Ahsanteni sana Marando, Prof. Safari kwa kutuonyesha undani wa Chadema

Hoja kubwa ya msingi niliyoisikia toka kwa Marando na Prof. Safari ni HAKI YA MTANZANIA KUPATIWA DHAMANA. Hakuna lingine. hawakuunga mkono uhuni, uharifu nk kama mtoa mada anavyojaribu kurembesha ! Kabla ya hukumu mtu yeyote nana hatia mbele ya sheria, mpaka inapothibitika, tena beyond reasonable doubt that some one is guilt ! Ningekuwa mimi ndiyo "Security guard" ningejitahidi sana kufupisha maneno na kubaki kwenye hoja ya msingi.
 
SIKU moja baada ya Jeshi la Polisi Tanzania kuyasambaratisha maandamano ya kutaka kushinikiza kuachiliwa huru kwa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda na wafuasi wake wanaokabiliwa na kesi mahakamani, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kiliongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kuunga mkono udini, vurugu na uhalifu mwingine.

Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho, Profesa Abdallah Safari na Mabere Marando, walidai kuwa serikali imeshindwa kushughulikia kwa miongo mingi madai ya waislamu, hatua iliyochochea vurugu katika miji ya Zanzibar na Dar es Salaam!

Marando kwa mfano alisema serikali imewahi kuzua kuwa chama cha Civic United Front (CUF) ni cha kiislamu, na sasa inaeneza propaganda kwamba Chadema nayo ni ya wakristo hususan wakatoliki.

Wakizuungumza kwa kupokezana kama walivyonukuliwa na baadhi ya magazeti, Marando na Safari waliilaumu serikali kwa kutuma polisi kuzima maandamano na kuwakamata watu wanaokimbia ili kukwepa wasitiwe mbaroni.

Baadhi ya malalamiko waliyodai yanapuuzwa na serikali ni kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi Tanzania Bara, Tanzania kujiunga na Umoja wa Nchi za Kiislamu Duniani (OIC) na kushinikiza kipengele cha dini katika sensa ya watu na makazi.

Wakizungumzia kutoweka kwa Kiongozi wa Jumuiya ya Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Uamsho) ambaye hatimaye alipochoka kujificha akajitoa mwenyewe mafichoni, Sheikh Faridi Hadi Ahmed, viongozi hao waandamizi wa Chadema waliishangaa serikali eti kwa kutojua alikokwenda!

"Inakuwaje serikali ijidanganye kuwa haijui alipo na kusababisha vurugu, uchomaji moto na kuharibu mali na hata kifo cha polisi Saidi Abdulrahmani aliyepigwa mapanga kuhusiana na tukio hilo? Alihoji Marando, ‘shushushu' wa zamani wa Idara ya Usalama wa Taifa ambaye hivi leo ni Mkuu wa Kitengo cha Intelijensia cha Chadema.

Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nafuatilia kauli na matendo mbalimbali yanayofanywa na viongozi wa Chadema wakiongozwa na gwiji la siasa za ghiliba, uzushi, uongo, uchochezi na kila aina ya vurugu na uvunjaji wa sheria kwa makusudi lililopewa kazi ya kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho baada ya kushindwa useja wa Kanisa Katoliki, Dk. Wilbroad Slaa.

Wapambe linaowaongoza katika kufanya hivyo ni pamoja na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Taifa ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo jijini Dar es Salaam, John Mnyika; Mjumbe wa Kamati Kuu na Mbunge wa zamani wa Arusha Mjini, Godbless Lema na ‘vichwa maji' wengine wa kisiasa kama Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Nyamagana mkoani Mwanza, Ezekiel Wenje na kadhalika.

Naweza kusema bila ya kumung'unya maneno kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema kwa Tanzania Bara ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ndiye kiongozi mwandamizi peke yake aliyejaliwa angalau kidogo tone la hekima, busara, adabu na siasa za kistaarabu.

Anazungumza kwa utafiti, tafakuri, nidhamu na hatetei uongo wala kukumbatia uzushi eti ili mradi tu unakinufaisha chama chake hata kama ni hatari kubwa kwa Watanzania wengine.

