Ahsanteni sana Marando, Prof. Safari kwa kutuonyesha undani wa Chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ahsanteni sana Marando, Prof. Safari kwa kutuonyesha undani wa Chadema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by security guard, Oct 29, 2012.

 1. s

  security guard JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 706
  Likes Received: 258
  Trophy Points: 80
  SIKU moja baada ya Jeshi la Polisi Tanzania kuyasambaratisha maandamano ya kutaka kushinikiza kuachiliwa huru kwa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda na wafuasi wake wanaokabiliwa na kesi mahakamani, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kiliongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kuunga mkono udini, vurugu na uhalifu mwingine.

  Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho, Profesa Abdallah Safari na Mabere Marando, walidai kuwa serikali imeshindwa kushughulikia kwa miongo mingi madai ya waislamu, hatua iliyochochea vurugu katika miji ya Zanzibar na Dar es Salaam!

  Marando kwa mfano alisema serikali imewahi kuzua kuwa chama cha Civic United Front (CUF) ni cha kiislamu, na sasa inaeneza propaganda kwamba Chadema nayo ni ya wakristo hususan wakatoliki.

  Wakizuungumza kwa kupokezana kama walivyonukuliwa na baadhi ya magazeti, Marando na Safari waliilaumu serikali kwa kutuma polisi kuzima maandamano na kuwakamata watu wanaokimbia ili kukwepa wasitiwe mbaroni.

  Baadhi ya malalamiko waliyodai yanapuuzwa na serikali ni kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi Tanzania Bara, Tanzania kujiunga na Umoja wa Nchi za Kiislamu Duniani (OIC) na kushinikiza kipengele cha dini katika sensa ya watu na makazi.

  Wakizungumzia kutoweka kwa Kiongozi wa Jumuiya ya Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Uamsho) ambaye hatimaye alipochoka kujificha akajitoa mwenyewe mafichoni, Sheikh Faridi Hadi Ahmed, viongozi hao waandamizi wa Chadema waliishangaa serikali eti kwa kutojua alikokwenda!

  "Inakuwaje serikali ijidanganye kuwa haijui alipo na kusababisha vurugu, uchomaji moto na kuharibu mali na hata kifo cha polisi Saidi Abdulrahmani aliyepigwa mapanga kuhusiana na tukio hilo? Alihoji Marando, ‘shushushu' wa zamani wa Idara ya Usalama wa Taifa ambaye hivi leo ni Mkuu wa Kitengo cha Intelijensia cha Chadema.

  Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nafuatilia kauli na matendo mbalimbali yanayofanywa na viongozi wa Chadema wakiongozwa na gwiji la siasa za ghiliba, uzushi, uongo, uchochezi na kila aina ya vurugu na uvunjaji wa sheria kwa makusudi lililopewa kazi ya kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho baada ya kushindwa useja wa Kanisa Katoliki, Dk. Wilbroad Slaa.

  Wapambe linaowaongoza katika kufanya hivyo ni pamoja na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Taifa ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo jijini Dar es Salaam, John Mnyika; Mjumbe wa Kamati Kuu na Mbunge wa zamani wa Arusha Mjini, Godbless Lema na ‘vichwa maji' wengine wa kisiasa kama Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Nyamagana mkoani Mwanza, Ezekiel Wenje na kadhalika.

  Naweza kusema bila ya kumung'unya maneno kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema kwa Tanzania Bara ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ndiye kiongozi mwandamizi peke yake aliyejaliwa angalau kidogo tone la hekima, busara, adabu na siasa za kistaarabu.

  Anazungumza kwa utafiti, tafakuri, nidhamu na hatetei uongo wala kukumbatia uzushi eti ili mradi tu unakinufaisha chama chake hata kama ni hatari kubwa kwa Watanzania wengine.

  Ukimwondoa Zitto peke yake, wote waliobaki wanapapasa kila kona ili kusaka mlango wa kuwatoa. Wanafanya kila aina ya siasa chafu ikiwemo uviziaji wa matukio bila kuangalia au kujali kitu chochote.

  Ndiyo maana kila ‘wanachogusa' wanadhania ‘mlango wa kuwatoa' kisiasa iwe kwa ghiliba, uzushi, uongo, uchochezi, hadaa, umbeya ama uchonganishi na hatimaye sasa wanashabikia au kuchekelea mpaka uhuni, vurugu, wizi, uvunjaji wa sheria kwa makusudi na uvunjifu wa amani!

