kutetea ujinga huo hawawezi kueleweka vinginevyo ila ni ulevi wa kisiasa, kuchanganyikiwa kimtazamo ama udhaifu wa kufikiri na kupembua mambo ya msingi kwa nchi yao!

Kuhusu madai eti kwamba serikali imewahi kusema CUF ni chama cha kiislamu na halafu sasa inasema Chadema ni cha wakristo hususan wakatoliki pia nazo ni tuhuma za kughushi, kubuni na uongo.

Ni mkutano gani wa serikali ambako Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Waziri, Naibu Waziri, Mkuu wa Mkoa ama Mkuu wa Wilaya aliyasema maneno hayo na alikuwa nani na lini kama siyo uzushi, umbeya na uzandiki wao wenyewe midomoni mwao?

Kana kwamba haitoshi, nawashangaa Marando na Safari kuisingizia serikali eti kwamba ilisababisha kuzuka vurugu, uchomaji moto barabarani, wizi na uharibifu wa mali kwa kutojua alikokuwa Kiongozi wa Jumuiya ya Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Umasho), Sheikh Faridi Hadi Ahmed!

Hivi ni kazi ya vyombo vya dola kumlinda kila sekunde, dakika au saa ya uhai wake utadhani Rais, Makamu wa Rais au Waziri Mkuu? Kama anaondoka nyumbani kwake, anakwenda safari zake anapaswa aige serikali ili impe ulinzi au amuage mkewe na watoto wake?

Aidha, nashindwa kabisa kumwelewa mwanasheria Safari anapotaka eti mhalifu akikimbia asikamatwe. Hivi kama akivamiwa yeye, akafanyiwa ukatili wowote unaoitwa jinai, kisha mhalifu akakimbia hawezi kumkimbiza wala kupiga kelele zozote za kuomba msaada ili akamatwe eti kwa sababu amekimbia?

Kwa nini uprofesa wake wa sheria anataka kuufananisha na uprofesa wa mitishamba kama alionao Maji Marefu ama aliokuwa nao marehemu ‘Profesa' Vulata?

Mbali na Safari, kwa nini pia Marando anataka ajidhalilishe kiasi kile utadhani mwanasheria wa maigizo au ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Deiwaka wa Makaburini?

Mwisho kabisa ni je; inakuwaje Chadema waunge mkono uhuni, vurugu, wizi na uvunjifu wa amani? Hawa ni kweli wanastahili kupewa madaraka ili walete serikali inayotetea wezi, wahuni, wachochezi huku wakichekelea umwagaji wa damu?

Nawaomba wananchi wote bila kujali itikadi za kisiasa kwamba kamwe wasiruhusu utawala ambao utawaacha wakichinjwa kama kuku wa kitoweo, kuchomewa nyumba zao, maduka yao, maghala yao, misikiti yao au makanisa yao; halafu mhalifu eti akishakimbia inakuwa marufuku kumkimbiza ama kumtia mbaroni.

Itakuwa marufuku kumkimbiza au kumkamata kibaka aliyepora mtaani, jambazi aliyevamia popote na kuvunja, kuiba na hata kufanya mauaji yoyote.

Huo ndio undani na ukweli wa Chadema uliobainishwa na Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho, Mabere Marando na Profesa Abdallah Safari na mimi nasema "ahsanteni sana".

Mungu Ibariki Tanzania!

Mwandishi wa makala hii ni Katibu Msaidizi, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ya CCM. Anapatikana kwa Simu Na. 0659 220 220 na 0762 633 244

Jitahidi umalize matatizo ya ndani mwenu kwanza ,Mwenyekiti wenu yasije mkuta yale ya Thabo Mbeki, kisha ndo uje nje si unamuona Mamvi anavyowagalagaza ohhhhhooo cheo uchwara kinaondoka hicho
 
Mtatapatapa sana magamba! Mwandishi huyu mbumbumbu kweli kweli! Anadhani propaganda zilizopikwa na chama chake za udini ni lazima zitajwe na hao aliowataja hadharani. Kweli akili yako ndogo. Mlipoanzisha hizi propaganda hamkuiona hiyo hatari?
 
we ni mbwa tu huna kitu hapo kwa sababu huna mwelekeo kutokana na kuvimbiwa rushwa za chaguzi za madiwani nini ?
 
security guard

Mkuu kumbe hujawajua hawa CDM na hasa MABERE MARANDO, ni kwamba jambo lolote la kinafiki mbele ya Watanzania kupitia CDM huwa linaachiwa Mabere Marando na mfano mzuri ni hili la vurugu za waislamu na lingine ni lile lililohusu kauli ya MABERE huyo huyo kuwa CCM wamenunua nchini ISRAELI kifaa cha kuingilia mawasiliano ya simu za mkononi. Huyu siyo mwanasiasa wala Mwanasheria bali mpayukaji tu anayejidai kujua siasa za uongo kumbe feki tu huyu MJALUO.
Kama wanachokisema ni uongo au uzushi unafikiri ni kwa nini serikali haiwakamati?
 
