Ahmed Shabiby, Vedasto Mathayo matatani kwa uchakachuaji wa mafuta

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
127,903
244,474
Hii ni taarifa ya Ewura iliyonakiliwa kwenye gazeti la Mwananchi .

Kwamba vituo vya AHMED SHABIBY PETROL STATION cha Makole Dodoma na BUNDA FILLING STATION cha Bunda Mjini kinachomilikiwa Vedasto Mathayo vimebainika kuchakachua mafuta .

Ikumbukwe kwamba hawa ni wabunge wa Jamhuri ya Muungano kupitia chama kilekile cha siku nyingi CCM , hata kama ni wachangiaji wazuri wa chama lakini taarifa hii ya EWURA haiwezi kupita bila kujadiliwa .

Ni kwanini hawajajiuzulu mpaka muda huu , ni athari kiasi gani wamelisababishia taifa hili katika kipindi chote walichofanya huu uchakachuaji wao ?

kama hali ndio hii kuna kazi kubwa sana mbele ya safari.
 
ikiwa kama wabunge wetu ndio wanayafanya haya , hakika hii ni aibu kubwa sana .
Kinachofata utasikia ata mkuu Wa kaya naye ameanza ufisadi hilo usishangae maana ata Wa awamu ya nje nae ailanza ila watendaji wake watafanya ufisadi mpaka Na yeye akawa fisadi mkuu
 
Kama mnajidanganya hapa maovu na madhambi yataisha poleni sana.




Labda mpaka lowasa akiwa rais
 
Hii nchi bila katiba mpya tutasikia hizi habari mpaka tutazizoea kama mashahiri ya nyimbo za Diamond!
 
Hamna namna zaidi ya kuwasikiliza awa mapopo si nchi hii ya baba yao bhana bt ipo siku watachomwa moto tu#viva LowaSsa
 
Itakuwa ni "message sent" maana hawa ni baadhi ya wabunge waliokuwa wakitamba kuwa watapiga kampeni kuhakikisha Ewura inafutwa! Mgongano wa maslahi...
 
Tolea maelezo zaidi je uchakachuaji huo ni apo katika petrol station tu au katika biashara nzima ya mafuta
 
Back
Top Bottom