  Sikutarajia hata kidogo kuwaona wanasheria wa siku nyingi akiwemo mpaka profesa, tena ni wanasiasa ambao ni Wajumbe wa Kamati Kuu ya chama chao wakishabikia hali hiyo badala ya kutumia midomo yao kuikaripia, kuisuta, kuikemea, kuilaani na sema vingine vyovyote ujuavyo.

  Haiwezekani kwa viongozi wa juu kiasi kile katika chama kinachodai kutawala nchi mwaka 2015 wakawa kama zezeta wa kisiasa.

  Haiwezekani wakaunga mkono uhuni, wizi ama uhalifu mwingine wowote unaofanywa na mtu yeyote bila ya kujali itikadi yake ya kisiasa, dini yake, kabila lake, familia yake, ukoo wake au eneo gani analotoka hapa nchini.

  Haiwezekani mwanasiasa wa siku nyingi kama Marando aliyewahi hadi kuwa Mwenyekiti wa Taifa na Katibu Mkuu wa chama cha siasa hivi leo ashabikie uozo na vurugu za kijinga.

  Haiwezekani eti kila kundi au mtu anapozuka tu asubuhi na kutaka chochote, wakati wowote na kwa namna yoyote ile basi serikali ikubali na kutekeleza matakwa yake yote, vilevile na bila kuangalia na hata kujali athari zake kwa taifa ama wananchi wengine.

  Haiwezekani kwa mfano wakitokea wendawazimu wachache siku moja wakaamka asubuhi na bangi zao vichwani, wakafunga barabara kwa maandamano, wakachoma moto majengo na magari ya watu, kupora maduka na kufanya uhalifu mwingine washinikiza majambazi wote waliofungwa jela waachiliwe huru eti serikali isikilizwe matakwa yao na kuyatekeleza.

  Haiwezekani hata siku moja kuwa likitokea kundi la watu au taasisi yoyote ikaleta madai ya kutaka serikali ifute dini zote za kigeni, iruhusu matambiko kwenye ofisi zake kama Ikulu, wizarani au kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya na gharama zote zilipwe na Halmashauri za Wilaya au Manispaa waliko kwa sababu ni sehemu ya ibada zao basi waruhusiwe.

  Haiwezekani kwamba wakitokea watu wakataka kuwa mahakama za ngazi zote nchini ziwe pia na ofisi za maaskofu, wachungaji, mapadri, mapasta, wainjilisti, makatekista au viongozi wengine wa kikristu na gharama zote ziwe mikononi mwa serikali basi wasikilizwe na hasa madai yao hayo yakidumu kwa miongo mingi.

  Haiwezekani eti wasiposikilizwa kwa miongo hiyo basi watafute kisingizio chochote cha kuingia barabarani na kuandamana, kufanya vurugu na kushinikiza serikali itekeleze kwa asilimia 100 matakwa yao yote.

  Mfano uliotolewa wa madai "ya miongo mingi" ya waislamu ya kutaka Mahakama ya Kadhi (Tanzania Bara) hata Marando na Safari wanafahamu kuhusu undani na ukweli. Wanaelewa kuwa tayari chombo hicho kimeshaundwa, lakini wakorofi wachache wanaendelea kusema vinginevyo na kulazimisha mambo yaliyopo nje ya Katiba ya nchi hii.

  Mahakama ya Kadhi ni taasisi inayowahusu waislamu na uislamu peke yake na si wananchi wote. Haihusiani kwa namna yoyote ile na kundi jingine lolote, hivyo haiwezekani iwe ni sehemu ya Mahakama Kuu ya Tanzania wala Mahakama ya Rufani.

  Inatakiwa iwe taasisi isiyokuwa ya kiserikali na gharama zake zote zitolewe, zisimamiwe na kuratibu kwa kuzingatia sheria, misingi na taratibu za dini hiyo yenyewe na siyo serikali.

  Ibara ya 3(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 Toleo la 2005 inayotumika sasa inasema: "Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, isiyokuwa na dini, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa" (mwisho wa kunukuu).

  Hapa maneno "isiyokuwa na dini" yana maana kwamba haifungamani na imani yoyote ile ya kiroho, hivyo haiwezekani kuwa serikali isimamie ama kuendesha taasisi yoyote ile ya kidini isipokuwa watu wake, kila mmoja kwa imani yake anaruhusiwa kuabudu au kuamini dini yoyote.

