Agnes Mkandya, DED Gairo ni nani?

Agnes Mkandya, DED Gairo ni nani?

Najilazimisha kuelewa maana ya hii thread lakini kichwa kinakataa sijui kwanini?!
 
Sijaona anaejadili mambo ya uchumi na maendeleo ,nini kifanyike Tanzania tusonge mbele...tunamjadili huyu dada lakini hatulengi jinsi gani afanye kazi
 
Kwa kifupi mleta uzi malengo yako hayajatimia. Yaani mtu msafi hata akiwekwa uwanjani week nzima atabaki kuwa msafi tu. Haya dada wa watu wala hakuna aliyemsemea ubaya maana hana ubaya. Haya mkaoge mlale
 
Mimi ndiye niliyemteua, na asipotekeleza majukumu yake nitampasua jipu, ninaposema kumpasua jipu nitampasua kwelikweli
Shikamoo!! Ni kweli wewe ndie mwenyewe au? Manake hawakawii kufungua a/c kama ile aliyoikana Mh. Makonda.
 
kwani shida iko wapi yey kuwa na nafasi hiyo
 
Mkome mbona walipokuwa wachaga mlikuwa hamsemi. Magufuli bhatolage bhenabha bhale Na kishimbe,


Hakuna mchaga aliyewahi kushika nafasi za uteuzi akawateua wachaga kwa wingi.
Hapajawahi hata kuwa na waziri mkuu mchaga hapa Tanzania.
Hata uwaziri tu ni wa kuhesabu.

Sasa hiyo zamu yao ilikua ipi?
Acheni ukabila?
Hii nchi ni ya watanzania wote na ndio maana Nyerere alikua hapendi haya makabila makubwa yashike Madaraka.
Mana hata wakati mwingine jambo likiwa sawa litaonekana kama ukabila.

Watanzania wataamua wenyewe kama kuna ukabila au hakuna kwenye teuzi.
Muda ndio utasema.
Na kwa sababu kuna Makabila 125 kabila moja halitaweza kamwe kuimiliki hii nchi peke yake.
Kodi wanatoa wote halafu kwenye nafasi zinapoishia hizo kodi ziishie kwenye kabila moja!!! Hiyo haitawezekana na haitakubalika kamwe.

Mpaka sasa naona kama mkuu wa nchi anafanya teuzi zake kwa mujibu wa katiba ya nchi. Sasa kama kuna watu wanataka ateue kwa ukabila eti ni zamu yao naona wanataka kumopotisha na kukiangusha chama cha mapinduzi kwani hii nchi ina makabila mengi sana na marais waliopita walijitahidi kuepuka hayo mambo.

Huwezi kusema kuwa kabila fulani ndilo linalolipa kodi kuliko wengine ili wao ndio waifaidi zaidi ya wengine.

Kama ni umaskini basi yapo Makabila mengine mengi sana maskini sana lakini ndio mtaji mkubwa wa kura za kuiweka CCM madarakani bila kujali nani anagombea.

Na haya maneno maneno yataondoka tu pale katiba itakapoondoa huu utaratibu wa rais kuteua watu kila sehemu.

Utaratibu uwekwe kwenye katiba kuwa kila nafasi za kisiasa ziwe ni za kugombea na nafasi za kitaalam watu watume maombi na nafasi zitangazwe watu washindane kwa taaluma na namna watakavyotekeleza malengo ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Kwa kweli mara nyingine kumtoa mtu fulani akawe mkuu wa wilaya au mkoa fulani ni kuwakosea watu wa mkoa huo haki kwa kuwa hawezi kuwa na nia ya thati ya kuwaletea maendeleo zaidi ya kujitafutia fursa kama kujimilikisha mashamba na viwanja na hatimaye kuhamishwa na kuacha migogoro ya ardhi.Bila shaka angekua mkazi na akagombea hiyo nafasi hangeweza kufanya ujinga wa kuangalia maslahi yake na yule aliyempa nafasi hiyo mezani.

Tubadili katiba vinginevyo tuache kulialia rais anapofanya uteuzi.
 
Akina Masawe hatuli nchi kwakuteuliwa, tunakula nchi kwa kutumia akili za kuzaliwa.... Sasahivi tupo ubia na ndugu zetu Wakinga tunataka inunua k, koo na sinza... Only Mrema is looking for uteuzi
Haya bhana tumewaachia kariakoo , sisi wazawa tumekimbilia kimanzichana na maneromango .
 
Mimi ndiye niliyemteua, na asipotekeleza majukumu yake nitampasua jipu, ninaposema kumpasua jipu nitampasua kwelikweli


Yaani wewe ni JPM...tuthibitishie, vinginevyo utakwenda na maji kwa kosa la impersonation....tehtehtehtehtehteh
 
Back
Top Bottom