Ukimwondoa Zitto peke yake, wote waliobaki wanapapasa kila kona ili kusaka mlango wa kuwatoa. Wanafanya kila aina ya siasa chafu ikiwemo uviziaji wa matukio bila kuangalia au kujali kitu chochote.

Ndiyo maana kila ‘wanachogusa' wanadhania ‘mlango wa kuwatoa' kisiasa iwe kwa ghiliba, uzushi, uongo, uchochezi, hadaa, umbeya ama uchonganishi na hatimaye sasa wanashabikia au kuchekelea mpaka uhuni, vurugu, wizi, uvunjaji wa sheria kwa makusudi na uvunjifu wa amani!

Sikutarajia hata kidogo kuwaona wanasheria wa siku nyingi akiwemo mpaka profesa, tena ni wanasiasa ambao ni Wajumbe wa Kamati Kuu ya chama chao wakishabikia hali hiyo badala ya kutumia midomo yao kuikaripia, kuisuta, kuikemea, kuilaani na sema vingine vyovyote ujuavyo.

Haiwezekani kwa viongozi wa juu kiasi kile katika chama kinachodai kutawala nchi mwaka 2015 wakawa kama zezeta wa kisiasa.

Haiwezekani wakaunga mkono uhuni, wizi ama uhalifu mwingine wowote unaofanywa na mtu yeyote bila ya kujali itikadi yake ya kisiasa, dini yake, kabila lake, familia yake, ukoo wake au eneo gani analotoka hapa nchini.

Haiwezekani mwanasiasa wa siku nyingi kama Marando aliyewahi hadi kuwa Mwenyekiti wa Taifa na Katibu Mkuu wa chama cha siasa hivi leo ashabikie uozo na vurugu za kijinga.

Haiwezekani eti kila kundi au mtu anapozuka tu asubuhi na kutaka chochote, wakati wowote na kwa namna yoyote ile basi serikali ikubali na kutekeleza matakwa yake yote, vilevile na bila kuangalia na hata kujali athari zake kwa taifa ama wananchi wengine.

Haiwezekani kwa mfano wakitokea wendawazimu wachache siku moja wakaamka asubuhi na bangi zao vichwani, wakafunga barabara kwa maandamano, wakachoma moto majengo na magari ya watu, kupora maduka na kufanya uhalifu mwingine washinikiza majambazi wote waliofungwa jela waachiliwe huru eti serikali isikilizwe matakwa yao na kuyatekeleza.

Haiwezekani hata siku moja kuwa likitokea kundi la watu au taasisi yoyote ikaleta madai ya kutaka serikali ifute dini zote za kigeni, iruhusu matambiko kwenye ofisi zake kama Ikulu, wizarani au kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya na gharama zote zilipwe na Halmashauri za Wilaya au Manispaa waliko kwa sababu ni sehemu ya ibada zao basi waruhusiwe.

Haiwezekani kwamba wakitokea watu wakataka kuwa mahakama za ngazi zote nchini ziwe pia na ofisi za maaskofu, wachungaji, mapadri, mapasta, wainjilisti, makatekista au viongozi wengine wa kikristu na gharama zote ziwe mikononi mwa serikali basi wasikilizwe na hasa madai yao hayo yakidumu kwa miongo mingi.

Haiwezekani eti wasiposikilizwa kwa miongo hiyo basi watafute kisingizio chochote cha kuingia barabarani na kuandamana, kufanya vurugu na kushinikiza serikali itekeleze kwa asilimia 100 matakwa yao yote.

Mfano uliotolewa wa madai "ya miongo mingi" ya waislamu ya kutaka Mahakama ya Kadhi (Tanzania Bara) hata Marando na Safari wanafahamu kuhusu undani na ukweli. Wanaelewa kuwa tayari chombo hicho kimeshaundwa, lakini wakorofi wachache wanaendelea kusema vinginevyo na kulazimisha mambo yaliyopo nje ya Katiba ya nchi hii.

Mahakama ya Kadhi ni taasisi inayowahusu waislamu na uislamu peke yake na si wananchi wote. Haihusiani kwa namna yoyote ile na kundi jingine lolote, hivyo haiwezekani iwe ni sehemu ya Mahakama Kuu ya Tanzania wala Mahakama ya Rufani.