  Hiyo ndiyo ibara inayoharamisha Mahakama ya Kadhi kusimamiwa, kuendeshwa na hata kugharamiwa na serikali, badala yake kazi hizo zote zinapaswa zifanywe na waislamu kwa kuzingatia misingi na kanuni zinazohusu uislamu.

  Aidha, ibara hiyohiyo ndiyo pia inayoharamisha kwa namna zote Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kujiunga na Umoja wa Nchi za Kiislamu Duniani (OIC). Ndiyo ileile iliyozuia na kuharamisha kuwepo na dodoso la dini katika sensa ya watu na makazi kutokana na sababu zilezile zinazozuia Mahakama ya Kadhi kusimamiwa, kuendeshwa na hata kugharamiwa na serikali.

  Mtu ambaye anaingia mitaani kuandamana kwa vurugu, wizi, uhuni, uvunjaji wa sheria na kuhatarisha amani ya watu wengine akishinikiza kuvunjwa kwa katiba, kisha wakatokea wanasheria na kutetea ujinga huo hawawezi kueleweka vinginevyo ila ni ulevi wa kisiasa, kuchanganyikiwa kimtazamo ama udhaifu wa kufikiri na kupembua mambo ya msingi kwa nchi yao!

  Kuhusu madai eti kwamba serikali imewahi kusema CUF ni chama cha kiislamu na halafu sasa inasema Chadema ni cha wakristo hususan wakatoliki pia nazo ni tuhuma za kughushi, kubuni na uongo.

  Ni mkutano gani wa serikali ambako Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Waziri, Naibu Waziri, Mkuu wa Mkoa ama Mkuu wa Wilaya aliyasema maneno hayo na alikuwa nani na lini kama siyo uzushi, umbeya na uzandiki wao wenyewe midomoni mwao?

  Kana kwamba haitoshi, nawashangaa Marando na Safari kuisingizia serikali eti kwamba ilisababisha kuzuka vurugu, uchomaji moto barabarani, wizi na uharibifu wa mali kwa kutojua alikokuwa Kiongozi wa Jumuiya ya Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Umasho), Sheikh Faridi Hadi Ahmed!

  Hivi ni kazi ya vyombo vya dola kumlinda kila sekunde, dakika au saa ya uhai wake utadhani Rais, Makamu wa Rais au Waziri Mkuu? Kama anaondoka nyumbani kwake, anakwenda safari zake anapaswa aige serikali ili impe ulinzi au amuage mkewe na watoto wake?

  Aidha, nashindwa kabisa kumwelewa mwanasheria Safari anapotaka eti mhalifu akikimbia asikamatwe. Hivi kama akivamiwa yeye, akafanyiwa ukatili wowote unaoitwa jinai, kisha mhalifu akakimbia hawezi kumkimbiza wala kupiga kelele zozote za kuomba msaada ili akamatwe eti kwa sababu amekimbia?

  Kwa nini uprofesa wake wa sheria anataka kuufananisha na uprofesa wa mitishamba kama alionao Maji Marefu ama aliokuwa nao marehemu ‘Profesa' Vulata?

  Mbali na Safari, kwa nini pia Marando anataka ajidhalilishe kiasi kile utadhani mwanasheria wa maigizo au ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Deiwaka wa Makaburini?

  Mwisho kabisa ni je; inakuwaje Chadema waunge mkono uhuni, vurugu, wizi na uvunjifu wa amani? Hawa ni kweli wanastahili kupewa madaraka ili walete serikali inayotetea wezi, wahuni, wachochezi huku wakichekelea umwagaji wa damu?

  Nawaomba wananchi wote bila kujali itikadi za kisiasa kwamba kamwe wasiruhusu utawala ambao utawaacha wakichinjwa kama kuku wa kitoweo, kuchomewa nyumba zao, maduka yao, maghala yao, misikiti yao au makanisa yao; halafu mhalifu eti akishakimbia inakuwa marufuku kumkimbiza ama kumtia mbaroni.

  Itakuwa marufuku kumkimbiza au kumkamata kibaka aliyepora mtaani, jambazi aliyevamia popote na kuvunja, kuiba na hata kufanya mauaji yoyote.

  Huo ndio undani na ukweli wa Chadema uliobainishwa na Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho, Mabere Marando na Profesa Abdallah Safari na mimi nasema "ahsanteni sana".

  Mungu Ibariki Tanzania!

