Stories of Change - 2023 Competition

jayboy

Member
May 26, 2023
19
15
Afya ni sehemu ni sehemu ya maendeleo endelevu katika kuimarisha afya bora za watu ili kuwawezesha kufanya vizuri na kuinua uchumi wao na nchi kwa ujumla katika jamii mtu mwenye afya bora huwa na uwezo wakushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii zao na kuchagia katika ujenzi wa jamii bora,afya bora inaweza kuathiriwa na mabadiliko ya tabia ya nchi ,uchafuzi wa mazingira na mtindo wa maisha unaokiuka ulaji mbaya wa vyakula na mambo mengine katika jamii, hali hii inaweza kuchangia kuongezeka kwa gharama ya matibabu na kupungua uwezo wa watu kufanya kazi na kuchangia uchumi wa nchi yao.

Katika kukabiliana na changamoto hizi za afya ni muhimu serikali kuwekeza katka huduma za afya bora na kuzuia magonjwa kwa kutumia kinga na chanjo mbalimbali dhidi magonjwa Kama vile surua,polio,pepopunda,uviko-19,mabusha na matende.Hatua hizi zinaweza zinaweza kujumuisha kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama,kuboresha usafi wa mazingira na kupunguza kiwango cha uchafuzi wa mazharaka pia zinaweza.

Pia ni muhimu kuchukua hata za kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo yanaathiri afya za watu kupitia kuongezeka kwa joto,kusambaa kwa wadudu wanaosambaza magonjwa kupitia chanjo ili kuzuia kuenea kwa magonjwa kwenye idadi kubwa ya watu Huduma bora za afya na za mikono pia zinaweza kuzuia magonjwa kuenea kwa haraka Sana, kwa mfano uviko-19,kipindupindu,Eboala homa ya manjano na magonjwa mengine.Hata za kuzuia magonjwa zinapaswa kushirikisha jamii pamoja na kutoa elimu ya afya ili watu wawez kujilinda na kuzuia kuenea kwa magonjwa. Kuna umuhimu wa kuwahimiza watu kufuata miongozo ya afya Kama vile kunawa barakoa,kuvaa barakoa,kunywa maji yaliyo safi na salama pamoja na mlo kamili.

Afya ni hali ya kuwa sawa kimwili,kiakili ,mawazo na kijamii ambapo humfanya mtu kuwa na furaha katika mwili wake ,mwenye nguvu na imara,hivyo kushiriki kwa ufanisi katika kufanya kazi kwenye jamii hivyo kujenga uhusiano mwema Kati yake na watu wengine,afya no msingi mkuu wa maisha ya binadamu kwa sababu inahusisha mzunguko mzima wa masuala ya lishe,mazoezi, maji safi na salama, matibabu,kings dhidi ya magonjwa na sababu nyingine.

Afya ni haki ya binadamu na inapaswa kupewa kipaumbele katika mipango na maendeleo endelevu ya jamii.Maendeleo endelevu ni maendeleo yanayozingatia mahitaji ya kizazi cha sasa bila ya kuathiri mahitaji ya kizazi kijacho,maendeleo endelevu yanalenga kujenga jamii na uchumi ambao unahakikisha usawa wa kijamii ,rasilimali za kutosha na mazingira bora kwa ajili ya kizazi vijavyo,maendeleo endelevu pia yanahusisha kufanya maamuzi yatakayodumu kwa muda mrefu nayanaweza kuhimili mabadiliko ya kiuchumi, kimazinendelevukijamii.

Hivyo maendeleo endelevu nibpamoja na kuchangia ustawi wa jamii kupitia uwekezaji wa kiuchumi unaojali mazingira na utumiaji wa teknolojia endelevu,pia pamoja na kushirikisha wanawake ,watoto na watu wenye ulemavu na kuhakikisha kuwa wanafikiwa na maendeleo ya kijamii na kiuchumi, maendeleo endelevu yanaangalia namna ya kuweka misingi imara ya maendeleo ambayo itakuwa endelevu katika utoaji wa rasilimali sawa katika jamii na ukuzaji wa kiuchumi kwa maendeleo ya mmazingira.Hali hii inamaanisha kwamba maendeleo yanafanyika kwa kuzingatia malengo ya maendeleo endelevu yaani "The sustainable Development Goals", Malengo haya yanajumuisha mambo Kama vile kupunguza umaskini,kuboresha afya na elimu,kuhakikisha usawa wa kijinsia ,kusaidia ukuaji wa uchumi endelevu na kuhifadhi mazingira kwa ajili ya kizazi vijavyo kwa lengo la kuongeza juhudi za pamoja za serikali, sekta binafsi, mashirika ya kiraia na kijamii ili kufikia malengo haya ya maendeleo.

Kuna mbinu mbalimbali za kuongeza uwajibikaji na utawala bora katika afya katika kuchochea maendeleo endelevu kwenye jamii Kama ifuatavyo:-

(a)Kusaidia jamii katika kutoa elimu dhidi ya kijikinga na magonjwa; kupitia wizara ya afya na ustawi wa jamii maendeleo na watoto inaweza kunguza mlipuka wa magonjwa nyemelezi katika jamii kupitia kuelimisha na kuwa habarisha wananchi kutokana na magonjwa habari Kama vile uviko-19,kisukari,saratani,UKIMWI, na magonjwa mengine,kupitia vyombo vya habari Kama vile redio,televisheni na magazeti,majarida,vipeperushi,mabango na hata pia mitandao ya kijamii Kama vile whatasapp.twitter, Instagram na YouTube kunaweza sana kusaidia kufikisha elimu kwa wanajamii katika kujikinga na maradhi mbalimbali ,hivyo afya zao kuimarika zaidi ,haya ni matokea ya kuwa na utawala bora na uwajibikaji katika jamii katika kuimarisha sekta ya afya nchini ili kufikia maendeleo endelevu hapo baadae.

