Kama kuna mambo yananisikitisha ni kuongozwa na mtu mwenye uwezo mdogo wa kufikiri,asiyechagua hata maneno ya kutumia awapo bungeni mbaya zaidi pamoja na ukakasi wa elimu yake alivoitumia kuudanganya umma wa watz kisha kujikuta yumo bungeni!!!!! Najiuliza hivi bunge ninalolifahamu Mimi lina watu kama hawa?? Aina ya watu kama hawa je wako wangapi humo mjengoni! Siamini kuwa hawa ndio wanajadili maendeleo ya nchi yangu, wanatunga sheria zinazotuongoza na kupitisha miswada mbalix2 na mengineyo! Pamoja na yooooote ya udanganyifu hakuna chombo chochote kinachochunguza udanganyifu unaotajwa hasa wa kielimu na kama alitumia elimu kama kigezo cha kuchaguliwa! Si bunge,serikali,vyombo vya dola hakuna mwenye habari! Jibu lililoturidhisha wote ni kwamba wanaomsema eti wamempa umaarufu? Kwa nchi makini hasa uongozi wa sasa hatuhitaji watu kama hawa! Vyombo vyote makini vifuatilie udanganyifu huu na kwa viongozi wengine pia na kuchukua hatua!