hahahaha! magamba bwana ni taabu tupu. kampelekee mkeo asome hyo makala yako. hope is slip of tongue.
 
full of udini, ushabiki wa serikali , jazba, matusi, unafiki, uchochezi, dharau, na upotoshaji pia ndizo sifa nilizooona kwa haraka haraka kwenye thread hiii na mambo kama haya msituhusishe waislam wote si wote wapenda posho kama ndugu yangu mwandishi anavyofikiria kama yeye kaandika matusi yake humu mengi kumtukana slaa, mara marando kafanya kwa msukumo wa posho tu ndugu zangu wasomaji ni njaa tu ndio inasumbua watu mwisho wa summary
 
Notes taking imekushinda rudi darasani. Kwanini watu washindwe kukuelewa?

1) maneno mengiiiiiiiiiiiiiiii na
2) kutojua unachoandika.
 
SIKU moja baada ya Jeshi la Polisi Tanzania kuyasambaratisha maandamano ya kutaka kushinikiza kuachiliwa huru kwa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda na wafuasi wake wanaokabiliwa na kesi mahakamani, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kiliongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kuunga mkono udini, vurugu na uhalifu mwingine.

Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho, Profesa Abdallah Safari na Mabere Marando, walidai kuwa serikali imeshindwa kushughulikia kwa miongo mingi madai ya waislamu, hatua iliyochochea vurugu katika miji ya Zanzibar na Dar es Salaam!

Marando kwa mfano alisema serikali imewahi kuzua kuwa chama cha Civic United Front (CUF) ni cha kiislamu, na sasa inaeneza propaganda kwamba Chadema nayo ni ya wakristo hususan wakatoliki.

Wakizuungumza kwa kupokezana kama walivyonukuliwa na baadhi ya magazeti, Marando na Safari waliilaumu serikali kwa kutuma polisi kuzima maandamano na kuwakamata watu wanaokimbia ili kukwepa wasitiwe mbaroni.

Baadhi ya malalamiko waliyodai yanapuuzwa na serikali ni kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi Tanzania Bara, Tanzania kujiunga na Umoja wa Nchi za Kiislamu Duniani (OIC) na kushinikiza kipengele cha dini katika sensa ya watu na makazi.

Wakizungumzia kutoweka kwa Kiongozi wa Jumuiya ya Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Uamsho) ambaye hatimaye alipochoka kujificha akajitoa mwenyewe mafichoni, Sheikh Faridi Hadi Ahmed, viongozi hao waandamizi wa Chadema waliishangaa serikali eti kwa kutojua alikokwenda!

"Inakuwaje serikali ijidanganye kuwa haijui alipo na kusababisha vurugu, uchomaji moto na kuharibu mali na hata kifo cha polisi Saidi Abdulrahmani aliyepigwa mapanga kuhusiana na tukio hilo? Alihoji Marando, ‘shushushu' wa zamani wa Idara ya Usalama wa Taifa ambaye hivi leo ni Mkuu wa Kitengo cha Intelijensia cha Chadema.

Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nafuatilia kauli na matendo mbalimbali yanayofanywa na viongozi wa Chadema wakiongozwa na gwiji la siasa za ghiliba, uzushi, uongo, uchochezi na kila aina ya vurugu na uvunjaji wa sheria kwa makusudi lililopewa kazi ya kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho baada ya kushindwa useja wa Kanisa Katoliki, Dk. Wilbroad Slaa.

Wapambe linaowaongoza katika kufanya hivyo ni pamoja na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Taifa ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo jijini Dar es Salaam, John Mnyika; Mjumbe wa Kamati Kuu na Mbunge wa zamani wa Arusha Mjini, Godbless Lema na ‘vichwa maji' wengine wa kisiasa kama Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Nyamagana mkoani Mwanza, Ezekiel Wenje na kadhalika.

Naweza kusema bila ya kumung'unya maneno kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema kwa Tanzania Bara ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ndiye kiongozi mwandamizi peke yake aliyejaliwa angalau kidogo tone la hekima, busara, adabu na siasa za kistaarabu.

Anazungumza kwa utafiti, tafakuri, nidhamu na hatetei uongo wala kukumbatia uzushi eti ili mradi tu unakinufaisha chama chake hata kama ni hatari kubwa kwa Watanzania wengine.