  Mwandishi wa makala hii ni Katibu Msaidizi, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ya CCM. Anapatikana kwa Simu Na. 0659 220 220 na 0762 633 244
   
 2. REMSA

  REMSA JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,569
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Nimejaribu kusoma nimeishia njia ni nitarudi nikipata muda.
   
 3. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,800
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  naomba msamaria asome atoe summary mm nimeshindwa!
   
 4. A

  Asa79 JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2012
  Joined: Jul 19, 2012
  Messages: 591
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Napita tuuuuu.....watu wengine wanadhani hatuna kazi ya kufanya zaidi ya kusoma miandishi mpaka inakera
   
 5. Makala Jr

  Makala Jr JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 3,397
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Unaleta upuuzi mwingi kwenye masuala yanayohusu imani za watu,ni kweli serikali haina uwezo wa kutosha kugharamia uendeshaji wa mahakama ya kadhi,sasa inapata wapi uwezo wa kushirikiana na wakristo kuendesha hospitali na shule hata kama waislamu hawana shule na hospitali,sasa unadhani waislamu watasema kuna usawa?
   
 6. KIMAROO

  KIMAROO JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 18, 2012
  Messages: 446
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  cjamuelewa
   
 7. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,636
  Likes Received: 4,746
  Trophy Points: 280
  Ukikosa kazi ya kufanya unaweza hata kuchukua nguo yako nzima ukaifumua ili upate kazi ya kuishona. Magamba hawana kazi ya kufanya ndiyo maana wana zusha kila aina ya udaku ili mradi tu siku ziende wakingojea kuzikwa kwenye kaburi la siasa hapa bongo
   
 8. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2012
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  du kazi kweli kweli...hapa napita tu
   
 9. don-oba

  don-oba JF-Expert Member

  #9
  Oct 29, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 1,384
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  utasoma mwenyewe
   
 10. +255

  +255 JF-Expert Member

  #10
  Oct 29, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 1,909
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Wewe 0 kabisa, ka unaonashida kusoma maandishi humu JF unatafuta nini?
   
 11. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #11
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Loading.....
   
 12. O

  Omulangi JF-Expert Member

  #12
  Oct 29, 2012
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 1,026
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Ni vizuri pia kusikiliza critics wanasema nini kwa njia hiyo ni rahisi kusasahisha yasiyo sawa
   
 13. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #13
  Oct 29, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,578
  Likes Received: 1,675
  Trophy Points: 280
  Mwandishi wa makala hii ni Katibu Msaidizi, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ya CCM. Anapatikana kwa Simu Na. 0659 220 220 na 0762 633 244Na Charels Charles

  Yani huyu pamoja na kuwa wakimataifa haoni tatizo la RAISI kuteua MUFTI.
   
 14. Jallen

  Jallen JF-Expert Member

  #14
  Oct 29, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 497
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  hebu summarize kazi yako ili tuweze kusoma
   
 15. ligendayika

  ligendayika JF-Expert Member

  #15
  Oct 29, 2012
  Joined: Aug 31, 2012
  Messages: 1,175
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 145
  Too long.jaribu kufupisha angalau weka point kwanza.
   
 16. n

  ni_mtazamo_tu Senior Member

  #16
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 17, 2012
  Messages: 155
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyu mtu hayuko sawa msameheni inaweza ikawa ni stress za maisha au yale maisha bora kwa kila mtanzania yanamsumbua
   
 17. Access Denied

  Access Denied JF-Expert Member

  #17
  Oct 29, 2012
  Joined: Aug 10, 2012
  Messages: 640
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  Access Denied!
   
 18. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #18
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Nadhani mwandishi wa makala hii alibanwa na kinyesi akakosa choo ndio maana akaamua kujiharishia.
   
 19. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #19
  Oct 29, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  security guard

  Mkuu kumbe hujawajua hawa CDM na hasa MABERE MARANDO, ni kwamba jambo lolote la kinafiki mbele ya Watanzania kupitia CDM huwa linaachiwa Mabere Marando na mfano mzuri ni hili la vurugu za waislamu na lingine ni lile lililohusu kauli ya MABERE huyo huyo kuwa CCM wamenunua nchini ISRAELI kifaa cha kuingilia mawasiliano ya simu za mkononi. Huyu siyo mwanasiasa wala Mwanasheria bali mpayukaji tu anayejidai kujua siasa za uongo kumbe feki tu huyu MJALUO.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. mtwana

  mtwana JF-Expert Member

  #20
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 399
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Matapishi ya Mbwa.............
   
Loading...