Rev. Kishoka,
Ukiona Mkandara amekaa kimya basi jua napata darasa safi sana. Kusema kweli wewe na Kitila mnanipa mavituz na kama msomaji ni lazima nipime pande zote kwa uzito wa hoja. Nadhani unaelewa fika mimi nimesimama upande gani lakini kuwa kwangu upande huu haina maana sintatazama upande wapili na hoja zake. Binafsi hulichukulia swala la mtazamo wa kisiasa kama vile dini, mathlan leo hii mimi nikiwa mkristu haina maana kabisa kuwa Uislaam ni dini ya Uongo na kukana hata kusikia mawaidha ya dini hiyo. Huo ni ujinga, na Upumbavu huwa pale unaposoma kisha ukataa vilevile kwa sababu tu neno hilo limesemwa na muislaam ama Kuran hata kama lina ukweli na fundisho.
Hivyo basi napokea hoja zote pamoja na kwamba dini yangu bado ni ile ile yaani mimi Mjamaa hadi kufa!...kama wasemavyo wenyewe - kuwa tulikunywa maji ya Uhuru!. Sasa wanapoupachika Ujamaa tafsiri yao huwa sina zaidi ya kuwatazama na kuwaachia imani yao, kwani haikatazwi hata siku moja Mkristu kuishi na Muislaam nchi moja maadam kila mmoja wetu anafuata ibada zake.
Nimefurahi sana kukusikia ukilichambua Azimio la Arusha na hasa Dira ya taifa ambayo marehemu baba wa Taifa alituachia, wakaja wachawi wakaivuruga na kuipachikia tafsiri kama ile imani ya nadharia isemayo Binadamu wote sawa walosema kina Martin Luther King. Mtu yeyote akitaka kuitafsiri anavyopenda basi haiwezi kuwa na mantiki hata kiidogo isipokuwa ni budi sisi waumini tuelewe yule msemaji alikuwa na maana gani na sio hiyo tunayojaribu kuitunga sisi. Hivyo basi napata darasa mkuu wangu mwageni manyanga!