Ukimwondoa Zitto peke yake, wote waliobaki wanapapasa kila kona ili kusaka mlango wa kuwatoa. Wanafanya kila aina ya siasa chafu ikiwemo uviziaji wa matukio bila kuangalia au kujali kitu chochote.

Ndiyo maana kila ‘wanachogusa' wanadhania ‘mlango wa kuwatoa' kisiasa iwe kwa ghiliba, uzushi, uongo, uchochezi, hadaa, umbeya ama uchonganishi na hatimaye sasa wanashabikia au kuchekelea mpaka uhuni, vurugu, wizi, uvunjaji wa sheria kwa makusudi na uvunjifu wa amani!

Sikutarajia hata kidogo kuwaona wanasheria wa siku nyingi akiwemo mpaka profesa, tena ni wanasiasa ambao ni Wajumbe wa Kamati Kuu ya chama chao wakishabikia hali hiyo badala ya kutumia midomo yao kuikaripia, kuisuta, kuikemea, kuilaani na sema vingine vyovyote ujuavyo.

Haiwezekani kwa viongozi wa juu kiasi kile katika chama kinachodai kutawala nchi mwaka 2015 wakawa kama zezeta wa kisiasa.

Haiwezekani wakaunga mkono uhuni, wizi ama uhalifu mwingine wowote unaofanywa na mtu yeyote bila ya kujali itikadi yake ya kisiasa, dini yake, kabila lake, familia yake, ukoo wake au eneo gani analotoka hapa nchini.

Haiwezekani mwanasiasa wa siku nyingi kama Marando aliyewahi hadi kuwa Mwenyekiti wa Taifa na Katibu Mkuu wa chama cha siasa hivi leo ashabikie uozo na vurugu za kijinga.

Haiwezekani eti kila kundi au mtu anapozuka tu asubuhi na kutaka chochote, wakati wowote na kwa namna yoyote ile basi serikali ikubali na kutekeleza matakwa yake yote, vilevile na bila kuangalia na hata kujali athari zake kwa taifa ama wananchi wengine.

Haiwezekani kwa mfano wakitokea wendawazimu wachache siku moja wakaamka asubuhi na bangi zao vichwani, wakafunga barabara kwa maandamano, wakachoma moto majengo na magari ya watu, kupora maduka na kufanya uhalifu mwingine washinikiza majambazi wote waliofungwa jela waachiliwe huru eti serikali isikilizwe matakwa yao na kuyatekeleza.

Haiwezekani hata siku moja kuwa likitokea kundi la watu au taasisi yoyote ikaleta madai ya kutaka serikali ifute dini zote za kigeni, iruhusu matambiko kwenye ofisi zake kama Ikulu, wizarani au kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya na gharama zote zilipwe na Halmashauri za Wilaya au Manispaa waliko kwa sababu ni sehemu ya ibada zao basi waruhusiwe.

Haiwezekani kwamba wakitokea watu wakataka kuwa mahakama za ngazi zote nchini ziwe pia na ofisi za maaskofu, wachungaji, mapadri, mapasta, wainjilisti, makatekista au viongozi wengine wa kikristu na gharama zote ziwe mikononi mwa serikali basi wasikilizwe na hasa madai yao hayo yakidumu kwa miongo mingi.

Haiwezekani eti wasiposikilizwa kwa miongo hiyo basi watafute kisingizio chochote cha kuingia barabarani na kuandamana, kufanya vurugu na kushinikiza serikali itekeleze kwa asilimia 100 matakwa yao yote.

Mfano uliotolewa wa madai "ya miongo mingi" ya waislamu ya kutaka Mahakama ya Kadhi (Tanzania Bara) hata Marando na Safari wanafahamu kuhusu undani na ukweli. Wanaelewa kuwa tayari chombo hicho kimeshaundwa, lakini wakorofi wachache wanaendelea kusema vinginevyo na kulazimisha mambo yaliyopo nje ya Katiba ya nchi hii.

Mahakama ya Kadhi ni taasisi inayowahusu waislamu na uislamu peke yake na si wananchi wote. Haihusiani kwa namna yoyote ile na kundi jingine lolote, hivyo haiwezekani iwe ni sehemu ya Mahakama Kuu ya Tanzania wala Mahakama ya Rufani.

Inatakiwa iwe taasisi isiyokuwa ya kiserikali na gharama zake zote zitolewe, zisimamiwe na kuratibu kwa kuzingatia sheria, misingi na taratibu za dini hiyo yenyewe na siyo serikali.

Ibara ya 3(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 Toleo la 2005 inayotumika sasa inasema: "Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, isiyokuwa na dini, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa" (mwisho wa kunukuu).

Hapa maneno "isiyokuwa na dini" yana maana kwamba haifungamani na imani yoyote ile ya kiroho, hivyo haiwezekani kuwa serikali isimamie ama kuendesha taasisi yoyote ile ya kidini isipokuwa watu wake, kila mmoja kwa imani yake anaruhusiwa kuabudu au kuamini dini yoyote.