Inatakiwa iwe taasisi isiyokuwa ya kiserikali na gharama zake zote zitolewe, zisimamiwe na kuratibu kwa kuzingatia sheria, misingi na taratibu za dini hiyo yenyewe na siyo serikali.

Ibara ya 3(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 Toleo la 2005 inayotumika sasa inasema: "Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, isiyokuwa na dini, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa" (mwisho wa kunukuu).

Hapa maneno "isiyokuwa na dini" yana maana kwamba haifungamani na imani yoyote ile ya kiroho, hivyo haiwezekani kuwa serikali isimamie ama kuendesha taasisi yoyote ile ya kidini isipokuwa watu wake, kila mmoja kwa imani yake anaruhusiwa kuabudu au kuamini dini yoyote.

Hiyo ndiyo ibara inayoharamisha Mahakama ya Kadhi kusimamiwa, kuendeshwa na hata kugharamiwa na serikali, badala yake kazi hizo zote zinapaswa zifanywe na waislamu kwa kuzingatia misingi na kanuni zinazohusu uislamu.

Aidha, ibara hiyohiyo ndiyo pia inayoharamisha kwa namna zote Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kujiunga na Umoja wa Nchi za Kiislamu Duniani (OIC). Ndiyo ileile iliyozuia na kuharamisha kuwepo na dodoso la dini katika sensa ya watu na makazi kutokana na sababu zilezile zinazozuia Mahakama ya Kadhi kusimamiwa, kuendeshwa na hata kugharamiwa na serikali.

Mtu ambaye anaingia mitaani kuandamana kwa vurugu, wizi, uhuni, uvunjaji wa sheria na kuhatarisha amani ya watu wengine akishinikiza kuvunjwa kwa katiba, kisha wakatokea wanasheria na kutetea ujinga huo hawawezi kueleweka vinginevyo ila ni ulevi wa kisiasa, kuchanganyikiwa kimtazamo ama udhaifu wa kufikiri na kupembua mambo ya msingi kwa nchi yao!

Kuhusu madai eti kwamba serikali imewahi kusema CUF ni chama cha kiislamu na halafu sasa inasema Chadema ni cha wakristo hususan wakatoliki pia nazo ni tuhuma za kughushi, kubuni na uongo.

Ni mkutano gani wa serikali ambako Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Waziri, Naibu Waziri, Mkuu wa Mkoa ama Mkuu wa Wilaya aliyasema maneno hayo na alikuwa nani na lini kama siyo uzushi, umbeya na uzandiki wao wenyewe midomoni mwao?

Kana kwamba haitoshi, nawashangaa Marando na Safari kuisingizia serikali eti kwamba ilisababisha kuzuka vurugu, uchomaji moto barabarani, wizi na uharibifu wa mali kwa kutojua alikokuwa Kiongozi wa Jumuiya ya Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Umasho), Sheikh Faridi Hadi Ahmed!

Hivi ni kazi ya vyombo vya dola kumlinda kila sekunde, dakika au saa ya uhai wake utadhani Rais, Makamu wa Rais au Waziri Mkuu? Kama anaondoka nyumbani kwake, anakwenda safari zake anapaswa aige serikali ili impe ulinzi au amuage mkewe na watoto wake?

Aidha, nashindwa kabisa kumwelewa mwanasheria Safari anapotaka eti mhalifu akikimbia asikamatwe. Hivi kama akivamiwa yeye, akafanyiwa ukatili wowote unaoitwa jinai, kisha mhalifu akakimbia hawezi kumkimbiza wala kupiga kelele zozote za kuomba msaada ili akamatwe eti kwa sababu amekimbia?

Kwa nini uprofesa wake wa sheria anataka kuufananisha na uprofesa wa mitishamba kama alionao Maji Marefu ama aliokuwa nao marehemu ‘Profesa' Vulata?

Mbali na Safari, kwa nini pia Marando anataka ajidhalilishe kiasi kile utadhani mwanasheria wa maigizo au ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Deiwaka wa Makaburini?

Mwisho kabisa ni je; inakuwaje Chadema waunge mkono uhuni, vurugu, wizi na uvunjifu wa amani? Hawa ni kweli wanastahili kupewa madaraka ili walete serikali inayotetea wezi, wahuni, wachochezi huku wakichekelea umwagaji wa damu?

