Ahadi hizi kweli wana-CCM wanazitekeleza?

Kichuchunge

JF-Expert Member
Dec 2, 2020
338
891

Hizi ni ahadi 10 za wana-CCM, ipi wanayoitekeleza kwa vitendo zaidi? Au ni kinyume chake?


1. Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja

2. Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote

3. Nitajitolea nafsi yangu kuondoa umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma.

4. Rushwa ni adui wa haki. Sitapokea wala kutoa rushwa.

5. Cheo ni dhamana. Sitakitumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida
yangu.

6. Nitajielimisha kwa kadiri ya uwezo wangu na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote.

7. Nitashirikiana na wenzangu wote kuijenga nchi yetu.

8. Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.

9. Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa CCM na raia mwema wa Tanzania na Afrika.

10. Nitakuwa mtiifu na mwaminifu kwa Rais wa Serikali ya Tanzania
 
Moderator headline ilipaswa kuwa tuambiane ukweli ahadi hizi wana CCM wanazitekeleza au ni kinyume chake?
 
Back
Top Bottom