(b) Kuajiri watumishi wa maendeleo ya jamii ili kusaidia madaktari na waaguzi katika kutoa kutoa huduma za ushauri wa kiafya kwa watu wenye matatizo ya kiakili ,msongo wa mawazo,waathirika wa madawa ya kulevya na pombe,wataalamu mbalimbali wa afya wamekuwa wakipata tabu Sana katika kutoa ushauri kwa watu wenye matatizo Kama haya ,hivyo basi baadhi yao kuchukua uwamuzi mgumu wa kutaka kujiua hali ambayo inapunguza rasilimali watu muhimu nchini katika kuongeza pato la nchi kwa matokeo ya maendeleo endelevu hapo baadae.Hivyo basi serikali naona budi kuajiri watu wa maendeleo ya jamii ili kuhudumu katika ngazi ya jamii na pia kutatua matatizo mbalimbali ya kiafya kupitia ushauri mzuri wa kitaalamu.

(c)kuboresha huduma ya bima ya afya katika upande wa malipo kutumia mfumo wa vocha au kifurushi;katika kukabiliana na changamoto za kugharamia huduma za kiafya nivyema serikali kuboresha mfumo wa bima za afya kupitia mfumo wa malipo ya vocha na vifurushi ili kuwasaidia wananchi wa hali za nchini kuweza kumudu gharama za matibabu nchini.

(d)kuajiri madaktari bingwa nchini ili kupunguza gharama za kutibiwa nje;pia serikali inapaswa kuajiri madaktari bingwa wa maradhi ya moyo,ini,mifupa,na misuli katika hospitali za rufaa na wilaya ili kusaidia wananchi wanaosumbuliwa na matatizo Kama haya ambao wanalamika kwenda nje kutafuta huduma za matibabu katika nchi Kama vile India,Marekani,Uturuki na nyingine baadhi ya watu wasioweza kumudu huduma hivi wanafariki kila siku hali ambayo inasababisha kupungua kwa rasilimali watu muhimu ambao ni wasimamizi wakubwa wa maendeleo endelevu.

(e)Kuvutia wawekezaji katika sekta ya afya kupunguza shida ya madawa na vifaa tiba hospitalini;katika kuunga mkono sekta ya afya nchini ,wizara ya biashara na uwekezaji nchini inatakiwa kuandaa mazingira mazuri ya uwekezaji kwa kutenga maeneo ya kutosha kwa ajilinya uwekezaji, kupunguza muda wa kufitilia vibali vya uwekezaji nchini ,kupitia upya Sera,masharti ya mikataba kati ya wizara na wawekaji hapa nchini ili kusaidia jitihada za serikali katika kukabiliana na shida ya kuigiza madawa kutoka nchi za nje ili kutibu afya za watu wake,kwa kufanya hivyo serikali itapunguza mzigo mkubwa wa kushughulikia upatikanaji wa madawa katika hospitali zote zilizopo nchini.

(f)kujenga hospitali za watoto na wanawake ili kusogeza karibu huduma ya haraka na ili kuokoa vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga;serikali inapaswa kushirikiana na wadau mbalimbali wa kiafya katika kukabiliana na changamoto ya vifo vya watoto wachanga na wa mama wajawazito katika kila mkoa nchini ili kupelela huduma za karibu kwa watoto wachanga na wamama wajawazito katika siku za karibuni kumekuwa na ongezeka upya la vifo vya kinamama na watoto wachanga hususani katika maeneo ya vijijini ambapo hudama za afya Sana ukilinganisha na miji hivyo basi uhakika wa maisha wa kuishi kwa watoto wanaozaliwa umekuwa mdogo na kushindwa kushiriki katika kuleta mabadiliko mbalimbali katika kufikia maendeleo endelevumatibabu

Mwisho, maendeleo endelevu katika jamii yanapaswa kugusa nyanja muhimu za maendeleo za kijamii,kisiasa,kiuchumi na kitamaduni,matokeo yanayopatikana kupitia nyanja hizi husaidia sana katika kuboresha hali za maisha ya wananchi katika kupata elimu bora ,maji safi na salama pamoja na matibabu ya kiafya. Katika kutumia afya Kama sehemu ya kuleta maendeleo endelevu nchini serikali haina budi kuweka Sera na mipango madhubuti itayoweza kusimamia Sera na mipango hiyo itakayoweza kuongeza ufanisi katika utendaji wa sekta ya afya nchini katika kuimarisha afya za wananchi wake dhidi ya magonjwa, hivyo kuimarishwa kwa afya za watu nchini kunachochoea sana maendeleo ya uchumi nchini na kipato kwa mtu mmoja mmoja katika kuondokana na hali ya utegemezi kwa watu wengine katika kuendesha maisha yake.

Hivyo basi ili kufikia maendeleo endelevu nchini hakuna budi kwa kila mwananchi kutunza na kukinga afya yake dhidi ya magonjwa mbalimbali yatayoweza kuathiri afya za watu na kushindwa kusimamia maendeleo endelevu kwa manufaa yetu na watoto wetu baadae.
 
Back
Top Bottom