Nawaomba wananchi wote bila kujali itikadi za kisiasa kwamba kamwe wasiruhusu utawala ambao utawaacha wakichinjwa kama kuku wa kitoweo, kuchomewa nyumba zao, maduka yao, maghala yao, misikiti yao au makanisa yao; halafu mhalifu eti akishakimbia inakuwa marufuku kumkimbiza ama kumtia mbaroni.

Itakuwa marufuku kumkimbiza au kumkamata kibaka aliyepora mtaani, jambazi aliyevamia popote na kuvunja, kuiba na hata kufanya mauaji yoyote.

Huo ndio undani na ukweli wa Chadema uliobainishwa na Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho, Mabere Marando na Profesa Abdallah Safari na mimi nasema "ahsanteni sana".

Mungu Ibariki Tanzania!

Mwandishi wa makala hii ni Katibu Msaidizi, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ya CCM. Anapatikana kwa Simu Na. 0659 220 220 na 0762 633 244
........[/QUOTE]

Kila anayeanza kuusoma utumbo huu anaishia njiani, nina uhakika hakuna anayemaliza kusoma mafinyofinyo yako ambayo kimsingi ulipoteza muda mrefu bora hata ungetumia huo muda kwenda Hospitali ya Mwanayamala kusalimia wagonjwa!! unahangaishwa na mahaba ya chama, kitakuoa!!!
 
Umeongea vyema sana mkuu nimekuelewa na nakuombea kila la kheri, Chadema hawaitakii mema nchi hii.
 
Huyu naye anaujauzito wa mawazo atajifungua lakin tumuombeee MUNGU bado mimba ni kubwa mawazo yake yana utege
ulipataje hicho cheo maswala madogo yasiyo hitaji hata certificate unashindwa kuyajua pole sana ngoja CCM ianguke ndio labda utastuka
 
sawa tunakushukuru kwa maoni yako na chama chako kama sisi waislam ni wahuni ,washenz tunakushukuru tumejua sasa
ndio maana miaka 50 yote tumekandamizwa tunakutajia mafanikio katika chama chako muone kama mtashinda 2015
 
Dr slaa alipotaja list of shame pale mwembayanga Temeke kuhusu EPA, nyinyiem walisema kama wewe ni mzushi,mwongo,kakimbia useja na mambo mengi tu,lakini ukweli ulijulikana na wezi wachache walirudisha pesa za walipakodi ,hata hivyo bado wengine hawajarudisha kodi zetu.Tunakumbuka waislamu walivyotumiwa na nyinyiem kule Igunga,tunakumbuka Igp mstaafu alivyotumiwa na nyinyiem kushambuliwa CUF sakata la majambia.kwahiyo tunawajua ukiwa wewe na hao wenzako unavyotaka.Lakini mkumbuke kuwa watanzania wa leo wanajua mabaya na mazuri .CDM na viongozi wake tunawaamini sana.Nakuomba waeleze wenzako pesa na mali za walipa kodi zinatakiwa haraka na ni kama ifuatavyo:
1.pesa zote za EPA ikiwamo meremeta
2.pesa zilifichwa Uswis
3.Nyumba zetu za serkali mlizogawana
Pia mikataba ya madini imekuwa inawanufaisha vigogo wa nyinyiem na watoto wao ivunjwe la sivyo ya Gadaffi na watoto wake yanawajia.
Mwisho nakuambia uiacha CDM istawi kama inavyo mpendeza Mungu kwa ajiri ya ukombozi wa maskini na wanyonge katika nchi iliyojaa utajiri
 
Jamani hii makala ni safi, ingelifaa muijadili barabara, acheni ushabeki.Tumia weledi muijadili. ina uzuri wake. Yaelekea wengi waliochangia ni mashabiki kwelikweli kiasi cha kushindwa kukubali ukweli hata kama unauma.
 
Jamani hii makala ni safi, ingelifaa muijadili barabara, acheni ushabeki.Tumia weledi muijadili. ina uzuri wake. Yaelekea wengi waliochangia ni mashabiki kwelikweli kiasi cha kushindwa kukubali ukweli hata kama unauma.
 
yaani waliye andaa habari hii ungepiga hata makofi mkewe angefanya kazi ya maana sana kuliko kuleta ujinga kama huu
 
Back
Top Bottom