Hiyo ndiyo ibara inayoharamisha Mahakama ya Kadhi kusimamiwa, kuendeshwa na hata kugharamiwa na serikali, badala yake kazi hizo zote zinapaswa zifanywe na waislamu kwa kuzingatia misingi na kanuni zinazohusu uislamu.

Aidha, ibara hiyohiyo ndiyo pia inayoharamisha kwa namna zote Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kujiunga na Umoja wa Nchi za Kiislamu Duniani (OIC). Ndiyo ileile iliyozuia na kuharamisha kuwepo na dodoso la dini katika sensa ya watu na makazi kutokana na sababu zilezile zinazozuia Mahakama ya Kadhi kusimamiwa, kuendeshwa na hata kugharamiwa na serikali.

Mtu ambaye anaingia mitaani kuandamana kwa vurugu, wizi, uhuni, uvunjaji wa sheria na kuhatarisha amani ya watu wengine akishinikiza kuvunjwa kwa katiba, kisha wakatokea wanasheria na kutetea ujinga huo hawawezi kueleweka vinginevyo ila ni ulevi wa kisiasa, kuchanganyikiwa kimtazamo ama udhaifu wa kufikiri na kupembua mambo ya msingi kwa nchi yao!

Kuhusu madai eti kwamba serikali imewahi kusema CUF ni chama cha kiislamu na halafu sasa inasema Chadema ni cha wakristo hususan wakatoliki pia nazo ni tuhuma za kughushi, kubuni na uongo.

Ni mkutano gani wa serikali ambako Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Waziri, Naibu Waziri, Mkuu wa Mkoa ama Mkuu wa Wilaya aliyasema maneno hayo na alikuwa nani na lini kama siyo uzushi, umbeya na uzandiki wao wenyewe midomoni mwao?

Kana kwamba haitoshi, nawashangaa Marando na Safari kuisingizia serikali eti kwamba ilisababisha kuzuka vurugu, uchomaji moto barabarani, wizi na uharibifu wa mali kwa kutojua alikokuwa Kiongozi wa Jumuiya ya Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Umasho), Sheikh Faridi Hadi Ahmed!

Hivi ni kazi ya vyombo vya dola kumlinda kila sekunde, dakika au saa ya uhai wake utadhani Rais, Makamu wa Rais au Waziri Mkuu? Kama anaondoka nyumbani kwake, anakwenda safari zake anapaswa aige serikali ili impe ulinzi au amuage mkewe na watoto wake?

Aidha, nashindwa kabisa kumwelewa mwanasheria Safari anapotaka eti mhalifu akikimbia asikamatwe. Hivi kama akivamiwa yeye, akafanyiwa ukatili wowote unaoitwa jinai, kisha mhalifu akakimbia hawezi kumkimbiza wala kupiga kelele zozote za kuomba msaada ili akamatwe eti kwa sababu amekimbia?

Kwa nini uprofesa wake wa sheria anataka kuufananisha na uprofesa wa mitishamba kama alionao Maji Marefu ama aliokuwa nao marehemu ‘Profesa' Vulata?

Mbali na Safari, kwa nini pia Marando anataka ajidhalilishe kiasi kile utadhani mwanasheria wa maigizo au ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Deiwaka wa Makaburini?

Mwisho kabisa ni je; inakuwaje Chadema waunge mkono uhuni, vurugu, wizi na uvunjifu wa amani? Hawa ni kweli wanastahili kupewa madaraka ili walete serikali inayotetea wezi, wahuni, wachochezi huku wakichekelea umwagaji wa damu?

Nawaomba wananchi wote bila kujali itikadi za kisiasa kwamba kamwe wasiruhusu utawala ambao utawaacha wakichinjwa kama kuku wa kitoweo, kuchomewa nyumba zao, maduka yao, maghala yao, misikiti yao au makanisa yao; halafu mhalifu eti akishakimbia inakuwa marufuku kumkimbiza ama kumtia mbaroni.

Itakuwa marufuku kumkimbiza au kumkamata kibaka aliyepora mtaani, jambazi aliyevamia popote na kuvunja, kuiba na hata kufanya mauaji yoyote.

Huo ndio undani na ukweli wa Chadema uliobainishwa na Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho, Mabere Marando na Profesa Abdallah Safari na mimi nasema "ahsanteni sana".

Mungu Ibariki Tanzania!

Mwandishi wa makala hii ni Katibu Msaidizi, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ya CCM. Anapatikana kwa Simu Na. 0659 220 220 na 0762 633 244

vipi ridhiwani amepona china?
 
Back
Top Bottom