Ageuza kituo cha yatima kuwa danguro

miss zomboko

miss zomboko

JF-Expert Member
2,685
2,000
Ukishangaa ya Musa utayaona ya firauni! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema kufuatia Mjerumani, Bernhard Bery Glaser, kukamatwa na Jeshi la Polisi nchini Uganda kwa tuhuma za kuwatumia kingono zaidi ya watoto 30, waliokuwa wakilelewa kwenye kituo alichokianzia cha Ssese Humanitarian Services & Bery’s place.

Kituo hicho kilichopo katika Kijiji cha Mwena, Kalangala nchini Uganda kilianzishwa kwa lengo la kuwasaidia watoto wa kike waliofiwa na wazazi wao, waliowahi kupitia vitendo vya unyanyasaji wa kingono na wale wanaoishi kwenye mazingira magumu wenye umri wa kati ya miaka mitatu hadi 22.

Kwa kipindi cha miaka zaidi ya kumi tangu kilipoanzishwa, kimekuwa kikiaminika kama sehemu salama ya watoto wa kike kuishi na kuzifukuzia ndoto zao za maisha kikiwa na wastani wa watoto wa kike 30.

Wasichana wengi waliowahi kubakwa, waliokuwa wakiishi kwenye mazingira magumu, waliowahi kutumika na waasi katika mapigano na waliofiwa na wazazi wao, wamekuwa wakiishi kwenye kituo hicho, wakilipiwa ada na kituo hicho pamoja na kupata mahitaji mengine muhimu kama chakula, mavazi na huduma za matibabu.

Hata hivyo, wasichokijua wengi ni kwamba kumbe ili kuendelea kuishi kituoni hapo na kufaidika na huduma zote zinazotolewa, Bernhard amekuwa akiwalazimisha wasichana hao kufanya naye ngono kadiri mwenyewe atakavyo.

Wale wanaoshindwa kukubaliana naye, wamekuwa wakifukuzwa kituoni hapo kimyakimya! Bernhard anatuhumiwa kufanya ngono na mabinti hao wadogo, wakati mwingine akilala nao watatu au wanne kwa pamoja chumbani kwake mkewe anapokuwa safarini. Baada ya kukamatwa na mabinti hao kuanza kuhojiwa, wametoa ushuhuda wa ajabu, uliomshangaza kila mtu.

“Huwa anatufanya kama wake zake, anachagua wa kulala nao chumbani kwake, na wote mnalala bila nguo na yeye akiwa hana nguo, anafanya mapenzi na sisi kwa zamu mpaka anapotosheka.

Kila siku anabadilisha wa kulala nao, hakuna ambaye hajawahi kufanya naye mapenzi hapa, tena siyo mara moja,” mmoja wa waathirika wa vitendo hivyo vya unyanyasaji, aliliambia Gazeti la The Independent.

Siri ilivyovuja Aliyefichua uovu huo ni mwanamama Asia Namusoke Mbajja, mwanzilishi wa Shirika la People In Need Agency (PINA). Mwanamama huyo anaeleza kwamba miaka miwili iliyopita, Glaser alimtafuta kwa lengo la kuanza kufanya naye kazi.

“Aliniambia kwamba umri wake umeenda sana na anahitaji mtu wa kusaidiana naye, niliona ni wazo zuri kama tunaunganisha juhudi zetu,” anasema Namusoke.

“Kwa hiyo ilibidi nifunge safari mpaka kwenye kituo chake, nikakutana naye. Wakati ananitembeza kwenye mazingira ya kituo hicho, nilibaini wasichana wote walikuwa wakilala kwenye bweni moja lakini kulikuwa na vyumba vingine vyenye vitanda, nikapatwa na wasiwasi lakini sikutaka kumuonesha chochote.

“Siku hiyo sikutaka kuondoka, nilitaka nipate muda wa kuzungumza na wasichana hao, kwa hiyo usiku nikaomba kulala nao. Ndipo hapo nilipoujua ukweli, wasichana hao walinililia kwamba wanaomba nifanye kitu kuwasaidia. Wakanieleza mchezo mzima wanaofanyiwa na mzungu huyo.

“Kwa kweli nilichoka sana na maelezo yao, kesho yake niliondoka na kwenda kutoa taarifa polisi, lakini cha ajabu, wala hawakuchukua uamuzi wowote. Sikukata tamaa, nilijaribu kuwasiliana na mamlaka zote zinazohusika lakini hakuna aliyekuwa tayari kunisaidia, nikaonekana eti namuonea wivu mtu anayeisaidia jamii.

“Nikaona njia pekee ni kutafuta watu waliopo mbali na eneo hilo, nako hali ikawa hivyohivyo, mpaka hivi karibuni nilipopata msaada kutoka kwa chama cha wanasheria wanawake wa Uganda ambao kwa kushirikiana na mimi pamoja na jeshi la polisi, mipango iliandaliwa na hatimaye kituo chake kikaenda kuvamiwa na askari na kukamatwa. Kamanda wa Polisi wa Kalanga, Willy Nkumbi amethibitisha kukamatwa kwa Glaser na mkewe, Ingrid Dilen.
 
Eng Kahigwa

Eng Kahigwa

JF-Expert Member
727
1,000

Dah! Huyu jamaa ana mapepo.
 
P

pye Chang shen

JF-Expert Member
5,226
2,000
Hayo ndio mibeberu inafanya kwa mgongo wa misaada fukuza wote
 
N

NAKWEDE

JF-Expert Member
27,995
2,000
Kumbe hata wazungu wanapenda hiyo kitu!!!
🥶🥶🥶🥶🥶
 
Nktlogistics

Nktlogistics

JF-Expert Member
1,785
2,000
...."Matatizo ni ya Jana , na Jana haya kutatuliwa".
 
Thread starter Similar threads Forum Replies Date
figganigga Uganda: Wafuasi wa Mgombea Ubunge Bobi wine watanza kituo cha polisi Ugandan News and Politics 1

Forum statistics

Threads
1,425,153

Messages
35,082,647

Members
538,214
Top Bottom